Ufafanuzi wa CHADEMA Kuhusu Maazimio ya Kamati Kuu - Novemba 2013

Ufafanuzi wa CHADEMA Kuhusu Maazimio ya Kamati Kuu - Novemba 2013

Status
Not open for further replies.
Napenda kuchukua nafasi hii adhimu kukipongeza Chama changu Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)—chama makini, chama imara na Chama Tawala 2015—kwa maamuzi sahihi waliyochukua kuwavua nyadhifa baadhi ya wanachama waliothibitika kuwa nyuma ya waraka wa kukichafua na kukivuruga chama. Haya ndiyo maamuzi sahihi (sio magumu kama CCM wanavyoyaita) yanayopaswa kuigwa na vyama vingine vinavyokumbatia wanachama wakorofi wanaovuruga na kuharibu taswira ya vyama vyao.

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilisitisha harakati zake za kuvuana magamba kwa sababu ya kuwagwaya na kuwalinda mafisadi ndani ya chama. Matokeo yake chama chao kimepoteza mwelekeo na mvuto kwa umma wa watanzania. Haya ndiyo madhara ya kuwabeba mafisadi na wasaliti ndani ya CCM. Bwana Nape alitembea nchi nzima akiwananga, kuwatukana na kutishia kuwavua uanachama mapacha watatu (Rostam, Chenge na Lowasa) lakini mwisho wa siku alisitisha zoezi zima na kuwaacha hao virusi waendelee kukivuruga chama, ijapokuwa mmoja wao alizidiwa nguvu na kuamua kuachia ngazi. Lakini bado hili limebaki kuwa doa sugu ndani ya CCM—kulindana na kuogopana kwa kisingizio cha kutokimegua chama kwa kujenga makundi kinzani yenye wafuasi walio na nguvu za kifedha na kifisadi.

CHADEMA hatuogopi kuchukua maamuzi sahihi kuwaadhibu wanachama wowote watakaoonekana kwenda kinyume na Katiba ya chama hata kama wangekuwa na vyeo au nguvu kiasi gani ndani ya chama. Chadema ni chama kinachofuata haki katika kufanya maamuzi kwani wanachama hupewa nafasi ya kusikilizwa kabla ya kuadhibiwa zaidi. Ndio maana chama kimetoa siku 14 kwa wahusika kujitetea kwani wasifukuzwe uanachama kwa makosa waliyoyatenda. Hii ni tofauti na CCM waliotembea Tanzania nzima wakiwatukana mapacha watatu lakini mwishowe wakashindwa kuchukua hatua stahiki kuwaadhibu kwa makosa waliyotenda.

Chama makini, CHADEMA, hakichukui hatua kwa kukurupuka (kama wafanyavyo CCM) kabla ya kuchekecha na kupembua kiyakinifu tuhuma za wahusika ili kuepuka kuchukua maamuzi yasiyotenda haki kwa watuhumiwa. Na tofauti na CCM, CHADEMA haitembei nchi nzima ikiwatukana, kuwananga na kuwadhalilisha wanachama wake wenye makosa bali hufuata taratibu na kanuni za chama katika kutoa maamuzi. Pia naomba ieleweke kwamba wanachama waliopatikana na hatia hawachaadhibiwa na Mbowe, Dr Slaa, Lema, Mnyika au mtu yeyote yule ndani ya chama (kama CCM wanavyotaka kuuaminisha umma wa watanzania) isipokuwa wameadhibiwa na Kamati Kuu—chombo huru kisichomuonea mtu wala kuegemea upande wowote—bali kinachoegemea zaidi katika ushahidi wa tuhuma halisi (sio bandia) na zilizothibitishswa kuhusu mwanachama yeyote yule ndani ya chama. Haya ndiyo yanaitwa maamuzi sahihi.

