kasi yav kwenda wapi????
kwani sattellite zinamove sio kwamba zimestick sehem1????
eb ndadavulie apa,..
KLF
Mkuu asante kwa swali - ni zuri sana.
Kuna satelite nyingi sana na ziko umbali tofauti kutoka ardhini kutegemea matumizi yake.
Baadhi ya matumizi ya satelite ni:
- Ku-spy
- Kupima hali ya hewa
- Kutafuta rasilmali (kama mafuta na madini)
- Kutoa huduma ya Global Positioning System (GPS) kwa kuongoza vyombo vya usafiri baharini na nchi kavu
- Kurusha matangazo ya TV na Redio
- Kituo cha utafiti kiitwacho International Space Station (ISS)
- nk.
Cha kwanza kujua ni kwamba satelite zote zinatembea kwa kasi kubwa sana. Zikisimama zitadondoka ardhini.
Kama kasi ya satelite ni sawa na kasi ya dunia inavyojizunguusha kwenye mhimili wake (mara moja kila baada ya masaa 24) basi sisi hapa ardhini tutaiona kama imesimama. Satelite za aina hii mara nyingi hutumiwa kurushia matangazo ya
TV na
Radio. Hii ndio maana madishi ya TV yanaelekezwa sehemu moja tu kwa sababu hiyo satelite itakuwepo hapo siku zote. Satelite hizi zinajulikana kama
GEO-SYNCHRONOUS satelites (satelites zinazoonekana kama zimesimama.) Satelite hizi zinawekwa umbali wa
36,000 km (22,300 miles) kutoka ardhini na zinatembea kwa kasi ya
11,000 km/saa (6876 maili/saa)
Mfano mwengine wa satelite ni ISS (namba 6 hapo juu). Hii station iko karibu zaidi nasi ikiwa umbali wa
km 400 (au
maili 250) hivi kutoka ardhini - fananisha na umbali wa
geosynchronous satelites. Station hii inaizunguuka dunia kwa kasi ya
27,400 km/saa (au
17,150 ml/saa) - fananisha na kasi ya
geosynchronous satelites.
Ukiachana na hizi
geosynchronous satelites, satelites nyingine zote nilizozitaja hapo juu na zaidi utaziona zinatembea angani kama utajua pa kuangalia.
Nenda hapa na utaweza kuona satelite zote zilizopo angani na zinavyotembea in real-time. Bonyeza kitufe cha
J-Track 3D Satellite Tracking ili kuona zinavyotembea.
J-Track 3D Satellite Tracking - NASA Science