Ufahamu kuhusu nyota za angani

Mkuu Kifyatu mie naomba nikuulize hii kitu nilijaribu kuuliza humu sikuweza kupata jibu sahihi.

Kwa mfano mwezi huu tarehe 1 ilitokea kupatwa kwa jua sasa ninachojiuliza kama dunia ipo katika njia yake ile ile kuizunguka dunia na IPO katika njia yake kwa maana ya speed ile ile kijuzungusha kama ilivyo kwa mwezi kuizunguka dunia kwanini hii kupatwa kwa jua isiwe inajirudia Kila mwaka kwa maana hakuna kitu kinachohama kwenye njia yake?

Na kwanini kupatwa kwa jua kama vile iwe Kila baada ya miaka 15±?
 
mkuu kipindi hiki ikifika jionimida yasaa1hadi saa 2 upande wa jua linapozama kuna 'nyota' kubwa sana inang'aa je itakua ndio jupiter ua?
Mkuu "nyota" unaoiona jioni sio nyota ni sayari ya VENUS.

Jupiter kwa sasa huwezi kuiona kwa sababu iko karibu sana na jua. Unaweza kuiona Jupiter kama tu kutakuwa na kupatwa kwa jua (total sun eclipse) nyingine.
 
Mkuu "nyota" unaoiona jioni sio nyota ni sayari ya VENUS.

Jupiter kwa sasa huwezi kuiona kwa sababu iko karibu sana na jua. Unaweza kuiona Jupiter kama tu kutakuwa na kupatwa kwa jua (total sun eclipse) nyingine.
na ile inayoonekanaga alfajiri wanayoiita nyota ya asubuhi ni ipi mkuu?
 
 
Kwa wapenz wa mipangilio ya sayari na jua na miezi na constellation mbali mbali angani download app Inaitwa star walk 2. Inakuonesha mpangilio Wajua ba sayari zake kwa wakati husika...we unachofanya unaweka simu yako angani then inakuletea anga ilivyojipanga!...
Itasaidia kujua nyota gan zipo angani kwa muelekeo gan!
 
pia mkuu ungegusia uhusiano wa constellation sagittarius na katikati ya milkway yetu(black hole)
Kwa sasa hivi BLACK-HOLE letu liko muelekeo wa constellations za Sagittarius na Scorpio. Kwa Tanzania, mitaa ya saa 12 jioni (wakati unaiona Venus inawaka sana Magharibi) basi ukiangalia utosini kwako ndipo Saggitarius ilipo na ndio muelekeo lilipo Black hole letu.
 

Nimeipata mkuu.

Thanks. [emoji1417]
 
Swali zuri sana hili.

Cha kwanza kufahamu ni kuwa kupatwa kwa jua hutokea mwezi ukiwa mchanga (ukiwa karibu na jua), na kupatwa kwa mwezi hutokea wakati mwezi ni full moon (mbali kabisa na jua).

Kitu kingine cha kufahamu ni kuwa jua linapatwa kila mwezi (mwezi mchanga). Kinachotokea ni kuwa hiki kivuli cha mwezi kama hakiangukii ardhini basi sisi hatuoni kuwa jua limepatwa.

Kama dunia invyozunguuka katika mhimili wake basi ukichora msitari kati ya jua na mwezi, huu mstari sio siku zote unaigusa dunia yetu. Ni pale tu myumbo wa dunia utakapoiweka iguswe na huu mstari ndipo eclipse inapotokea.

Hii inatokana na kuwa kama ukichora bapa (au plane) ya dunia inavyolizunguuka jua, na ukichora plane ya mwezi inavyoizunguuka dunia, hizi planes mbili sio sawa. Ni nyakati chache tu ndio kivuli cha mwezi kinapoweza kuangukia duniani na tunaweza kuzitabiri hizi tarehe za eclipses.
 
Nimeipata mkuu.

Thanks. [emoji1417]
Ahsante mkuu!!,technology Inafanya mambo mengi yanakuwa mepesi!
Kwa kutumia hiyo inaweza kuvuta sayari kwa ukaribu kwa kutumia technologia ya 3D na sayari ambazo zina miezi yake unaona vzr!
Japo kuna ingine ya solar system yetu peke yake Inaitwa solar walk lite....nzuri kwa kumfahamu kuhusu solar system yetu
Neo1.
 

Mkuu tuna bahati sana kizazi cha leo. Elimu na technology vinatuzunguka tu. We can learn anything.

[emoji3]
 
Asante Mkuu nimekupata vizuri
 
Eeehhhh hahahahahaha hii umeipatia wap mkuu.
 
Mkuu Kifyatu je kuna possibility ya kukamatwa kwa Jupiter??,
I mean siku Jua,Jupiter na dunia zikiwa aligned pamoja??
Hilo tukio linategemea kuchukua muda gan??,
Kama possible hilo tukio linategemea kutokea mwaka gan??
 
Mkuu Kifyatu je kuna possibility ya kukamatwa kwa Jupiter??,
I mean siku Jua,Jupiter na dunia zikiwa aligned pamoja??
Hilo tukio linategemea kuchukua muda gan??,
Kama possible hilo tukio linategemea kutokea mwaka gan??
Kivuli cha dunia yetu kwenye uso wa Jupiter ni kidogo sana hivyo huwezi kukiona. Ni sawasawa na wewe utumie unyasi kujiziba na jua (au ndege, satelites, nk hupita mbele ya jua lakini vivuli vyao ni vidogo kuliziba jua). Mfano Mercury mara nyingi tu inapita mbele ya jua lakini hatuoni kama ni kupatwa. Ukiwa na darubini pamoja na filters maalum unaweza kuona kidoti cha Mercury au hata Venus kikipita mbele ya uso wa jua.

Jupiter kwa sasa iko karibu sana na jua na kama mwezi mmoja uliopita ilikuwa karibu sambamba na jua lakini sisi hatukuona jua kupatwa kwa sababu ilikuwa kama kidoti tu kwenye jua. Hivi karibuni tutaiona Jupiter kama nyota nyingine ya asubuhi karibu na Mercury lakini kamwe haiwezi kuliziba jua.

Mwezi unaliziba jua kwa sababu, kutokana na umbali wake toka hapa duniani, mduara wake unalingana na ule wa jua na ndio maana unaweza kuliziba jua kabisa.

Sijui kama nimelijibu swali lako lakini limetoa insight nzuri sana kuhusu eclipses.
 
Mkuu Kifyatu kuna chombo kilitumwa Jupiter kinategemewa kuwepo kwa miezi 18 toka kimefika huko!!.
Nini wanategemea kugundua toka kwenye icho chombo...
Kwa nini ni mission ya miezi 18 wakati chombo kimetumia miaka 4 kusafiri toka Duniani mpaka Jupiter???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…