Natoa wito kwa wahusika kujitetea kwa ukamilifu, bila jazba yoyote, juu ya makosa yanayowakabili na ikibidi wakubali na kutubu na kuahidi kutorudia tena kukisaliti chama na bila kupokea ushauri wowote wa giza (hasa utakaotolewa na upande wa pili—CCM). Lengo la maamuzi yaliyochukuliwa si kumkomoa mtu yoyote isipokuwa ni katika kukiweka chama katika mstari ulionyooka na bila kuyumbushwa na nguvu zozote (halisi au za bandia) kutoka ndani au nje ya chama. Ndio maana imetolewa nafasi kwa wahusika kutoa utetezi wao yakinifu juu ya adhabu iliyotolewa kwao na kwanini wasiadhibiwe zaidi. Hivyo basi, tunatarajia kwamba wahusika watajieleza kwa ufasaha na hatimaye kurejea kukitumikia chama kwa moyo mkujufu na bila kinyongo chochote.
Nawasilisha.
 
ni maamuzi magumu,sahihi na makini

kama tayari ushahidi upo wa kutosha,siku 14 ni muda sahihi kufanya maamuzi chanya kwa mustakabali wa chama na taifa

my take;

pelekeni hoja na ushahidi wenu kwa kamati kuu na si kwa wanahabari na mitandaoni

Thubuutuuu! Hata wewe mkuu ungekubali kujipeleka kirahisi hivyo!?,Nawaomba wanahabari watakao kuwepo siku hiyo wasiwaonee aibu badala yake wawatandike maswali ya kiutu uzima,Na kama hawana waseme tuwachangie kuwapa maswali mapema hata hapahapa jamvini.
 
Hii ni kwa sababu baada ya kuwatimua zitto na wenzake, chama kina muda wa kutibu makovu na kuelewesha wanachama suala halisi kuliko wangewatimua karibu na election, wangekuwa na madhara na muda wa ku-absorb shock usingekuwepo
 
Dr. Slaa amepewa adhabu gani kwa

1. kujikopesha pesa za ruzuku kwa matumizi yake binafsi?

2. Kumlipa Josephine Mushumbusi mamilioni kwa kazi anayooita ya kujitolea?

3. Kutumia rasilimali za chama kumtuma Josephine Mushumbusi kujenga mtandao wa Slaa mikoani?

haikuhusu takataka wewe kavuaneni magamba......yenu yamewashinda mnataka ya chadema mtayaweza? umbwa wewe.....
 
Tutaendelea kuwavua uongozi na hata ikibidi uanachama wale wote watakaothibitika bila shaka kwamba kwa namna moja ama nyingine wamekisaliti chama,wanakisaliti chama ama wanapanga kukisaliti chama,na mimi niseme tu ,waendelee kuvuliwa nyazifa zao na ikibidi hata uanachama kwa maana hatuna namna nyingine zaidi ya kufanya hivyo ,ikiwa wao watajiona ndo bora zaidi,wazalendo zaidi,wanauchungu wa chama zaidi,wanastahili kuwa viongozi zaidi na wanaweza kushirikiana na serikali na magamba ya CCM huku wakiwa wapinzani,me niombe tu kwa kusisitiza CHADEMA kiendelee na moto huhuu ,kwa maana safari yetu ya kumtoa CCM ilikuwa ngumu zaidi nyuma na ngumu kidogo sasa,hivo hatuwezi kukubali kikundi cha watu wachache wenye malengo yao watuvuruge ama kutukatisha tamaa kwa ajili ya ujinga wao,taifa linaihitaji CDM zaidi kuliko wakati wowote ule.
M4C DAIMA

