The Transporter
JF-Expert Member
- Aug 26, 2016
- 3,580
- 7,203
Mkuu Kifyatu mie naomba nikuulize hii kitu nilijaribu kuuliza humu sikuweza kupata jibu sahihi.Goldilocks (yule mtoto wa kike aliepotea mwituni na kuingia kwenye pango la madubu au bears -- hadithi ya watoto wa shule za vidudu) zone ni zone ya kawaida (average zone). Katika universe kuna sehemu zenye extremes conditions (kama joto kali sana au baridi kali sana au gravity kubwa kama za blackholes) ambako uhai (kama wetu) hauwezi kushamiri. Lakini kuna sehemu chache (kama dunia yetu) ambako hali yake ni ya wastani (just right) kwa maisha kama yetu. Katika solar system yetu mpaka sasa bado hatujaona sehemu nyingine inayoweza ku-support maisha (kama yetu) isipokuwa hapa duniani kwetu - na pengine Mars. Hizi space missions nyingi zinatumwa kuona kama kuna sehemu nyingine tunakoweza kuishi.
Mimi naamini kuwa katika hii universe yetu yenye utitiri wa galaxies, nyota, na sayari ni lazima (law of probabilities) kutakuwa na sehemu nyingi tu zenye maandhari kama ya hapa duniani kwetu. Ni muda tu tunaohitaji kupaona.
Kuna Goldilocks Zones za aina ngapi?
Uwepo wa maisha lazima tuuangalie kwa mtazamo mwingine. Inawezekana kabisa kuna maisha katika sehemu nyingine kwenye hii solar system yetu (au kwengine) lakini sio kama maisha yetu sisi (carbon-based). Inawezekana kabisa kwamba kuna viumbe wengine wa aina tofauti (labda ni silicone-based au based on elements nyingine). Tumesikia riwaya za majini, aliens, n.k., wanaoonekana katika nyakati na mazingara tofauti. Kama hii ni kweli basi hizi Goldilocks zone zipo nyingi za aina tofauti (zone ya sisi binadamu, zone ya majini, n.k.).
Tukipanua uga wa kutafsiri maisha ni nini au ni kitu gani basi tunaweza kushangaa kuona kumbe kuna viumbe wa aina nyingi tu (na wengine tunaishi nao bali hatuwaoni tu) hapa duniani, solar system yetu, na universe.
Hapa ndipo panapoleta utamu wa sayansi.
Kwa mfano mwezi huu tarehe 1 ilitokea kupatwa kwa jua sasa ninachojiuliza kama dunia ipo katika njia yake ile ile kuizunguka dunia na IPO katika njia yake kwa maana ya speed ile ile kijuzungusha kama ilivyo kwa mwezi kuizunguka dunia kwanini hii kupatwa kwa jua isiwe inajirudia Kila mwaka kwa maana hakuna kitu kinachohama kwenye njia yake?
Na kwanini kupatwa kwa jua kama vile iwe Kila baada ya miaka 15±?