Ufahamu na kujiepusha na Jicho baya kwa watoto wadogo!!

Ufahamu na kujiepusha na Jicho baya kwa watoto wadogo!!

Nilivyosoma unazungumzia JICHO nikaja nduki huku mguu wangu wa tatu ukiwa umekaza. Laahaula kumbe ni jicho hilo?!
 
Katika nyakati tofauti nimesikia watu wakizungumzia Zongo na nilikuwa nachukulia kama jambo la kawaidia kabisa kwani sina ufahamu nalo kabisa.

Juzi nilikuwa nakula sehemu public na ndugu yangu mmoja, akaniambia kunja miguu ukiwa unakula sehemu za watu wengi kwani naweza nikapigwa zongo. Nikamuhoji kidogo kwan zongo ni nini, hakunipa majibu ya kuridhisha. Nilipuuza kwa mara nyingine.

Kuna wakata nilisikia pia mtu anapigwa hicho kinachoitwa zongo kwamba akiwa anakula nyama haishuki tumboni na inaweza leta madhara makubwa hadi kifo.

Kilichonifanya niulize leo humu ni baada ya kukuta na ndugu mwengine wa kike ambaye awali alikua na ngozi softi tu ya Uso ila ghafla ikabadilika na kupata vipele vilivyomsumbua kwa muda, hospital walimwambia hana allergy yeyote kwani katika kipindi hicho hakuwakubadili mazingira, mafuta ya kula wa wala kujipaka.

Wadau tupeni Elimu kidogo, Hii Zongo ni nn haswa,Uchawi ama?

Kwako Mwalimu @@Mshana
 
Kijicho.kweli kipo...Ila tunaomba Dua na kuwakabidhi mwenyezi Mungu watoto na vingine vya thamani tulivyonavyo.

ILA HALIMKUTI MTU BAYA AU UCHAWI AU KIJICHO ILA KWA IDHINI YAKE MWENYEZI MUNGU
 
ni kweli usemacho

mimi sikua najua hayo mambo ya macho ya husda nilipojifungua mtoto wangu mama alinambia nichukue mvuje niufunge kwenye kitambaa cheusi nimfunge nao mkononi

nilikua napingana naye sana tu nikimwambia mama tumuamini Mungu tu anatosha mama akanijibu ye kashatangulia kuliona jua kabla yangu nisiwe mbishi

honestly, nilikua namfunga ili mama asione nampuuza siku ambayo narudi kwangu ile kamba niliifungua nikaiweka kabatini katika kutembelea ndugu na majirani ile narudi kwangu jioni mtoto kila anyonya anatapika na kilio kama chote hatukulala ile siku ilibidi nimwamshe mama mtu mzima nimweleze akanijibu kama hivo nimpake wanja na kidoti juu ya paji la uso halaf niyaoshe maziwa yangu kwa jivu na magadi na nimfunge mvuje mkononi la mwisho nichane kitambaa ambacho nilikua natumia nikiwa kwenye ada yangu nimfunge nacho nikaona hi mizigo mwanangu yote ya nn akanambia nimfunge kiunoni ili isionekane nikafanya hivo na alinambia inasaidia husda au jicho baya au ile kumakiwa haimpat mtoto

kumakiwa n kule mtu humshangaa mtoto like khaaa kadogoo, au mtoto mweusi huyoo au mtoto mweupe kama mzunguu
Bado mnatumia vitambaa kwenye ada zenu?
 
hii ktu ipo sana kaskazin uko Imagine mzee mmoja algoma kuuza ng'ombe wake kwa bei ya chin ikapta siku tatu yule ngombe hata kusimama hawez tukamchinja uez amn tumbon alkua na lile tofal wanalo wawekeaga ngombe il alambe sasa jiulze liliendaje
 
hii ktu ipo sana kaskazin uko Imagine mzee mmoja algoma kuuza ng'ombe wake kwa bei ya chin ikapta siku tatu yule ngombe hata kusimama hawez tukamchinja uez amn tumbon alkua na lile tofal wanalo wawekeaga ngombe il alambe sasa jiulze liliendaje
Du vijicho
 
usomi na usasa unatuponza sana, mambo mengi ya zamani wazee wetu walifanya ya kiutamaduni yalitulinda sana, sasa km mtu haupo karibu sana na Mungu inabidi tu ufundishwe jinsi ya kujikinga na macho mabaya, kwenye elimu yako kazi afya n.k. macho mabaya yapo hata biblia inasema kwenye Timotheo nimesahau mstari na sura inasema Bwana ataniepusha na kila neno baya lilikusudiwa kwangu.