  • A%20S%20103.gif

Subject:
Fw: kazi nzuri
Date:
Sunday, November 17, 2013 20:28
From:
" Mwigulu Nchemba " <shimbi85@ gmail.com> >
To:
Emmanuel Nchimbi < [email protected]>
On Sunday, November 17, 2013 6:15:44 PM, Mwigulu Nchemba <shimbi85@ gmail.com> wrote:
sawa boss,,jumatano saa moja imekaa safi kabisa. tuchape kazi. ntakupa update nikitoka kuonana na zzk. mh. Lukuvi namtafuta punde
MN
2013/11/17 Emmanuel Nchimbi < [email protected]>
bila shaka vijana wamefanya kazi nzuri sana. mapambano yanaendelea, hakuna kulala, hapa sasa tume lote livunjwe na huyo waryoba apumzishwe. mtafute mh. Lukuvi ana mazuri ya kuongea na wewe. kuna mapya pale ufipa, nimeshaongea na mh. zitto na amenipa brifieing .. tukutane jumatano basi jioni ya saa1 pale pale cheer,, Emma
Sent from my ipad
On Sunday, November 17, 2013 5:55:02 PM, Mwigulu Nchemba <shimbi85@ gmail.com> wrote:
Naona vijana wametekeleza shuguli vizuri, na cham imewakilishwa vizuri sana. Msangi jembe, sasa tutaipata katiba tunayoitaka hicho kikwazo kikishaondolewa bila shuruti. Alafu upande wa pili (cdm) inabidi tuongeze dau ili shujaa zzk abakie ndani, nasikia kuna mkakati wa kumtoa kwenye kinyang'anyiro. tujitahidi sana sana kumsaidia kujenga mtandao wa ndani apate u wenyekiti. taarifa zaidi za ndani zinasema wkamba wanajaribu kumfukuza kabla ya mwisho wa mwaka, tuendeleze vita hilo lisitokee, naona kundi ndani ya bavicha hasa hiyo mitoto inafanya sana mashambulizi lakini hawataweza. inabidi wadhibitiwe. rockup wiki mbili itawasambaratisha. Tuongeze kasi kwa wajumbe wa kamati kuu. wengi wao ni njaa sana nazani 5mil kila moja inatosha kabisa.wananifata sana kuomba hela ili wasaidie nakutana na ZZK baadae plae pa siku ile, unaweza kufika saa 1 jioni
MN
 
nimeona bwana kama ni kweli hakika kz alikuwa kondoo mwenye ngozi ya mbwa mwitu.
 
Ndugu yangu si kila kitu kutoka kwenye nyaraka kinatolewa kwenye umma. Kuna madhara ya kuwa muwazi sana.

Ndiyo maana kuna msemaji wa maamuzi ya kikao.

Ata vyama vingine hawatoi kila kitu. Vinginevyo utaingia kwenye kashfa ya kuvujisha siri za kikao.

Popote utakapokuwa kuna miiko na maadili yake. Sioni kiashiria cha udini hapa. Wanaosema udini wao ndio wadini.
Swali. Kwa nini watanzania wa leo mnatumia Dini kama kinga?
 
Yuda Isikariote alikuwa karibu na Bwana Yesu na alikuwa ameteuiwa miongoni mwa mitume 12 lakini badala ya kutumia nafasi aliyokabithiwa kwa kupewa heshima juu ya wingi waliokuwa na uwezo kama Yeye alichagua uzisujudia centi na kuamua kumsaliti Bwana pamoja na kazi nzima ya ukombozi. Njia ya usaliti ya Yuda badala ya kuangamiza maono ya ukombozi iliharakisha ukombozi. Yuda alivyoona yaliyotendeka ilimlazimu kwa majuto awarudishie wale waliokuwa wamempa fesha kwa kazi yake ya usaliti, nao wakijua kabisa kuwa ule ujira walimpimia kipimo stahiki kwa kazi yake ya usaliti, hawakutaka hiyo haki ya Yuda na walikataa kuzipokea. Lau kama yuda angetubu historia ingemshuhudia vinginevyo tofauti na sasa maana mlango wa toba kwake ulikuwa wazi kwa maneno ya Bwana Yesu ''baba wasamehe maana hawajui watendalo''. Tanzania tuna ahadi ya ukombozi dhidi ya udhalimu wa serikali ya ciciem iliyochukua nafasi ya farao wa misri kwa raia zake. Lakini kwa kazi kama hii haikosi wasaliti watakao zitamani centi za mafarao kusaliti mageuzi. Hata hivyo wasaliti wameruhusika ili Mungu ajitwalie utukufu baada ya kushinda vizingiti vyote. Yanayotokea Chadema leo ni fundisho la kutukumbusha kwamba kuna mawili ama msaliti atubu usaliti wake kwa kujisahihisha na kuamua kurudi kambini ama (2) msaliti aamue kutokukubali kosa na ajitundike kama Yuda maana ni dhahiri kuwa waliokuwa wakimpa vijicenti kwa kazi ya usaliti hawakubali kuzipokea tena kutoka mikononoi mwake isipookuwa kama watamhurumia sana watamruhusu kuwa miongoni mwa walio katika dust bin lao kama kina T. Hiza, Kaburu, Lamwai nk.
MUNGU IBARIKI CHADEMA ULIYOITUNUKU KULETA UKOMBOZI KUTOKA MIKONONI MWA WAKOLONI WEUSI CCM.
.
 
