Ufahamu kuhusu nyota za angani

Eti muheshimiwa hii umbali kutoka galaxy,spidi ya mwanga ndani ya sekunde moja vinapimwaje?

Kasi (speed) ya Mwanga:
Hii ni rahisi kupima siku hizi tulivyokuwa na hii teknolojia ya LASERs (Light Amplification by Stimulated Emission of Radiation), au hata RADAR (Radio Detection and Ranging). Mionzi ya LASER au RADAR inatembea kwa kasi ya mwanga. Sasa ukielekeza hii mionzi kwenye kitu unachokijua umbali wake (kama mwezi, minara kati ya mlima na mlima) na kupima muda unaotumika kwa hiyo mionzi kwenda na kurudi (mwangi au reflection) basi unaweza kukokotoa kasi ya mwanga.

Umbali wa Nyota au Galaxy:
Kuna njia nyingi ya kupima umbali wa nyota au galaxies. Mojawapo ni kutumia Parallax. Ngoja nikupeleke kwenye ukurasa huu hapa chini utaokupa vielelezo vizuri zaidi kuliko kama mimi nikikuelezea hapa.

Parallax and Distance Measurement
 

Kifyaru; tafadhali naomba unieleweshe khs hizi satellite zetu zinazorushwa angani je zipo umbali gani? Zinavuka hili tabaka la ozon layer? Pia kuna ile dhana inayosemwa sana ktk hiyo ozon layer pindi unapokuwa unatoboa anga za mbali ni sehemu ambayo chombo huwa kinatumia nguvu kubwa na kasi ya ajabu kupita ukanda huo mana kunasemekana kuna mvutano wa ajabu na ukipita tu hapo nimeskia kuwa ndiyo unaangukia upande mwingine yaani chombo kinakuwa kama kinaserereka kipo free mpk kwenye destination.

Na ndivyo hivyo hivyo wkt wa kurudi duniani ukivuka tu hapo upo free.
 
sasa si ufanye utafiti na kutafuta hivo vitu vinavyotumika kupima mwendokasi wa mwanga ili usiendelee na wewe kuwalilisha wanafunzi wako mwalimu vp?
Mkuu shule niliyopo hata library tu haina, sasa itakuwa kuhusu hivo vifaa.
kwa kifupi humu ndani sina uhakika kama hizi data wanazotoa wanauhakika nazo au wamethibitisha... .. .zaid ni kuwa mimi na wewe tunasema tulichoambiwa
 

Kifyatu; tafadhali naomba unieleweshe khs hizi satellite zetu zinazorushwa angani je zipo umbali gani?

Kuna zilizoko umbali wa 36,000 km (geosynchronous satellite za TV, Radio, na huduma za simu) na,
kuna zilizoko karibu sana kama 400 km (International Space Station) au chini ya hapo (spy satelites).

Zinavuka hili tabaka la ozon layer?
Ozone layer yetu iko umbali wa kati ya 10km mpaka 17km (asilimia 90) na inaendelea mpaka 50km. Satelite zote ziko juu ya hii layer. Orbit ya chini kabisa ya satellites ni kama 160 km hivi.

Swali lako la mwisho:
Ili satelite ikae kwenye orbit (umbali) fulani lazima itembee katika kasi itakayoipa uwiano kati ya gravity (uzito wake) na centripetal force. Orbit za chini zinahitaji spidi kubwa na zile zilizo mbali zinatembea kwa kasi ndogo. Ili kuirudisha satelite duniani cha kufanya ni kupunguza tu spidi yake na itadondoka tu.
 
Shuklani kwa majibu. Sasa satellite inaangukaje wakati gravitation force inapungua kutokana na height kwa nini zisielee tu angani kwa sababu hakuna gravity.
 
Shuklani kwa majibu. Sasa satellite inaangukaje wakati gravitation force inapungua kutokana na height kwa nini zisielee tu angani kwa sababu hakuna gravity.

