Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ndugu ukitaka kufa mapema tena kwa mawazo changanya sayans na din haijalish ni uislam au ukristoJamani samahani ndugu zangu wote Mimi mkristo ila na soma sana Quran kujifunza mambo,katika Quran MUNGU MKUU anasema kuna mbingu saba ambazo ameziumba na anasema mbingu ya kwanza ambayo niyakwetu ndio aliyoipamba sana kwa nyote ili hali hizo mbingu sita azijapambwa kama hiii,na Ulikuwa maalumu kwa ajili yetu,pia Mola anasema anaendelea kuujenga kila Siku ulimwengu,kumbuka haya yamezungumzwa kwenye Quran Tukufu ata kabla sayansi ya juu kutambulika je Ina maana tunaposema kuna nyote katika galaxy nyingine tunapingana na MUNGU MKUU!?
Asante kwa elekezo la hiyo Odyssey. Natumaini itawasaidia wengi.
Kwan jua sio nyota?NYOTA ni kama jua lakini ziko mbali sana na dunia kushinda jua.NYOta ni kubwa kushinda jua.
Kwan Mars hakuna viumbe?Swali kwako Kifyatu ni umbali wa km ngapi kutoka duniani ndio utakao kuwezesha kuelea ........................... Sisi (duniani ) tukitaka kwenda sayari au anga za mbali tunakwenda kwa kuelekea juu je na wao kwa mfano mars ( pangekuwa na viumbe ) wangetaka kuja kwetu ( duniani ) wangekuwa wanajielekezaje ???
Kifyatu asante kwa kufyatua ujinga akilini mwangu!Haya, BISMILLAH.
Nyota ni nini?
Nyota ni kama jua letu, lakini ziko mbali sana.
Nyota ziko mbali kiasi gani?
Mwanga unasafiri kwa kasi (speed) ya 299,793 km/sekunde au 1,079 milioni km/saa. Mara nyingi umbali wa nyota hupimwa kwa muda utakaotumiwa na mwanga kusafiri mpaka kutufikia sisi. Kwa mfano, mwanga kutoka jua letu unasafiri kwa takriban dakika 8 hivi kutufikia sisi (au, jua liko umbali wa 8 light-minutes kutoka hapa duniani). Nyota iliyo karibu sana na sisi ni ile iitwayo alpha-Centauri (kwenye constellation ya Centaurus) ambayo iko umbali wa 4.4 light-years kutoka hapa (mwanga kutoka alpha-centauri huchukua miaka 4.4 kutufikia) ndio maana nyota zinaonekana ndogo sana ukifananisha na nyota yetu (jua) hapa duniani. Jua letu ni moja ya nyota ndogo sana. Kuna mizinga ya nyota kama Betelgeuse (kwenye Constellation ya Orion) ambayo ina ukubwa wa majua yetu 1,000 na iko umbali wa 643 light-years kutoka hapa.
Chanzo cha mwanga wa nyota.
Nyota zote (pamoja na jua letu) zinatoa mwanga, joto, na nishati nyingine kutokana na nguvu za nyuklia aina ya fusion. Fusion inachukua atom mbili za hewa ya hydrogen na kuziunganisha ili kutengeneza atom moja ya hewa ya Helium. Uzito wa zile atom mbili za hydrogen ni mkubwa kuliko uzito wa atom ya helium iliyotengenezwa. Hii tofauti ya uzito "m" haipotei bali hubadilika kuwa nishati (E) kufuatia kanuni ya mkulu Albert Einstein kuwa E=mC2. Hii C ni ile kasi (speed) ya mwanga tuliyozungumzia hapo juu.
(Nguvu za nyuklia pia zinaweza kupatikana kwa kupasua (Fission) atom nzito kama za Urani (Uranium). Njia hii inatumika kwenye mitambo ya nyuklia inayozalisha umeme, mabomu, nk. Njia hii ya fission ni less efficient kuliko ile inayotokea kwenye jua kupitia fusion.)
Kwa kuwa nyota zote zina ujazo mkubwa sana wa hewa ya hydrogen, inachukua mabilioni ya miaka kuimaliza hii hydrogen. Kwa hiyo usiwe na wasiwasi, jua letu litaendelea kuwaka kwa mabilioni mengine ya miaka.