sijui kwanini ktk characters wote wa Bible Zitto kampenda Yuda Isakriote?Au kwa vile alikimbilia wahi dili ambalo hakuhitajia hata kidogo.Yuda alikimbilia tuu bila sababu dili ambalo by the way Yesu alikuw auwawe tuu.

Zitto alikimbili aujinga tuu ,pengine ni akili ya kutaka kuwa first ktk kila kitu..awe first kufikisha hoja nyepesi zisizokuwa nahitimisho, kuwa Rais wa Kwanza kupitia upinzani etc.

Angesubiri muda wake unefika kabla hata ya akina Jogn Myika kuwa Marais.
 
Re: Kuvuliwa uongozi kwa Zitto; CHADEMA Mmejipangaje kuepuka propaganda za UDINI na Ukanda zidi yenu
Katika hili, "Tuwe werevu kama nyoka lakini wapole kama hua." Tutashinda!

Reply Reply With Quote Send PM
Haki sawa
Today 02:47 #147
JF Senior Expert Member
Array
Join Date : 4th October 2007
Posts : 668
Rep Power : 9404
Likes Received
544
Likes Given
6
Tafsiri ya Udini na Ukanda wa CHADEMA kwa hatua za Kamati Kuu.
Kikao cha Kamati Kuu ya Chadema kilichomalizika juzi na maazimio yake kutangazwa jana kiliamua kuwavua Uongozi wajumbe wa Kamati kuu wawili ambao ni aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu , Mhe .Zitto Kabwe na Dr. Kitila Mkumbo.
Aidha kilimvua madaraka ya uongozi aliyekuwa Mwenyekiti wa Mkoa wa Arusha Samsoni Mwigamba .

Ukiangalia kwa umakini uamuzi huo wa Kamati Kuu utaona kuwa kwa upande wa dini , Ukabila , Mikoa na Ukanda utaona ifuatavyo;

Zitto Kabwe , huyu ni Muislamu, Kanda yake ni Magharibi , Kutoka Mkoa wa Kigoma , Kabila lake ni Muha.....

Dr.Kitila Mkumbo, huyu ni Mkristo, Kanda yake ni ya Kati, Kutoka Mkoa wa Singida, Kabila lake ni Mnyiramba .....

Samsoni Mwigamba, huyu ni Mkristo, kanda yake ni Kaskazini, Mkoa wa Arusha ( ndio alikuwa Mwenyekiti wa Mkoa) , Kabila lake kwa kweli sijui, ila Nina uhakika kuwa huyu sio Muha wala sio Mnyiramba.

