Ufahamu kuhusu nyota za angani

Umenipa somo baaabu kubwa,kwahiyo tuseme kwa vizazi hivi vya sasa hatutashuhudia binadamu kwenda nje ya solar system yetu.
 
Umenipa somo baaabu kubwa,kwahiyo tuseme kwa vizazi hivi vya sasa hatutashuhudia binadamu kwenda nje ya solar system yetu.
Kwa sasa hatuweza kushuhudia tatizo kubwa ni kwamba mtu hawezi kupona na hizo radiation zilizopo kwenye outer space na vile vile chance ya kurudi duniani ni ndogo sana na wakiwa kwenye hicho chombo wanaweza kuwa machizi sababu watakuwa wamekaa sehemu moja ndogo kwa muda mrefu

Ila kupeleka chombo peke yake mpaka sasa hivi tumeweza kuna chombo kinaitwa voyager 1 and voyager 2 vimeishika toka nje ya solar system yetu, vilipelekwa angani mwaka 1977 na vitaendelea na safari mpaka itakapofika mwaka 2025,vimeisha tembea billions of kilometres kuna kipindi viliiona dunia kama kidoti kidogo cha blue, ila kwa sasa sidhani kama vinaiona dunia maana vipo mbali sana
 
Kwa maana hiyo dhumuni la wanaanga kwa sasa ni nini ............. Ikiwa ndani ya solar system yetu hakuna sehemu nyingine kwenye uhai,na huko nje ya solar system yetu ndio haiwezekani kufika binadamu.......???
 
Kwa maana hiyo dhumuni la wanaanga kwa sasa ni nini ............. Ikiwa ndani ya solar system yetu hakuna sehemu nyingine kwenye uhai,na huko nje ya solar system yetu ndio haiwezekani kufika binadamu.......???
Kwa sasa wanaanga wana madhumuni mengi tu, ila kubwa moja wapo ambalo wanalipigania ni kuweka space base kwenye mwezi,na pia kuweka camp na kuanzisha makazi kwenye sayari ya mars,na wameanza na hilo kwa ku tengeneza kituo cha utafiti maarufu kama international space station ( ISS) huko wanaanga wanafanya majaribio mengi yakiwepo binadamu atawezaje kuishi kwenye zero gravity,mimea itawezaje kukua kwenye zero gravity

Huwezi jua huenda kukawa na uhai kwenye mifumo mingine ya nyota maana kuna nyota nyingi sana, na kila nyota ila planet zake huenda kukawa na uhai somewhere wanaanga bado wanaendelea kufanya utafiti,voyager 1 na 2 zilivyotumwa mwaka 1977 zilikuwa na details kuhusu sisi ikiwepo DNA structure yetu na location ya solar system yetu ili endapo kama kuna aliens huko wakikiona chombo hicho au kikienda kuangukia sehemu walipo wapate hizo details na watutafute

Kuna mwaka wanaanga waliiona sayari moja siikumbuki jina lake ila. walituma radio signals ziende kwenye sayari wanasema ina possibility yakua na uhai, ila hizo signal zitachukua takribani miaka 25,000 kufika kwa hiyo kama tutapata majibu basi ni miaka mingi ijayo
 
Duh haya mambo kazi kweli kweli kuna muda wanasayansi wenyewe huwa wanachunguza mpk wanachoka
 
mkuu hivi hizo Pete za Saturn zilisababishwa na nini? Na kwanini zipo vile?
Nini msaada wake kwa Saturn?
 
Tukiweza kuijaza Mars na hewa ya Oxygen maisha yanawezekana hata kama kuna baridi. Hapa Duniani Waeskimo wanaishi north pole ambako kumeganda karibuni mwaka mzima.
Mkuu kwanini north pole ndio tu kuwe na barafu sio na south pole na kwa dunia yetu south ipo wapi?
 
samahani kwa maswali mengi kwani binadamu alitokeaje yaani chanzo cha binadamu kuwa hapa sayansi inasemaje?
 
samahani kwa maswali mengi kwani binadamu alitokeaje yaani chanzo cha binadamu kuwa hapa sayansi inasemaje?
Nakumbuka hili swali lilijibiwa mwanzo kabisa wa mada kuwa chanzo cha uhai au kutokea kwa binadamu kulitokana na vumbi (dust) na vipande vipande vilivyobaki katika utengezwaji wa nyota na kupitia katika process mbalimbali za mabadiliko ndipo uhai ukatoa...if not mistaken
 
OK asante sana sikuwa nimeona kama lilijibiwa ndio maana nikauliza
 
Hivi wamatumia njia gani kupata mawasiliano na hizo voyages ambazo zipo mbali na dunia? Kuna mionzi inatumika hapo
 
Hakijazidi 30,000km/h...........speed ya mwanga hata 10% bado hutajaweza kufikia
Mkuu vipi kuhusu tachyonic particles zilizogunduliwa kwenye space inasemekana zinamove faster than light. hii imekaaje hapo
 
Kuhusu voyage mkuu kifyatu alilijibu vzr hapa!
jay john
 
mkuu hivi hizo Pete za Saturn zilisababishwa na nini? Na kwanini zipo vile?
Nini msaada wake kwa Saturn?
Pete za Saturn zinaweza kuwa zilitengenezwa na vimondo vikubwa au hata takataka ambazo hazikuweza kujitengeneza kuwa mwezi na zikabaki ndogondogo na zinaelea angani. Sehemu kubwa ya hizi takataka katika hizi pete ni maji (barafu)
 
South pole pia kuna barafu. Wakati North pole kuna barafu iliyoko juu ya ardhi, south pole ni barafu tupu hivyo ikiyeyuka yote kutakuwa na ardhi chache sana.
Una maana ardhi yote itamezwa na maji?
 
Mkuu vipi kuhusu tachyonic particles zilizogunduliwa kwenye space inasemekana zinamove faster than light. hii imekaaje hapo
Wanayasansi wanasema ni hypothetical tu, bado hawajazigundua, ina maana hazipo, na kama zikiwepo duuh inabidi rewrite baadhi ya laws za physics
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…