Ufahamu kuhusu nyota za angani

Ufahamu kuhusu nyota za angani

Goldilocks (yule mtoto wa kike aliepotea mwituni na kuingia kwenye pango la madubu au bears -- hadithi ya watoto wa shule za vidudu) zone ni zone ya kawaida (average zone). Katika universe kuna sehemu zenye extremes conditions (kama joto kali sana au baridi kali sana au gravity kubwa kama za blackholes) ambako uhai (kama wetu) hauwezi kushamiri. Lakini kuna sehemu chache (kama dunia yetu) ambako hali yake ni ya wastani (just right) kwa maisha kama yetu. Katika solar system yetu mpaka sasa bado hatujaona sehemu nyingine inayoweza ku-support maisha (kama yetu) isipokuwa hapa duniani kwetu - na pengine Mars. Hizi space missions nyingi zinatumwa kuona kama kuna sehemu nyingine tunakoweza kuishi.

Mimi naamini kuwa katika hii universe yetu yenye utitiri wa galaxies, nyota, na sayari ni lazima (law of probabilities) kutakuwa na sehemu nyingi tu zenye maandhari kama ya hapa duniani kwetu. Ni muda tu tunaohitaji kupaona.

Kuna Goldilocks Zones za aina ngapi?
Uwepo wa maisha lazima tuuangalie kwa mtazamo mwingine. Inawezekana kabisa kuna maisha katika sehemu nyingine kwenye hii solar system yetu (au kwengine) lakini sio kama maisha yetu sisi (carbon-based). Inawezekana kabisa kwamba kuna viumbe wengine wa aina tofauti (labda ni silicone-based au based on elements nyingine). Tumesikia riwaya za majini, aliens, n.k., wanaoonekana katika nyakati na mazingara tofauti. Kama hii ni kweli basi hizi Goldilocks zone zipo nyingi za aina tofauti (zone ya sisi binadamu, zone ya majini, n.k.).

Tukipanua uga wa kutafsiri maisha ni nini au ni kitu gani basi tunaweza kushangaa kuona kumbe kuna viumbe wa aina nyingi tu (na wengine tunaishi nao bali hatuwaoni tu) hapa duniani, solar system yetu, na universe.

Hapa ndipo panapoleta utamu wa sayansi.
Mkuu Kifyatu mie naomba nikuulize hii kitu nilijaribu kuuliza humu sikuweza kupata jibu sahihi.

Kwa mfano mwezi huu tarehe 1 ilitokea kupatwa kwa jua sasa ninachojiuliza kama dunia ipo katika njia yake ile ile kuizunguka dunia na IPO katika njia yake kwa maana ya speed ile ile kijuzungusha kama ilivyo kwa mwezi kuizunguka dunia kwanini hii kupatwa kwa jua isiwe inajirudia Kila mwaka kwa maana hakuna kitu kinachohama kwenye njia yake?

Na kwanini kupatwa kwa jua kama vile iwe Kila baada ya miaka 15±?
 
c6d481443f39a591e4c3772d35fd3154.jpg

Hiyo ni Nyota ikiwa katika hatua ya kufa taratibu baada ya kupasuka kutokana na kuisha kwa fuel.

Picha imepigwa mwezi huu September, 2016. NASA - Hubble Views a Colorful Demise of a Sun-like Star.

Source: http://www.nasa.gov/image-feature/goddard/2016/hubble-views-a-colorful-demise-of-a-sun-like-star
 
mkuu kipindi hiki ikifika jionimida yasaa1hadi saa 2 upande wa jua linapozama kuna 'nyota' kubwa sana inang'aa je itakua ndio jupiter ua?
Mkuu "nyota" unaoiona jioni sio nyota ni sayari ya VENUS.

Jupiter kwa sasa huwezi kuiona kwa sababu iko karibu sana na jua. Unaweza kuiona Jupiter kama tu kutakuwa na kupatwa kwa jua (total sun eclipse) nyingine.
 
na ile inayoonekanaga alfajiri wanayoiita nyota ya asubuhi ni ipi mkuu?
 
halafu ningependa ugusie na constellation canis major kuna nyota yaitwa sirius inang'aa sana kuliko ile 'giant' VY sasa ipi ni kubwa hapo?[/ QUOTE]

Kwenye post zangu za nyuma nilizungumzia hii constellation ya Canis Major (Big Dog) na nyota Sirius.