Rangi ya nyota nyingine kubadilika badilika (Nyekundu/bluu)
Nyota nyingi ziko moja moja, kama jua letu. Lakini kuna nyota nyingine zinakuwa pacha (mbili karibu karibu au Binary-stars). Zikiwa hivi basi zina-spin. Sisi hapa duniani tukiziangalia tunachoona ni matokeo ya hii spin (naomba mtu anisaidie maana ya spin).
Wakati moja ya hizi nyota ikiwa inakuja kwetu mwanga wake unaonekana kama una wave-length fupi (wave-length ya rangi ya bluu.) Ile nyota inayo tukimbia mwanga wake unaonekana kama una wave-length ndefu (wave-length ya rangi nyekundu). Hali hii inafanya tuone nyota ina-twinkle na rangi mbili, nyekundu na bluu. Hii inajulikana kama Doppler-effect iliyogunduliwa na mwanasayansi Christian Doppler mwaka 1842 alipowasilisha mada yake kwenye kongamano huko Prague kuhusu hizi binary-stars na rangi zake (alikuwa ni Astro-Physicist Kutoka Austria).
Nawasilisha.
I am sorry if this is an overkill.
Swali kwako Kifyatu ni umbali wa km ngapi kutoka duniani ndio utakao kuwezesha kuelea ........................... Sisi (duniani ) tukitaka kwenda sayari au anga za mbali tunakwenda kwa kuelekea juu je na wao kwa mfano mars ( pangekuwa na viumbe ) wangetaka kuja kwetu ( duniani ) wangekuwa wanajielekezaje ???
Siyo chuo kikuu tu tena anafanya masters.
Samahani nimechelewa kukujibu.
Mfano: Ukifunga jiwe na kamba halafu ukalizunguusha kwa kasi huku ncha moja ya kamba ukiwa umeishikilia mkononi, lile jiwe litazunguuka katika mduara. Ukiwa kwa mbali (usimuone alieshika kamba na ile kamba) utadhani lile jiwe linaelea angani. Hivyo hivyo, ukiwa unaizunguuka sayari, mwezi au jua kwa kasi maalumu, hutaanguka chini kwa sababu uzito wako (gravity) vinalingana na nguvu inayojaribu kukutupa (centripetal force) mbali na sayari (ndio maana unajisikia kuelea - huna uzito). Hii inaweza kutokea katika umbali wowote ule kutegemea na kasi yako. Kama sayari unayoizunguuka ina hewa, basi ni vema uizunguuke kwenye umbali ambao hewa haipo ama sivyo itaungua kwa msuguano.
Wakati wowote unapoelea angani ina maana uko kwenye orbit ya sayari fulani au jua. Kitu kutoka Mars (mfano jiwe lililogongwa na meteor na likaweza kuepuka gravity ya Mars) linaweza kufika hapa kwetu duniani (na mengi yamefika) kwa kuelea na kwa bahati yakanaswa na gravity yetu.
Kuna mahesabu ambayo siyo magumu sana yanayofanya ujue sayari ziko wapi. Vitu vyote angani vinatembea kufuatia kanuni maalum. Hivyo ukizijua hizo kanuni basi utajua lini jua litapatwa au nikitaka kwenda Jupiter niondi=oke lini hapa duniani na nielekee upande gani.umenijibu kiasi flani nilikua najiulizaga hiv hao watu wanajuaje kama.mars ipo huko kwann wasikosee wakaenda zuhura hata ila wanajuaje
Kuna mahesabu ambayo siyo magumu sana yanayofanya ujue sayari ziko wapi. Vitu vyote angani vinatembea kufuatia kanuni maalum. Hivyo ukizijua hizo kanuni basi utajua lini jua litapatwa au nikitaka kwenda Jupiter niondi=oke lini hapa duniani na nielekee upande gani.
Ilm hiyo mkuu hujulikana kama "Celestial Mechanics"unaweza kunitajia mkuu hayo mahesabu nigugo kdg niondoe huu ujinga
Ilm hiyo mkuu hujulikana kama "Celestial Mechanics"
Nyota za rangi rangi ni Pleiadian Motherships. Yaani siyo nyota,ni space vehicles.
Ilm hiyo mkuu hujulikana kama "Celestial Mechanics"
Mkuu ivi unaijua nyota sirius kama unaijua inaonekana kwa upande upi apa bongo?