Ukafanya uchambuzi ambao sio biased , kwa vyovyote vile utaona kuwa kwa upande wa dini, Muislamu yuko mmoja na Wakristo ni Wawili.Hii ni sawa na kusema kuwa 75% ni Wakristo ndio wamepunguzwa Chadema na 25% ya Waislamu ndio wa epunguzwa kwa maamuzi hayo, huwezi kusema kuwa kulikuwa na ajenda ya kuiumiza dini moja , ila dini iliyoathirika zaidi ni Wakristo kwa kuwa ni asilimia 75% ndio wameathiriwa na maamuzi hayo.

Ukija kwa upande wa Ukanda unakuta kuwa Kanda ya Magharibi imeathirika kwa 33.33% , Kanda ya Kati imeathirika kwa 33.33% na Kanda ya Kasikazini imeathirika kwa 33.33% , hivyo maamuzi hayo haya kufanyiwa kwa misingi ya Ukanda Kwani kila Kanda imeathirika kwa kiwango sawa sawa, huwezi kutoa conclusion kuwa kulikuwa na ajenda ya Ukanda katika maamuzi yaliyofikiwa.

Ukitazama maamuzi hayo kwa Dhana ya Mikoa , utakuta kuwa hakuna Mkoa ambao uliathiriwa kuliko Mkoa mwingine Kwani kila Mkoa umeumia kwa kiwango sawa yaani Singida 33.33%, Arusha 33.33% na Kigoma 33.33% , hivyo unaweza kufikia conclusion kuwa hapakuwa na Mkoa ulipokuwa umelengwa Mahususi , ndio maana maamuzi hayo haya wezi kuitwa yalikuwa ya kuumiza ama kupendelea Mkoa fulani.

Ukiamua kuyatazama maamuzi hayo kwa misingi ya Ukabila unakuta kuwa hapakuwa na Kabila ambalo lililengwa Mahususi, kwani hapakuwa na Kabila moja lililoumia kuliko Kabila lingine , yaani kwa kupoteza idadi kubwa ya wajumbe kwenye vikao vya Chadema .

Hivyo, basi nawataka wale wote ambao wana jengo hoja kuwa uamuzi huu ulikuwa ni kwa misingi ya Ukanda, Udini na au ukabila wathibitishe madai yao kwa facts na sio kwa hoja nyepesi na Propaganda za kizamani kama ambavyo wanafanya kwenye kujenga hoja zao ili Jukwaa hili liweze kuwa na heshima yake ya miaka hiyo .

Aidha, kwa wale ambao tunaamino kuwa maamuzi hayo yalifanywa kwa misingi ya haki na kwa lengo la uwajibikaji,tunaamino kuwa hatua ya Kamati Kuu ilikuwa sahihi nailizingatia merits na sio kwa kutazama jambo lingine lolote lile.

Mwenye hoja unakaribishwa kwa mjadala wa Nguvu ya Hoja na sio Hoja za nguvu , kama unafikiri kuwa IQ yako iko chini please soma subiri wengine wachangie kwa kujenga hoja , Moods zingatieni hoja kwa maslahi ya jukwaa hili.

Thanks, CC, Nguruvi3, Mchambuzi, Mkandara, Mwanakijiji, Mungi, et all.
Alinda and TsafuRD like this.
 
Kitendo cha kuanzisha makundi kutokea kwa akina Kafulila, then akina Mchange, Nyakarungu, Mtela Shonza, then Mwigamba, na Kitila nk yaliyogeuka watukanaji wa viongozi wakubwa ndani ya chama, huku yakitoa siri za chama, Zitto Kabwe afukuzwe, tena mara moja maana hafai hata kuwa mjumbe wa nyumba kumi. Huwezi kuniambia kwa haya yote alikuwa hajui anlichokuwa anafanya. Ameonywa mara kibao, si tu mtandaoni hapa lakini hata ndani ya chama chake ikiwamo kupigiwa kura ya kutokuwa na imani naye kutoka kwa wabunge wenzake. Huyu mtu amechangia sana kuharibu future ya vijana tena wengi kisiasa badala ya kuwa mentor.