Sirius ndio nyota inayong'aa sana katika anga letu kwa sababu ipo karibu nasi (8.6 light years) lakini mwanga wake ni mara 25 tu ya mwanga wa jua letu.

VY ni mzinga wa nyota katika constellation hiyo hiyo ya Canis Major. Radius yake ni sawa na ya jua letu mara 1,450. Mwanga na mwanga wake ni mara 270,000 ya mwanga wa jua letu. Lakini kwa sababu ipo mbali sana (3,900 light years kutoka hapa kwetu) basi mwanga wake kwenye anga letu unazidiwa na ule wa Sirius.
 
Kwa wapenz wa mipangilio ya sayari na jua na miezi na constellation mbali mbali angani download app Inaitwa star walk 2. Inakuonesha mpangilio Wajua ba sayari zake kwa wakati husika...we unachofanya unaweka simu yako angani then inakuletea anga ilivyojipanga!...
Itasaidia kujua nyota gan zipo angani kwa muelekeo gan!
 
pia mkuu ungegusia uhusiano wa constellation sagittarius na katikati ya milkway yetu(black hole)
Kwa sasa hivi BLACK-HOLE letu liko muelekeo wa constellations za Sagittarius na Scorpio. Kwa Tanzania, mitaa ya saa 12 jioni (wakati unaiona Venus inawaka sana Magharibi) basi ukiangalia utosini kwako ndipo Saggitarius ilipo na ndio muelekeo lilipo Black hole letu.
 
Kwa wapenz wa mipangilio ya sayari na jua na miezi na constellation mbali mbali angani download app Inaitwa star walk 2
Inakuonesha mpangilio Wajua ba sayari zake kwa wakati husika...we unachofanya unaweka simu yako angani then inakuletea anga ilivyojipanga!...
Itasaidia kujua nyota gan zipo angani kwa muelekeo gan!

Nimeipata mkuu.

Thanks. [emoji1417]
 
Mkuu Kifyatu mie naomba nikuulize hii kitu nilijaribu kuuliza humu sikuweza kupata jibu sahihi,
Kwa mfano mwezi huu tarehe 1 ilitokea kupatwa kwa jua sasa ninachojiuliza kama dunia ipo katika njia yake ile ile kuizunguka dunia na IPO katika njia yake kwa maana ya speed ile ile kijuzungusha kama ilivyo kwa mwezi kuizunguka dunia kwanini hii kupatwa kwa jua isiwe inajirudia Kila mwaka kwa maana hakuna kitu kinachohama kwenye njia yake?
Na kwanini kupatwa kwa jua kama vile iwe Kila baada ya miaka 15±?
Swali zuri sana hili.

Cha kwanza kufahamu ni kuwa kupatwa kwa jua hutokea mwezi ukiwa mchanga (ukiwa karibu na jua), na kupatwa kwa mwezi hutokea wakati mwezi ni full moon (mbali kabisa na jua).

Kitu kingine cha kufahamu ni kuwa jua linapatwa kila mwezi (mwezi mchanga). Kinachotokea ni kuwa hiki kivuli cha mwezi kama hakiangukii ardhini basi sisi hatuoni kuwa jua limepatwa.

Kama dunia invyozunguuka katika mhimili wake basi ukichora msitari kati ya jua na mwezi, huu mstari sio siku zote unaigusa dunia yetu. Ni pale tu myumbo wa dunia utakapoiweka iguswe na huu mstari ndipo eclipse inapotokea.

Hii inatokana na kuwa kama ukichora bapa (au plane) ya dunia inavyolizunguuka jua, na ukichora plane ya mwezi inavyoizunguuka dunia, hizi planes mbili sio sawa. Ni nyakati chache tu ndio kivuli cha mwezi kinapoweza kuangukia duniani na tunaweza kuzitabiri hizi tarehe za eclipses.
 
Nimeipata mkuu.

