Ufahamu na kujiepusha na Jicho baya kwa watoto wadogo!!

Ufahamu na kujiepusha na Jicho baya kwa watoto wadogo!!

Hakuna cha jicho baya wala jicho jema!

Ujinga wenu tu na kukosa elimu ndio vinawatesa ndio maana mnakanyaga mafuta hovyo mpaka roho zinawatoka!

Hata mavi mtalishwa ninyi kwa kuamini yasiyokuwepo!

Hilo jicho baya linakuwa na rangi gani? hudhurungi?
 
Duniani mnayo dhiki, naji jipeni moyo kwa maana mimi nimeushinda ulimwengu.. alisema Jamaa mmoja.

Mkuu, ukiona jambo linazungumziwa public kama hivi shukuru, maana ni moja ya bahati ya kuepukika hayo macho ya husuda au macho mabaya kwa kutumia msaada wa imani yako kwa ajili afya, upendo na furaha ya kizazi chako.

Maana siku mtoto wako anapopgwa jicho baya hata shughuli za kiuchumi na Muda wa kuchangia hoja jamii forum huwezi pata.

Hakuna cha jicho baya wala jicho jema!

Ujinga wenu tu na kukosa elimu ndio vinawatesa ndio maana mnakanyaga mafuta hovyo mpaka roho zinawatoka!

Hata mavi mtalishwa ninyi kwa kuamini yasiyokuwepo!

Hilo jicho baya linakuwa na rangi gani? hudhurungi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duniani mnayo dhiki, naji jipeni moyo kwa maana mimi nimeushinda ulimwengu.. alisema Jamaa mmoja.

Mkuu, ukiona jambo linazungumziwa public kama hivi shukuru, maana ni moja ya bahati ya kuepukika hayo macho ya husuda au macho mabaya kwa kutumia msaada wa imani yako kwa ajili afya, upendo na furaha ya kizazi chako.
Maana siku mtoto wako anapopgwa jicho baya hata shughuli za kiuchumi na Muda wa kuchangia hoja jamii forum huwezi pata.



Sent using Jamii Forums mobile app
Hakuna lolote!
 
usomi na usasa unatuponza sana, mambo mengi ya zamani wazee wetu walifanya ya kiutamaduni yalitulinda sana, sasa km mtu haupo karibu sana na Mungu inabidi tu ufundishwe jinsi ya kujikinga na macho mabaya, kwenye elimu yako kazi afya n.k. macho mabaya yapo hata biblia inasema kwenye Timotheo nimesahau mstari na sura inasema Bwana ataniepusha na kila neno baya lilikusudiwa kwangu.

So mtu mwingine anakupiga jicho la kutofurahishwa na wewe na kukunenea mabaya moyoni. kuomba ulinzi wa Mungu ni muhimu sana. km wewe sio muumini wa dini na sio mtu wa kusali sana basi itabidi tu ufate njia za zamani za kupaka watoto mikaa na kufunga vitambaa, kuogeshea maji ya chumvi n.k.

by the way wkt nakua nyumbani tulikuwa tukisaga unga tunauanika halafu ktktk tunaweka mkaa, sikuwa naelewa ndo naelewa sasa kwa nini.
 
Karibuni nyote katika mada hii inayokusudia kupata ufafanuzi na ufahamu juu ya JICHO BAYA katika maada hii najaribu tu kuchokoza wajuzi wa mambo kama akina Mshana Jr waje kutufahamisha na wengine;

Hoja ni JICHO ila ntaita jicho baya
kwa ufupi tu ni jicho ambalo mtu humtazama hasa mtoto kwa kumtamani au kumshitukia au kumshangaa aidha kwa uzuri wake, unene na sifa zake nyingie alizojaliwa na Muumba.

Tamaduni zetu zina mambo sana;

TANGA
Muku

Nilikuwa Tanga miaka fulani nikasikia habari ya "Muku" na kupigwa "zongo" hiyo muku ni watu huchanjia ili wawe na nguvu. Kwa jinsi nilivyosikia mtu aliyechanjiwa hiyo muku hapasi kukasirika hovyo ila ukimkasirisha na akikasirika na kuchuka hatua ya kukupiga hata kofi tu basi kuamka kwako kwa hitaji kudra za Muumba. (kwa wanaojua hili mtafafanua zaidi).