Kwa haya tu naunga mkono kutimuliwa regardless ya utetezi
 
Acha hizo zzk amejipambanua, amechangia sana kukua kwa cdm, ndio maana tukio hili limeibua mjadala kitaifa
 
Huyu Zitto ni hatari! Hebu tazama haya mawasiliano kati ya Mwigulu na Waziri Nchimbi!!

Subject: Fw: kazi nzuri
Date: Sunday, November 17, 2013 20:28
From: " Mwigulu Nchemba " <[email protected]> >
To: “Emmanuel Nchimbi” < [email protected] >

On Sunday, November 17, 2013 6:15:44 PM, Mwigulu Nchemba <[email protected]> wrote:

sawa boss,,jumatano saa moja imekaa safi kabisa. tuchape kazi. ntakupa update nikitoka kuonana na zzk. mh. Lukuvi namtafuta punde

MN

2013/11/17 Emmanuel Nchimbi < [email protected] >

bila shaka vijana wamefanya kazi nzuri sana. mapambano yanaendelea, hakuna kulala, hapa sasa tume lote livunjwe na huyo waryoba apumzishwe. mtafute mh. Lukuvi ana mazuri ya kuongea na wewe. kuna mapya pale ufipa, nimeshaongea na mh. zitto na amenipa brifieing .. tukutane jumatano basi jioni ya saa1 pale pale cheer,, Emma

Sent from my ipad

On Sunday, November 17, 2013 5:55:02 PM, Mwigulu Nchemba <[email protected]> wrote:

Naona vijana wametekeleza shuguli vizuri, na cham imewakilishwa vizuri sana. Msangi jembe, sasa tutaipata katiba tunayoitaka hicho kikwazo kikishaondolewa bila shuruti. Alafu upande wa pili (cdm) inabidi tuongeze dau ili shujaa zzk abakie ndani, nasikia kuna mkakati wa kumtoa kwenye kinyang'anyiro. tujitahidi sana sana kumsaidia kujenga mtandao wa ndani apate u wenyekiti. taarifa zaidi za ndani zinasema wkamba wanajaribu kumfukuza kabla ya mwisho wa mwaka, tuendeleze vita hilo lisitokee, naona kundi ndani ya bavicha hasa hiyo mitoto inafanya sana mashambulizi lakini hawataweza. inabidi wadhibitiwe. rockup wiki mbili itawasambaratisha. Tuongeze kasi kwa wajumbe wa kamati kuu. wengi wao ni njaa sana nazani 5mil kila moja inatosha kabisa.wananifata sana kuomba hela ili wasaidie nakutana na ZZK baadae plae pa siku ile, unaweza kufika saa 1 jioni

MN

Endeleeni ila mtaula wa chuya
​
 
Kwa kuamini hizi takataka ni dhahiri kuwa nawe ni akili ndogo,nakushauri...usimeze kila kitu kwani ata waliotunga hili watakuona kichwa maji.
 
mwee alafu nyie na huu upuuzi wenu mtaipeleka nchi matatani maana hapo pana husisha kifo cha mtuu..sasa mtu anakaa kwake anatunga kitu kama hichi anakipeleka mtandaoni SMH
 
Huyu Zitto ni hatari! Hebu tazama haya mawasiliano kati ya Mwigulu na Waziri Nchimbi!!

Subject: Fw: kazi nzuri
Date: Sunday, November 17, 2013 20:28
From: " Mwigulu Nchemba " <[email protected]> >
To: “Emmanuel Nchimbi” < [email protected] >

On Sunday, November 17, 2013 6:15:44 PM, Mwigulu Nchemba <[email protected]> wrote:

sawa boss,,jumatano saa moja imekaa safi kabisa. tuchape kazi. ntakupa update nikitoka kuonana na zzk. mh. Lukuvi namtafuta punde