Angani pia kuna gravity. Ni gravity hiyo ya dunia ndio inayoufanya mwezi wetu uizunguuke dunia.

Satellite zinaonekana kama zinaelea angani kwa sababu tu zinatembea kwa kasi kubwa. Hii kasi ikipungua basi nayo inaanza kuanguka taratibu kuja ardhini. Mara nyingi hizi satellite zinapoanguka zikifika kwenye hewa ya Oxygen (kama km 50 au chini yake) basi zinaungua kabisa, kama vimondo, na hazitui ardhini.
 
Kifyatu; bado kuna maswali mengi sana kwenye thread, swali hivi ikitokea mtu ameanguka au amechomoka ndani ya hiko chombo kwa bahati mbaya je anapotelea wapi?

Dunia duara ndiyo ila ukitazama vzr Picha iliyopigwa kwa satellite na jinsi sisi binadam tunavyoishi juu ya dunia hii yenye umbo kama la mpira najiuliza haya maji ya bahari kwanini yasimwagike na kupotelea huko angani mana picha inaonesha tunaishi nje ya dunia mithili ya mjusi anayekatiza katikati ya Dari lkn haanguki sababu tafadhali.
 

swali hivi ikitokea mtu ameanguka au amechomoka ndani ya hiko chombo kwa bahati mbaya je anapotelea wapi?
Ikitokea hivyo basi anaweza kubaki kwenye hiyo orbit milele kama ilivyo mwezi wetu. Mara nyingi atagongana na takataka nyingine angani na kupunguza kasi yake na kuanguka halafu kuungua anapoingia kwenye anga lenye hewa.

Swali la pili:
Sijui kama nimelielewa vizuri swali lako la pili. Sisi sote (pamoja na maji ya bahari) tunavutwa kuelekea katikati (center) ya dunia. Maji au kitu chochote kile hakiwezi kutoka na kuachana na huu mvuto wa dunia isipokuwa kama kitaruka kwenda juu katika kasi kubwa (escape velocity) ya 40,270 km/saa au zaidi.
 
Kifyatu; nimeibuka na swali jingine, kama vyombo hivyo wakati wa kurudi kama hizo satellites na mavimondo sasa inakuaje kwa mwana anga kurudi kwake duniani ikiwa kama hicho chombo kikiingia kwenye hewa kinalipuka?? Hebu fafanua vizuri hapo uzima wa huyu mtu toka anga za mbali mpk anapotua anavyoeuepuka huo moto.
 
Kifyatu; nimeibuka na swali jingine, kama vyombo hivyo wakati wa kurudi kama hizo satellites na mavimondo vinàlipukia angani kwenye hewa, sasa inakuaje kwa mwana anga kurudi kwake duniani ikiwa kama hicho chombo kikiingia kwenye hewa kinalipuka?? Hebu fafanua vizuri hapo uzima wa huyu mtu toka anga za mbali mpk anapotua anavyoeuepuka huo moto.
 
Huku ukimsubiri labda nieleze Chombo kikaribia kwenye anga za chini kwa vile kinakutana gravity na air resistance basi kinachemka sana kuna mawe special wanayaweka ndani ya hicho chombo ambapo yana heat na kuwa kama mekundu but apo apo unaweza kulishika na lisikuunguze
 
Ahsante sana kifyatu kwa jibu jemaa
 
nakumbumbuka nlisomaga haya mambo olevel,..
majibu ya swali lako la2,..sijaelewa
hivi tunavutwa na hiyo kani sijui kuelekea centre ya dunia minaona kama fix/kamba,.
mbona ndege zinaruka angani lakini haziendi moja kwa moja kwenye space inayoonekana pembeni ya dunia
alaf huwa kama bonde/shimo kubwaaaa sana mbna ndege huwa hazipotei,...
 
dahhh aya mkuu,..
haya yanawenyewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…