Thanks. [emoji1417]
Ahsante mkuu!!,technology Inafanya mambo mengi yanakuwa mepesi!
Kwa kutumia hiyo inaweza kuvuta sayari kwa ukaribu kwa kutumia technologia ya 3D na sayari ambazo zina miezi yake unaona vzr!
Japo kuna ingine ya solar system yetu peke yake Inaitwa solar walk lite....nzuri kwa kumfahamu kuhusu solar system yetu
Neo1.
 
Mkuu tuna bahati sana kizazi cha leo. Elimu na technology vinatuzunguka tu. We can learn anything.

[emoji3]
 
Swali zuri sana hili.

Cha kwanza kufahamu ni kuwa kupatwa kwa jua hutokea mwezi ukiwa mchanga (ukiwa karibu na jua), na kupatwa kwa mwezi hutokea wakati mwezi ni full moon (mbali kabisa na jua).

Kitu kingine cha kufahamu ni kuwa jua linapatwa kila mwezi (mwezi mchanga). Kinachotokea ni kuwa hiki kivuli cha mwezi kama hakiangukii ardhini basi sisi hatuoni kuwa jua limepatwa.

Kama dunia invyozunguuka katika mhimili wake basi ukichora msitari kati ya jua na mwezi, huu mstari sio siku zote unaigusa dunia yetu. Ni pale tu myumbo wa dunia utakapoiweka iguswe na huu mstari ndipo eclipse inapotokea.

Hii inatokana na kuwa kama ukichora bapa (au plane) ya dunia inavyolizunguuka jua, na ukichora plane ya mwezi inavyoizunguuka dunia, hizi planes mbili sio sawa. Ni nyakati chache tu ndio kivuli cha mwezi kinapoweza kuangukia duniani na tunaweza kuzitabiri hizi tarehe za eclipses.
Asante Mkuu nimekupata vizuri
 
nyota ni ndogo sana kuliko dunia, ni kama mwezi. zinategemea mwanga wa jua. na nyota ulizoona zinazobadilika kutoka rangi kutokea ya blue kwenda ya kijani ni kutokana na kuzibwa na miti na bahari .na ukiona nyekundu ujue hapo kuna radi na mvua inanyesha.
Eeehhhh hahahahahaha hii umeipatia wap mkuu.
 
Mkuu Kifyatu je kuna possibility ya kukamatwa kwa Jupiter??,
I mean siku Jua,Jupiter na dunia zikiwa aligned pamoja??
Hilo tukio linategemea kuchukua muda gan??,
Kama possible hilo tukio linategemea kutokea mwaka gan??
 
Kivuli cha dunia yetu kwenye uso wa Jupiter ni kidogo sana hivyo huwezi kukiona. Ni sawasawa na wewe utumie unyasi kujiziba na jua (au ndege, satelites, nk hupita mbele ya jua lakini vivuli vyao ni vidogo kuliziba jua). Mfano Mercury mara nyingi tu inapita mbele ya jua lakini hatuoni kama ni kupatwa. Ukiwa na darubini pamoja na filters maalum unaweza kuona kidoti cha Mercury au hata Venus kikipita mbele ya uso wa jua.

Jupiter kwa sasa iko karibu sana na jua na kama mwezi mmoja uliopita ilikuwa karibu sambamba na jua lakini sisi hatukuona jua kupatwa kwa sababu ilikuwa kama kidoti tu kwenye jua. Hivi karibuni tutaiona Jupiter kama nyota nyingine ya asubuhi karibu na Mercury lakini kamwe haiwezi kuliziba jua.

Mwezi unaliziba jua kwa sababu, kutokana na umbali wake toka hapa duniani, mduara wake unalingana na ule wa jua na ndio maana unaweza kuliziba jua kabisa.

Sijui kama nimelijibu swali lako lakini limetoa insight nzuri sana kuhusu eclipses.
 
Mkuu Kifyatu kuna chombo kilitumwa Jupiter kinategemewa kuwepo kwa miezi 18 toka kimefika huko!!.
Nini wanategemea kugundua toka kwenye icho chombo...
Kwa nini ni mission ya miezi 18 wakati chombo kimetumia miaka 4 kusafiri toka Duniani mpaka Jupiter???
 
Back
Top Bottom