Zongo
Kwa mara ya kwanza nasikia neno zongo mkoani Tanga, utasikia wanasema amepigwa zongo hii ni kama uchawi fulani hivi ambao wanyekujua waje kutuelimisha kuufahamu na kujiepuisha nao. Hii inadalili zake pia mara kuuvimba tumbo nk. (Wenyekujua zaidi mtujuze).


ARUSHA
Jicho

Na sasa nimepata habari ya JICHO au macho, hii hali imeshamiri sana mkoani Arusha, kwa ndugu zetu wale wafugaji. Utasikia mtoto huyu anajicho kali sana inabidi akatengenezwe. Katika udadisi wangu mdogo, nimejifunza kwamba jicho au macho huwapata watoto weupe ikiwa ni watu aidha kwakujua au kutokujua wakimtazama mtoto kwa kumtamani, wivu au wakashtuka labda "dah mtoto mzuri huyu".
Hivyo mtoto hupatwa na hilo jicho na kuanza msumbua homa za mara kwa mara, kulia lia bila sababu na kadha wa kadha. Wanasema mtu akimshtukia mtoto basi ni sharti awahi kumshika sikio au kutema mate chini ili ule ubaya wa jicho lake la mshtuko limwepuke mtoto au mtu.

JICHO BAYA LIMPATAVYO MTOTO
Mtu aakimwona mtoto na kumshangaa aidha kwa uzuri wake au weupe wake basi au kwa kumtamani au wivu tu basi ubaya wa hayo macho humpata mtoto na kuanza mkusumbua.

DALILI ZA JICHO KWA MTOTO
Kwa na joto kali na katika vipimo hakuna ugonjwa, kushindwa kula, kukosa furaha, kulia na kuhangaika hasa nyakati za usiku, kutapika nk.

TIBA YA JICHO
Zipo njia kadhaa nimebaini ambazo hutumika kuwatibu au kupoza jicho kwa watoto, njia moja wapi ni maji, chumvi na magadi hapo kama umetoka tembea kwa mkusanyiko wa watu wengi na mtoto basi unapaswa kumwogesha mtoto na maji yenye chumvi na magadi. Husaidia kutoa jicho au kutuliza kama jicho kali.

Ila, kwa namna ya kutengeneza jicho hapo sasa wanasema ukisha mtengeneza mtoto wako wa kwanza basi sharti uwatengenezo wote hadi utakao wazaa hapo baadae (sijajua mahusiani yako hapo).'

Maombi, hii pia ukimwomba Mungu uponyaji wapatikana wa watoto au mtoto mwenye jicho baya.

KINGA YA JICHO
Hapa namna ya kumkinga na jicho huwa wanatumia mkaa au kumpaka mtoto usoni kama kwenye nyusi kama wanja vili hii wakiamini kwamba jicho baya humezwa na weusi kwa maana ya mkaa au kitu chochote cheusi (ndio maana pana baadhi ya wazazi huwafunga watoto hirizi wengine vitambaa vyeusi shingoni, kiunoni au mkononi ili machao ya watu wabaya badala ya kumshangaa mtoto yaishie kushangaa hirizi au kitambaa kwa mtoto).

Hii ndio maana utakuwa watoto wadogo huwa wanapakwa wanjaa au mkaa usoni ili wata wakimtazama wabakia kushaa ule wanja au mkaa nakuacha kumshanga mtoto hapo unakuwa umemlinda mtoto na hatari ya hayo macho ya watu.

Njia nyingi ni kukwepesha mtoto na macho ya watu, kwa mkufungia ndani tu au ikibidi kutembea nae nje basi utakuta mtu anamfunika mtoto gubigubi ili tu asionekane.
Kumwekea mtoto mkaa atembee nao.

Maji ya baraka na Maombi.

Kisa cha kujifunza
kuna mtu mmoja kila alipokuwa akija nyumbani kwangu na kuwaona mtoto wangu basi siku hiyo hakuna kulala mtoto analia tu, ila baada ya kugundua hivyo nikawa namwepusha mtoto na huyu mtu. Japo nilikuja kumwambia, ila wanasema pana watu wengine wanafahamu kuwa wana hayo macho mabaya na wengine hawafahamu.