So mtu mwingine anakupiga jicho la kutofurahishwa na wewe na kukunenea mabaya moyoni. kuomba ulinzi wa Mungu ni muhimu sana. km wewe sio muumini wa dini na sio mtu wa kusali sana basi itabidi tu ufate njia za zamani za kupaka watoto mikaa na kufunga vitambaa, kuogeshea maji ya chumvi n.k.

by the way wkt nakua nyumbani tulikuwa tukisaga unga tunauanika halafu ktktk tunaweka mkaa, sikuwa naelewa ndo naelewa sasa kwa nini.
Kweli mmuu
 
Hii kweli kabisa mwanangu nusura afeee kwa zongo.hospital tunapima homa hakuna yupo safiii ila mtoto hanyonyi ni kulia tu ndio mamaa mmoja jirani akanipa hiyo ya magadi ile kumeogesha tu mtoto alilala usingizi safi na kunyonya vzr.yule mama akasema mwanao kapigwa zongo au kijicho manaake kila mtu mtoto wako mzuri jamani ikabidi nimwambie wife asiwe anatoka nje kwa mda mpaka mtoto atengamae vizuri.binafsi mwanzo nilikuwa siaminigi hivi vitu.mila zipo jamani
Mkuu nipe tiba na mimi nijue maana dogo analia sana hadi nashikwa na wazimu
 
kumbe hadi kwenye mazai linahusika!
nakumbuka zamani kiasi mwanzoni mwa miaka 2000s nilipanda bus la hood kuelrkea Mbeya kutokea Msamvi, so nilipoingia ktk bus hakikuwa na abiria wengi nikajichagulia kukaa seat moja na mdada fulani hivi siwajua tena safari kama huna kitabu cha kusoma basi kaa na mti kupiga stori za hapa na pale ili kufupisha safari.
nilipofika nikamsabahi kama desturi yetu wa afria yule dada aliitikia kwa shari sana siku hofu nikamwmbia naweza kaa hapa! Akanijibu dry saana; kwakweli sikutegemea alivyojibi na nilijikuta nimekereka saana. Nikamtazama na kujisemea moyoni "hii safari kama utafika Mbeya au uendako sijui". nikatafita seat nyingine nikakaa,safari ikaanza tumefika maeno ya ngerengeri mkaguzi wa tiketi huyu anakagua mara paaaah akamfikia bidada kumdai tiketi mdada hana tiketi akaambiwa atoe nailu akasema yeye ni staff kapandiswa gari jamaa fulani hapo msavu akamtaja! Mkagua tiketi akamkazia toa nauli kama hauni utashuka hapo mbele Mzumbr urudi mjini.
Kweli bwana tumefika njia panda ya Mzumbe bus likapati jamaa akaja kampatia mdada elfu moja na akamshusha akamwambia hii nauli urudi mjini!

Nikajikuta natabasamu nikajisemea laiti kama angekubali kuniruhusu kukaa hapo huenda ningemlipia nauli.

baada ya miaka kadhaa ndio najitathmini ile ilikuwa ni nguvu ya namna gani ilitokea hata yule binti kusushwa njiani sawa sawa na nolivyonema moyoni mwangu wakati namtazama baada ya kunzuia kukaa nae!!

Au ndio nguvu hasi ya jicho!?!
Hii kitu imenikuta wiki iliyopita tu,, nilikuwa kwa fundi wangu wa nguo, anae kijana wa dada yake humsaidia majukumu pale,, sasa alipotokea tu ghafla nafsi ikanambia mwambie aendeshe vizuri baiskeli la sivyo itamuangusha,,, ila nikasita kusema hivyo nikanyamaza,,muda ule ule akaagizwa kama dakika 6-10 hivi si akampigia simu mama yake mdogo kuwa kapata ajali, ikabidi akimbie kwenda kukuta kaanguka na baiskeli akiwa peke yake, na alivunjika mguu katikati ya paja,,, nilipata mfadhaiko Sana maana Ni kitu nilikiwaza muda huo huo na kikatokea
 
Back
Top Bottom