Ufahamu kuhusu nyota za angani

Ufahamu kuhusu nyota za angani

Hah ha ha ha mimi nimeshangaa unavyosemaga yupo wakati hapa naona ukimpinga kwa sayansi [emoji12]
Wakina newton, releigh walikuwa wanasayansi wakubwa na waliamini mungu yupo nakushungaa ww unajipa upofu wa kudai mungu hayupo. Unajua Charles Darwin aliamini mungu pamoja na uwongo wake ambao nyinyi mmeujalili Kama chanzo cha maisha.
 
Wakina newton, releigh walikuwa wanasayansi wakubwa na waliamini mungu yupo nakushungaa ww unajipa upofu wa kudai mungu hayupo. Unajua Charles Darwin aliamini mungu pamoja na uwongo wake ambao nyinyi mmeujalili Kama chanzo cha maisha.
Kwani kuamini kwake kunanihusuje mimi?
Kuamini tu! Waweza kuamini hata kikombe ni mungu wako.
 
Kwani kuamini kwake kunanihusuje mimi?
Kuamini tu! Waweza kuamini hata kikombe ni mungu wako.
Mi nimekumpa mfano kukuonyesha tu kwamba huwezi kuja na conclusion ya kusema mungu hayupo kisa tu maswala ya sayansi. Usichanganye dini na sayansi. Kuna vitu vingi bado havifahamiki.
 
Suala la kusema kuwa mungu hayupo,sikweli,kwa mtizamo tuu ,haya magalaxy yoote yalitokeaje,hakuna mashaka juu ya uwepo wa mungu,ila tu kusema,sisi katika ulimwengu hizi ni viumbe wachache sana,kama inavyoandikwa kuwa tunaangamia kwa kukosa maarifa,huenda bado wanadamu wanaweza kutumia maarifa zaidi kujua mengi zaidi,mfano kusafiri kutoka sayari hadi sayari,mfumo hadi mfumo,na galaxy hadi galaxy,
 
duuu?... haya mambo mazito, mwenzenu shule niliyosoma haikuwa na kifaa chochote cha kupima umbali wa jua,nyota wala kasi ya mwanga kusafiri, zaidizaidi niliyasoma tu kwenye abort na lumbert, na hata mwalimu wangu alisema yeye mwenyewe hajawahi kujihakikishia kuhusu hizi takwimu kama ni za kweli ila nae aliambiwa vivyohivyo na mwalimu wake... hata mimi sasa ni mwalimu na ninafundisha hivohivo nilivyoambiwa
 
UY_Scuti_size_comparison_to_the_sun.png
 
duuu?... haya mambo mazito, mwenzenu shule niliyosoma haikuwa na kifaa chochote cha kupima umbali wa jua,nyota wala kasi ya mwanga kusafiri, zaidizaidi niliyasoma tu kwenye abort na lumbert, na hata mwalimu wangu alisema yeye mwenyewe hajawahi kujihakikishia kuhusu hizi takwimu kama ni za kweli ila nae aliambiwa vivyohivyo na mwalimu wake... hata mimi sasa ni mwalimu na ninafundisha hivohivo nilivyoambiwa
sasa si ufanye utafiti na kutafuta hivo vitu vinavyotumika kupima mwendokasi wa mwanga ili usiendelee na wewe kuwalilisha wanafunzi wako mwalimu vp?
 
Baadhi ya nyota unazoziona si zote ni nyota zingine ni sayari,ukiamka alfajiri sana kuanzia saa 10 hadi saa 12,kuna nyota huwa zinang'aa sana na kubwa mno kuliko zingine zote,huwa hazizidi mbili,zile ni sayari,hata dunia tuliyomo nayo ni sayari,maajabu ni kwamba ukienda kwenye
sayari na nyota kipi kikubwa??
 
hii elimu yetu ya bongo bure kabisa,...kumeza history,...
na haya mambo tofauti,...
physics nlisoma o level,..ila nmejiona mtupu kwa hili somo,..khaa
elimu ya kumeza,..elimu cheti,unavyovisoma olevel science serikali
inakuchagua hkl advance,..science ya olevel ya kumeza huapply sehemu,..shida tupu
 
kasi yav kwenda wapi????
kwani sattellite zinamove sio kwamba zimestick sehem1????
eb ndadavulie apa,..
KLF

Mkuu asante kwa swali - ni zuri sana.

