Ufahamu kuhusu nyota za angani

Ndugu ukitaka kufa mapema tena kwa mawazo changanya sayans na din haijalish ni uislam au ukristo
 
Swali kwako kifyatu,endapo mwezi wetu uje upigwe dhoruba utadondokea wapi?,pia kwa mtazamo wa jua letu,inaonesha mpangilio wa sayari,hivi hakuna sayari zingine ambazo zimemezwa na jua ,na zimo ndani ya jua ila wanasayansi hawazioni kutokana na joto kali,wanashindwa kuchunguza huko?,pia niliwahi soma mabandiko yako, kuwa ulimwengu unakuwa kila siku,unakuwa kivp?pia unaweza kuniambia ni vp nguvu ya nyuklia inavyohusishwa na kutokea kwa ulimwengu?
 
Kifyatu nadhani lumia21 anaongelea cosmos space odyssey2014 ya NEIL DEGRASSE TYSON

Kifyatu baba kwa tathmini yako unamtazamo gani kuhusu uwezekano wa kuwa na ulimwengu(universe) Zaidi ya moja.
Asante kwa elekezo la hiyo Odyssey. Natumaini itawasaidia wengi.

Kama unazungumzia dhana ya MULTIVERSE au universe zaidi ya moja, hii kwa sasa ni dhana tu (theory). Lakini kama ukifahamu kinachotokea ndani ya atoms (Quantum Physics) au Physics ya vitu vidogo unaweza kushangaa mamiujiza (probabilistic nature of existence) yanayotokea huko (sio dhana bali ni kiukweli). Mimi nasubiri wataalam waendelee na utafiti wao waje watujuze lakini sitashangazwa kama kuna universe nyingine zaidi ya hii yetu au kama universe yetu ina pacha wake (Parallel Universe).
 
Swali kwako Kifyatu ni umbali wa km ngapi kutoka duniani ndio utakao kuwezesha kuelea ........................... Sisi (duniani ) tukitaka kwenda sayari au anga za mbali tunakwenda kwa kuelekea juu je na wao kwa mfano mars ( pangekuwa na viumbe ) wangetaka kuja kwetu ( duniani ) wangekuwa wanajielekezaje ???
 
Kwan Mars hakuna viumbe?
 
Kifyatu asante kwa kufyatua ujinga akilini mwangu!
 

Samahani nimechelewa kukujibu.

Mfano: Ukifunga jiwe na kamba halafu ukalizunguusha kwa kasi huku ncha moja ya kamba ukiwa umeishikilia mkononi, lile jiwe litazunguuka katika mduara. Ukiwa kwa mbali (usimuone alieshika kamba na ile kamba) utadhani lile jiwe linaelea angani. Hivyo hivyo, ukiwa unaizunguuka sayari, mwezi au jua kwa kasi maalumu, hutaanguka chini kwa sababu uzito wako (gravity) vinalingana na nguvu inayojaribu kukutupa (centripetal force) mbali na sayari (ndio maana unajisikia kuelea - huna uzito). Hii inaweza kutokea katika umbali wowote ule kutegemea na kasi yako. Kama sayari unayoizunguuka ina hewa, basi ni vema uizunguuke kwenye umbali ambao hewa haipo ama sivyo itaungua kwa msuguano.

Wakati wowote unapoelea angani ina maana uko kwenye orbit ya sayari fulani au jua. Kitu kutoka Mars (mfano jiwe lililogongwa na meteor na likaweza kuepuka gravity ya Mars) linaweza kufika hapa kwetu duniani (na mengi yamefika) kwa kuelea na kwa bahati yakanaswa na gravity yetu.
 
Nyota za rangi rangi ni Pleiadian Motherships. Yaani siyo nyota,ni space vehicles.
 

umenijibu kiasi flani nilikua najiulizaga hiv hao watu wanajuaje kama.mars ipo huko kwann wasikosee wakaenda zuhura hata ila wanajuaje
 
umenijibu kiasi flani nilikua najiulizaga hiv hao watu wanajuaje kama.mars ipo huko kwann wasikosee wakaenda zuhura hata ila wanajuaje
Kuna mahesabu ambayo siyo magumu sana yanayofanya ujue sayari ziko wapi. Vitu vyote angani vinatembea kufuatia kanuni maalum. Hivyo ukizijua hizo kanuni basi utajua lini jua litapatwa au nikitaka kwenda Jupiter niondi=oke lini hapa duniani na nielekee upande gani.
 

unaweza kunitajia mkuu hayo mahesabu nigugo kdg niondoe huu ujinga
 
Napenda kujua kuwa, jua ni nyota inayotuwezesha dunia kuwa na uhai (najua Mungu ndiye anatoa uhai ila naamini nimeeleweka) Je hizo nyota nyingine kuna utafiti uliofanywa ukaonyesha kuwepo uhai kama kwenye nyota jua?
 
Mkuu ivi unaijua nyota sirius kama unaijua inaonekana kwa upande upi apa bongo?

Sirius ni nyota ilioko kwenye Constellation Canis Major (Big Dog). Iko kwenye pua ya huyu mbwa.

Kama unasoma hili jibu sasa nimeweka picha ya Sirius ilipo sasa hivi Tanzania (DSM). Simama nje mwili wako ukiangalia kaskazini. Angalia juu (utosini) na utauona mwezi. Teremsha macho yako kidogo kuelekea kaskazini-magharibi na utaiona nyota moja yenye muanga mkubwa zaidi ya nyingine karibu. Hiyo ndio Sirius.


Kama hukuupata huu ujumbe muda muafaka, nipe siku na muda (usiku) utakapokuwa tayari kutoka nje na kuangalia angani (kusiwe na mawingu) na nitakutumia chart kukuelekeza uangalie wapi. Ukinipa mji itasaidia zaidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…