MADHARA YA JICHO BAYA
Kuumwa, kukosa afya na husababisha kifo,

MJADAWA UPO WAZI KUJADILIWA
Binafsi na hitaji kujua zaidi haya mambo, je jicho ni uchawi? na mambo mengine kuhusu macho au jicho hasa kwa watoto nk.
Karibuni..
masai dada Mshana Jr Masai Kaskazini Masai Ladislaus Masai Msukuma Original na wengine wote wenyekujua haya mambo!!!

Marejeo
https://descubrir.online/sw/aprende-la-poderosa-oracion-contra-el-mal-de-ojo/
Tamaa kutoka jicho baya
Jinsi ya kujiondoa jicho baya?
Nitarejea hapa ngoja nitulie

Jr[emoji769]
 
Nitarejea hapa ngoja nitulie

Jr[emoji769]
Mshana jicho katika mazao linazuiwa vipi? Mazao yangu yamekuwa yakiharibika kimaajabu wakati nimefuata principle zote za kilimo.Wakati mwingine huwa nawaza niende kutafuta kinga kwa masangoma lakini nashindwa kwa sababu ya vitisho kuwa unaweza pewa nasharti ya kudhuru.Ujweli upoje mkuu.
 
Mshana jicho katika mazao linazuiwa vipi? Mazao yangu yamekuwa yakiharibika kimaajabu wakati nimefuata principle zote za kilimo.Wakati mwingine huwa nawaza niende kutafuta kinga kwa masangoma lakini nashindwa kwa sababu ya vitisho kuwa unaweza pewa nasharti ya kudhuru.Ujweli upoje mkuu.

kumbe hadi kwenye mazai linahusika!
nakumbuka zamani kiasi mwanzoni mwa miaka 2000s nilipanda bus la hood kuelrkea Mbeya kutokea Msamvi, so nilipoingia ktk bus hakikuwa na abiria wengi nikajichagulia kukaa seat moja na mdada fulani hivi siwajua tena safari kama huna kitabu cha kusoma basi kaa na mti kupiga stori za hapa na pale ili kufupisha safari.
nilipofika nikamsabahi kama desturi yetu wa afria yule dada aliitikia kwa shari sana siku hofu nikamwmbia naweza kaa hapa! Akanijibu dry saana; kwakweli sikutegemea alivyojibi na nilijikuta nimekereka saana. Nikamtazama na kujisemea moyoni "hii safari kama utafika Mbeya au uendako sijui". nikatafita seat nyingine nikakaa,safari ikaanza tumefika maeno ya ngerengeri mkaguzi wa tiketi huyu anakagua mara paaaah akamfikia bidada kumdai tiketi mdada hana tiketi akaambiwa atoe nailu akasema yeye ni staff kapandiswa gari jamaa fulani hapo msavu akamtaja! Mkagua tiketi akamkazia toa nauli kama hauni utashuka hapo mbele Mzumbr urudi mjini.
Kweli bwana tumefika njia panda ya Mzumbe bus likapati jamaa akaja kampatia mdada elfu moja na akamshusha akamwambia hii nauli urudi mjini!

Nikajikuta natabasamu nikajisemea laiti kama angekubali kuniruhusu kukaa hapo huenda ningemlipia nauli.

baada ya miaka kadhaa ndio najitathmini ile ilikuwa ni nguvu ya namna gani ilitokea hata yule binti kusushwa njiani sawa sawa na nolivyonema moyoni mwangu wakati namtazama baada ya kunzuia kukaa nae!!

