Mkuu
Kifyatu vipi kuhusu wanasayansi je huwa wanakwenda anga za mbali au hutumwa vyombo tu. Na nilisikia kujengwa kwa vituo vya utafiti wa anga huko kwenye sayari nyengine je ni kweli? Na vifaa na vyombo vinavyokuwa huko vinatumia power source ya aina gani?
Majibu ni kama yafuatayo:
Vipi kuhusu wanasayansi je huwa wanakwenda anga za mbali au hutumwa vyombo tu?
Kati ya hapa duniani na mwezi wetu binaadamu wamesafiri sana. Hata hivi sasa kuna wanasayansi kadhaa kwenye kituo cha utafiti angani
(International Space Station) wakiendelea na tafiti zao. Kituo hiki siku zote kina watu. Huwa wanabadilishana tu mara kwa mara.
Nilisikia kujengwa kwa vituo vya utafiti wa anga huko kwenye sayari nyengine je ni kweli?
Ni kweli lakini kwa sasa hakuna kituo chenye binaadam. Nitakupa mifano michache ya vyombo vya tafiti vilivyokwenda kwenye sayari.
Mars: Safari za kwenda Mars zilianza tangu 1960. Nyingi zilipeleka vyombo kupitia tu au kuizunguuka. Sasa hivi kuna magari 2 (Rovers zilizotua 2003 na 2011) yaliotua na kuendelea na utafiti. Lengo ni kuona kama baadae wanaweza kujenga kituo cha kudumu ili watu waende.
Saturn: Mwaka 2004 chombo kiitwacho
Cassini-Huygens kilifika Saturn.
Cassini kinaizunguuka hii sayari hata leo. Mdogo wake
Huygens kilitua kwenye mwezi mmoja wa Saturn uitwao
TITAN na kuona kuwa unafanana sana na dunia yetu na kuwa una mito, maziwa na mvua. Lakini mvua hii sio ya maji bali ya Methane (methane ni hewa hapa kwetu lakini ni kama maji kule kwa ajili ya baridi kali)
Kuna vyombo vingi sana vilivyopelekwa angani. Vingine vinazunguuka sayari, vingine vinatoswa ndani ya sayari kuona kuna nini, na vingine vinaendelea tu kusafiri na kuna vinavyotoka sasa kwenye solar system yetu lakini bado vinawasiliana nasi.
Vifaa na vyombo vinavyokuwa huko vinatumia power source ya aina gani?
Vyombo vyote viendavyo angani hasa kama vimepangiwa kwenda masafa marefu vinatumia vyanzo viwili vya nishati.
- Kwanza vinakuwa na solar panels kutengenezea umeme kutokana na mwanga wa jua.
- Lakini chanzo cha muhimu sana kwa vyombo hivi ni nguvu za nyuklia. Hivi vyombo vinakuwa na nuclear reactors zinazotengeneza umeme na kuutumia moja kwa moja au kuuhifadhi kwenye batteries. Chanzo hiki cha nishati ni muhimu sana hasa ikifikia kuwa chombo kiko mbali sana na jua mpaka jua kuonekana kama nyota tu.