Kuna satelite nyingi sana na ziko umbali tofauti kutoka ardhini kutegemea matumizi yake.

Baadhi ya matumizi ya satelite ni:
  1. Ku-spy
  2. Kupima hali ya hewa
  3. Kutafuta rasilmali (kama mafuta na madini)
  4. Kutoa huduma ya Global Positioning System (GPS) kwa kuongoza vyombo vya usafiri baharini na nchi kavu
  5. Kurusha matangazo ya TV na Redio
  6. Kituo cha utafiti kiitwacho International Space Station (ISS)
  7. nk.
Cha kwanza kujua ni kwamba satelite zote zinatembea kwa kasi kubwa sana. Zikisimama zitadondoka ardhini.

Kama kasi ya satelite ni sawa na kasi ya dunia inavyojizunguusha kwenye mhimili wake (mara moja kila baada ya masaa 24) basi sisi hapa ardhini tutaiona kama imesimama. Satelite za aina hii mara nyingi hutumiwa kurushia matangazo ya TV na Radio. Hii ndio maana madishi ya TV yanaelekezwa sehemu moja tu kwa sababu hiyo satelite itakuwepo hapo siku zote. Satelite hizi zinajulikana kama GEO-SYNCHRONOUS satelites (satelites zinazoonekana kama zimesimama.) Satelite hizi zinawekwa umbali wa 36,000 km (22,300 miles) kutoka ardhini na zinatembea kwa kasi ya 11,000 km/saa (6876 maili/saa)

Mfano mwengine wa satelite ni ISS (namba 6 hapo juu). Hii station iko karibu zaidi nasi ikiwa umbali wa km 400 (au maili 250) hivi kutoka ardhini - fananisha na umbali wa geosynchronous satelites. Station hii inaizunguuka dunia kwa kasi ya 27,400 km/saa (au 17,150 ml/saa) - fananisha na kasi ya geosynchronous satelites.

Ukiachana na hizi geosynchronous satelites, satelites nyingine zote nilizozitaja hapo juu na zaidi utaziona zinatembea angani kama utajua pa kuangalia.

Nenda hapa na utaweza kuona satelite zote zilizopo angani na zinavyotembea in real-time. Bonyeza kitufe cha J-Track 3D Satellite Tracking ili kuona zinavyotembea.

J-Track 3D Satellite Tracking - NASA Science
 
Darasa zuri sana,napenda kujua kuwa kuna uwezekano wa dunia siku moja ikavamiwa na jua na kuangamia?

Hii itatokea for sure, labda dunia yetu iangamizwe na kitu kingine kabla ya siku hiyo ya mwisho.

Jua letu kwa sasa linachoma hewa ya Hydrogen kutengeneza Helium. Itachukua mabilioni ya miaka kuimaliza hii Hydrogen. Hydrogen ikimalizika itaanza kuchoma helium kutengeneza element nyingine nzito.

Jua litakapoanza tu kutengeza chuma (Iron) basi hilo jiko la nuklia linakufa mara moja na kishindo kikubwa kitatokea (soma maelezo yangu ya awali kuhusu Super-Nova katika uzi huu huu). Jua letu halitakufa kwa kishindo kikubwa kama cha supernova bali kitatosha kutimua vumbi lenye joko kali litakaloimeza Mecury, Venus, sisi (Earth) na hata kuikaribia Mars.

Jibu rahisi la swali lako ni "NDIO", dunia yetu itakujamezwa na jua siku moja (hakuna utata hapa). Lakini itachukua mabilioni ya miaka kufikia huko.

Kwa sasa, wewe jivinjari tu na moja moto moja baridi ukijua wazi kuwa wewe, watoto wako, wajukuu, vilembwe, nk. wataamka kila asubuhi yao na kiliona jua kama lilivyo leo.
 
Back
Top Bottom