Au ndio nguvu hasi ya jicho!?!
 
ngoja niweke kambi hapa.kwa sie wenye watoto wadogo.
Tupate mawili matatu ya kujifunza
 
Sio Watoto tu kunajamii ukiingia MTU mzima pia ukila adharani lazima upate zongo.Utasikia kama tumbo limejaa gesi na kucheua harufu ya mayai.Mwa maasai IPO sana
 
Mkuu ulichokisema ni kweli tupu ntapata ku share story moja ilitokea maeneo ya uchagani huko miaka ya 80's

Aliishi bwana mmoja naye alikua na hicho unachoita macho basi huyo bwana akija kuangalia mtoto mchanga lazma huyo mtoto atafariki au akiangalia ndizi changa kabisa lazima itanyauka au kuvunjika

Mtoto wake wa kwanza na wapili walifariki mda mchache tu baada ya yeye kuja kuwaangalia na hapo ndio wazee wa mila wakagundua kua huyu jamaa ana hicho kitu ulichoita macho

Bas bhana mtoto wake wa tatu alipozaliwa kabla hawajamwonyesha mtoto halisi walichukua lile uwa la mgomba (lile linaning'inia kwenye ndizi) na kulifunga na baby show ikawa mithili ya katoto ka changa kamefunikwa bas wakamkabidhi jamaa kua huyu ndio mtoto wako jamaa kweli akampokea kumfunua ndio akakutana na lile uwa la mgomba kisha baada ya hapo ndipo wakamleta mtoto halisi na hiyo ndio ikawa pona ya kile kichanga ikafanyika hivyo kwa mtoto wa nne na wa tano pia.

Watu wenye macho ya aina hiyo hua wana uwezo wa kuathiri hata vyakula na vinywaji mfano pombe za kienyeji ndio maana kwa kule uchagani mtu akiwa ameanika chakula mfano ulezi,unga,nk kuna jani la mti fulani unaitwa mfifina hua wanaliweka juu yake inaaminika kua hilo jani lina uwezo wa ku deal na nguvu hasi kutoka kwenye macho ya watu

Pia wanapobeba vyakula mfano ndizi ,mihogo nk huliweka hilo jani kwa juu yake ili ku absolve negative energies kutoka kwenye macho ya watu na pia hata kutoka kwa washirikina hii pia kwa case ya pombe za kienyeji hasa mbege na dadii hilo jani linawekwa kwa mantiki hiyohiyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kweli.Zongo iyo ni kwamba anavyoshangaa moyo wa mtoto unachanika kama wembe ndio maana wanachukua lile uwa LA mkungu lenye umbo kama moyo.
 
Ni kweli.Zongo iyo ni kwamba anavyoshangaa moyo wa mtoto unachanika kama wembe ndio maana wanachukua lile uwa LA mkungu lenye umbo kama moyo.
Kwa hiyo nikichukua lile ua la mgomba nikawa natembea nalo kwenye nguo za mtoto.linaweza kumwepusha???
 
Kwa hiyo nikichukua lile ua la mgomba nikawa natembea nalo kwenye nguo za mtoto.linaweza kumwepusha???
Hapana iyo ni another case.Kuzuia zongo.Kuna matatu
1.MTU mwenye zongo kama anajijua akimuona mtoto anamtemea mate kichwani kama Maasai au anakuita kabla ajamuona mtoto ili asishtuke.Alafu anamshika kichwani.sababu zongo ni laana na kushika kichwani ni baraka so inanutralise laana
2.Mtoto akitoka apakwe wanja hata kama ni wakiume
3Usile hovyo kwenye jaamii ya asili au barabarani
 
Hapa kupitia uzi huu naona wachaga wa migombani ndio wanaongoza kwa kuwa na watu wenye macho ya hatanri na nguvu hatarishi, Kuna mangi mwingine alikuwa anaitwa MAKO huyu alikuwa anaweza kuangusha mti kwa kusukuma kwa mikono ama kuungoa kabisa alikuwa anabaka kila mtu amtakaye na polisi walikuwa wanampiga risasi haziingii alikuja kuuliwa na ndugu yake
 
Hakuna cha jicho baya wala jicho jema!

Ujinga wenu tu na kukosa elimu ndio vinawatesa ndio maana mnakanyaga mafuta hovyo mpaka roho zinawatoka!

Hata mavi mtalishwa ninyi kwa kuamini yasiyokuwepo!

Hilo jicho baya linakuwa na rangi gani? hudhurungi?


hahaha habari ya gereza huadithiwa vizuri na mfungwa na si askari magereza!!!
 
Back
Top Bottom