Ila bima pia sio lazima kukata unless upo Hazina. Huko nadhani ni lazima uwe na bimaNafahamu faida za bima ila tuwe wawazi aisee....... Imagine kulipia bima maisha Yako yote afu waja fariki kwa ajali na hujawahi kutibiwa zaidi ya malaria
Hii pia nenda hata bima nyingine mfano za magari na kadhalika na kadhalika
Bima na kubet ni same things kama umesoma advanced Probability kuna kitu kinaitwa Poisson distributionTukienda pasu bin pasu kusema kweli bima ni wizi uliohalalishwa
Nhif tetesi za muds mrefu zinasema kuna wakuu walipiga hela, kwa kwa muda mrefu imekua ipo katika upungufu wa hela, ndo maana vikwazo vingi sana nhif,Nhif ndio balaa wameweka vikwazo vingi kwa wategemezi wetu
Sawa sawa, ndio maana mie hata nikiumwa kichwa naenda zangu TMJ au Kairuki HospitalMe huu mwaka bima nimetumia mara 1. Napo sikuwa naumwa nilifosii tu ili itumike.
😁😁 wanatuibia sana bwana. Dec nitapima hiyo FBP
Tena mtu single ndio tunaibiwa sana
Heri familia. Mume, mke & kids. Asipiumwa mume, ataumwa mke or watoto.
Bima ni utapeli tu bora mtu utumie cash
Mwaka jana brother angu alivunjika mguu kwenda Hospital et wanadai Bima haihusiki na upasuaji na ni NHIF ni huzuni
"Bima ni Utapeli tu"
kama hujapata hiyo hasara pesa yako unarudishiwa?Unaponunua Bima, nia ni kuzuia hasara inayoweza kutokea kama ukiwa mgonjwa au ajali kwenye mali zako, unajua exactly utakachopata, Kamari hujui utakachopata kwa hiyo statement yako sio kweli
Wahindi na waarabu ndiyo wanaonufaika sana na hizi Bima ,hasa bima za magari .Nimepita huko mtandaoni yule mdada Diva amepost barua aliyotumiwa na bima yake ya afya, Jubilee Insurance. Barua imemtaka afute post zake kuhusu bima hiyo na aombe radhi kwa kuwa bima yake iliisha tangu 2 Machi 2025.
It seems kwamba Diva alienda hospitali baada ya bima kuisha na alipokosa huduma akaanza kuwashukia wenye bima kwamba hajaumwa mwaka mzima hela yake imeenda wapi?
Katika post ya barua amesema kuwa hatofuta kwa kuwa anapigania haki yake na huku ni kama anahisi atapata bguvu ya Rais kwa kuwa ni CCM.
Sasa najiuliza kama alishawahi kwenda kuomba hela yake mara baada ya bima ya gari kuisha? Kama hajawahi kuomba hela yake anategemea bima za afya zinajiendesha kwa mfumo tofauti na bima za mambo mengine?
Huyu dada muda si mrefu atakuja kuomba mchango wakianza kumdai kwa kuchafua brand kwa jambo ambalo hata wafuasi wake wanamuandikia kumwambia bima sio kikoba lakini amekaza fuvu.
Jiandaeni kumchagia
View attachment 3475796
View attachment 3475797
Nina mengi ya kusema ila viapo vya kazi na taarifa za ndani siruhisiwi kusema ngoja ninyamazeMfumo wa bima bhana....ni kama vile kamari na ndio maana hata kujiunga kwake ni kama kulazimishana Tu......
Imagine unalipia gharama kwa ajili ya majanga ambayo unahisi au kutazamia yatakutokea ndani ya kipindi cha mwaka wa ada ya bima......ina maana kama hakujatokea lolote ni kama vile umeliwa.......
Ni mfano wa mtu aliyebashiri dakika tisini za mpira mambo yasipokuwa kama ulivyotaka imekula kwako
Ni kweli lakini alitakiwa kuuliza na kuelewa hizi habari kabla ya kukubali kuingia kwenye mkataba wa bima.Tukienda pasu bin pasu kusema kweli bima ni wizi uliohalalishwa