MN

2013/11/17 Emmanuel Nchimbi < [email protected] >

bila shaka vijana wamefanya kazi nzuri sana. mapambano yanaendelea, hakuna kulala, hapa sasa tume lote livunjwe na huyo waryoba apumzishwe. mtafute mh. Lukuvi ana mazuri ya kuongea na wewe. kuna mapya pale ufipa, nimeshaongea na mh. zitto na amenipa brifieing .. tukutane jumatano basi jioni ya saa1 pale pale cheer,, Emma

Sent from my ipad

On Sunday, November 17, 2013 5:55:02 PM, Mwigulu Nchemba <[email protected]> wrote:

Naona vijana wametekeleza shuguli vizuri, na cham imewakilishwa vizuri sana. Msangi jembe, sasa tutaipata katiba tunayoitaka hicho kikwazo kikishaondolewa bila shuruti. Alafu upande wa pili (cdm) inabidi tuongeze dau ili shujaa zzk abakie ndani, nasikia kuna mkakati wa kumtoa kwenye kinyang'anyiro. tujitahidi sana sana kumsaidia kujenga mtandao wa ndani apate u wenyekiti. taarifa zaidi za ndani zinasema wkamba wanajaribu kumfukuza kabla ya mwisho wa mwaka, tuendeleze vita hilo lisitokee, naona kundi ndani ya bavicha hasa hiyo mitoto inafanya sana mashambulizi lakini hawataweza. inabidi wadhibitiwe. rockup wiki mbili itawasambaratisha. Tuongeze kasi kwa wajumbe wa kamati kuu. wengi wao ni njaa sana nazani 5mil kila moja inatosha kabisa.wananifata sana kuomba hela ili wasaidie nakutana na ZZK baadae plae pa siku ile, unaweza kufika saa 1 jioni

MN

Endeleeni ila mtaula wa chuya
​

Sasa hio ndio ushahidi? Umewezaje kuingia email ya zito au mchemba? Ujinga kutaka kuhalalisha uovu
Hizo email fake nikueekre za kutoka kwa slaa? Si una edit tu email ya kwako unaweka kutoka kwa slaa kwenda kwa mboe na kuiweka hapa ! Cheap propaganda .
Unafikiri rahisi kusoma email za watu? Hao fbi wanatumia billions pamoja na kuwalazimisha yahoo na gmails kutoa paaswrd za watumiaji .itakuwa wewe utuletee upuuzi hapa ?
Kwa ufupi ujumbe na ushauri kwq zitto ni huu

Ushauri .kama zito unaamini uko sahihi usikubali kufanywa kafara kirahisi kwa kujivua uanachama.
Umetumia muda wako na nguvu zako nyingi kukitetea na kukijenga chama chako.
Uwepo wako na umakini na weledi ulionao wa mambo ya siasa umekijenga na kusaidia mwenekano wa chadema usiwe ule wa fujo fujo kwa kuwa mbali na wenye muelekeo hio.
Wengine tunaamini kuwa ni mmoja kati ya viongozi watarajiwa ww nchi hii .
Simama imara kupigana na wale wanaofanya vyama mali yao na familia zao.utaratibu huu ndio unarudisha nyuma democrasia hii ya vyama vingi kumefanya watu wengi kutoamini opposition na kuendelea kwa nguvu za ccm .
Umekua ukipinga mara nyingi chadema kuhusishwa na udini na ukabila lakini kama hilo halipo kama unavo amini basi kunaa tazizo la Udugunazation ambao lazima lipigwe vita.
Simama imara usikubali kuanguka kirahisi .
Kujitoa kutakidhoofisha chadema sana na itakua pigo kubwa kwa siasa za upinzani nchi hii .ulisema umetoka kigoma na hukukimbia ila uliaga hivo tunajua hutakua goi goi kukubali chadema kipotelee kwenye lindi la udini ukabila au udugu dugu
 
Technology haikusubiri wewe na umburura wako ikiwa watu wanaweza kuiba fedha kwenye a/c yako na kadi unayomwenyewe sembuse ki spy e-mail? Acha ushamba kima wewe ,mateka wa Ccm
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom