Ufanyike mdahalo (Debate) kumaliza utata kuhusu Bandari

Ufanyike mdahalo (Debate) kumaliza utata kuhusu Bandari

Sasa kama Kuna vipengele ambavyo wanajua wazi sio vizuri, nini kinawazuia wasivibadilishe au kurekebisha wakaweka vilivyo vizuri? Sio msahafu huu Wakuu.
Wanaogopa kuongea wazi kisa ni agizo😂
 
NAKUSHAURI utafute MKATABA uusome ACHA uvivu.

Upo WA kiingereza.

Upo WA kiswahili.

Ushindwe wewe?
 
Yes wanawaza kwa ajili ya wananchi though madhaif yapo kama wanadam. Kama saiv TRA inakusanya 7T wakat kuna uwezekano wa kukusanya zaid ya hio if wakimpa sector binafsi why asipewe huyo DP WORLD.

ASEE KWENY SWALA LA BANDAR UPINZAN YOU GAT NOTHING TO OFFER ZAIDI YA BLA BLA NA UPOTOSHAJI
Okay,

Nimekuelewa KADA
 
Sasa kama Kuna vipengele ambavyo wanajua wazi sio vizuri, nini kinawazuia wasivibadilishe au kurekebisha wakaweka vilivyo vizuri? Sio msahafu huu Wakuu.

Ilisikika sauti ikisema Wanangu kwa hili nimeziba masikio. Mwisho wa kunukuu.
 
Pale una debate nini katika kitu kibovu namna ile.
 
Kwema Wakuu?

Kwa sasa MAIN TOPIC au AGENDA nchini ni swala la Bandari. Kuanzia ma ofisini, majumbani, vijiweni, kwenye daladala, bar hizi story zimetapakaa.

Kila mmoja anazungumzia issue za bandari kwa muktadha wake. Wapo wanaoihusisha Bandari na dini, utanganyika v/s uzanzibar, kuibiwa, kuuzwa, u chama, maendeleo etc.

Katika wale wanaopinga huu mkataba, wapo waliokata tamaa kwa maana ya liwalo na liwe, wapo ambao hawajakata tamaa wakijaribu kuelezea huku na kule ikiwamo kuupinga mahakamani, wapo ambao wana matumaini utakuja kubadilishwa baadae.

Ukiacha huku mitaani au mitandaoni tunakojibishana kila Leo, pande zote mbili hazijawahi kukutana pamoja kuulezea au kuelezana why wanaona uko au hauko sawa. Utaona tu viongozi wa Serikali wakiutetea wakiwa wao peke Yao, vivyo hivyo wanaoupinga nao hua peke Yao.

Kwa ukubwa na wingi wa hii mijadala ni wazi kua haitoisha leo wala kesho. Na Serikali Kwa upande mmoja ikiamua kuutekeleza huu mkataba basi upande wa pili utabaki na kinyongo.

Sasa mimi nilikua nina wazo au ushauri. Itafutwe siku moja au mbili, ufanyike mdahalo wa wazi, Serikali v/s Watu kadhaa hivi wanaopinga, labda, kumi kumi kila upande. Mdahalo huu urushwe live kwenye television wananchi tuone au tusikilize kila pande tuuelewe.

Kama hadidu za rejea zitoke kwenye huo mkataba ambao sio Siri tena maana upo mitandaoni. Kijadiliwe kifungu kimoja baada ya kingine. Wanaoona kifungu kina walakini waelezee walikini wao upo wapi na wanaoona kifungu kiko sawa wajibu hoja hizo.

Iwe ni DEBATE ambayo watu watachangia Kwa staha na ustaarabu, sio jazba, vijembe au mihemuko. Isiwe DEBATE kama vile tuko bungeni kwamba wenye kelele nyingi za "ndio" ndo wanakua wameshinda. Bali watu waende point kwa point, neno kwa neno mpaka wafikie muafaka.

Pale upande mmoja utakaposhindwa kwa hoja basi usisite kukubali ili kutopoteza muda waende kwenye kifungu kingine. Mfano wanaoutetea kwamba mkataba unao kikomo wakifanikiwa kuonyesha ukomo ulipo basi wale wanaoupinga wakubali tu.

Debate hii itasaidia hata wale ambao ambao hawaelewi in details bali bendera fuata upepo kuelewa kilichomo humo, kinachopingwa au kutetewa ni kipi. Sababu wako wengine huamua kubisha sababu tu wamemsikia fulani akisema hivi au vile.

Washiriki wa kila upande wapewe taratibu, ratiba na hadidu za rejea za debate hiyo siku kadhaa kabla ili waweze kujiandaa. Isiwe kama ni kesi mahakamani kwamba nani mwenye maswali ya kubana zaidi bali points, data na facts ndio ziongee zaidi.

Tukifanya haya basi tutakua tumefanikiwa kwa kiwango kikubwa kuzima hii mijadala ili watu waendelee na mambo yao mengine, wanaopinga waweze kuukubali ikitokea ni mzuri au wanaoutetea waweze kuurekebisha ikitokea una walakini.

Yangu ni hayo tu Kwa Leo.
Mjadala kama huu utakuwa sawa na maandamano CCM hawawezi kuukukubali
 
Debate ndo itakuletea maendeleo?

Tatizo Watanzania mnaoenda sana kupiga mdomo alafu kazi zero.

Hakuna cha debate wala nini. Uwekezaji uendelee maana tumechelewa sana na muda hauko upande wetu
Tukikaa kimya ndio tutapata maendeleo? Tumechelewa wapi? Nani katuchelewesha? Aliyechelewesha maendeleo NDIO Huyu huyu anayetaka kutuwahisha? Hii akili hata Bata wangu hanayo Mpwa
 
Sasa ni wakati wa Mkuu wa JWTZ kuingilia kati katiba ifuatwe Kama tunavyo elezwa wakati Makamu wa Raisi alipotaka kuporwa kuwa Raisi baada ya kifo Cha Magu

Hivyo na Sasa Jeshi lisikubali nchi kuja kutaifishwa waingilie kati mapema

Nchi itakapo taifishwa JWTZ watalinda Nini?

Mkuu wa Majeshi wakati ni wako Kwa Jambohili

Utakuja kuachiwa manyoya na Waarabu Kuku watamla wao
Ukicheka na Nyani Utavuna mabua

Kazi kwako!!
 
Kwamba watakwepa kama ilivyokua kwenye midahalo ya urais?
Hahaaa wakija siku hio niite Mbwa, Niko paleeeee
20220903_163539.jpg
 
Debate ndo itakuletea maendeleo?

Tatizo Watanzania mnaoenda sana kupiga mdomo alafu kazi zero.

Hakuna cha debate wala nini. Uwekezaji uendelee maana tumechelewa sana na muda hauko upande wetu
Na vijembe na taarabu zitakuletea maendeleo? Umechelewa kwenda wapi na ulikuwa unafanya nini mpaka ndo umegundua umechelewa?
Jamaa kaongea point ya maana sana. Hii nchi ni ya watu wote, tukifanikiwa tunafaidika wote na tukifeli tunaumia wote. Makosa hufanywa na wanadamu, ni kawaida, tatizo ni kushupaza shingo.
Kama kuna nia njema yoyote kwenye mkataba huu, hakuna sababu ya kuogopa kuwakabili wanaopinga, kwa kusikiliza hoja zao na kuzijibu.
Lakini unasikiliza mtu kama Waitara eti kwa kuwa hili jambo limeanzishwa na Mwenyekiti wetu lazima tumuunge mkono,sasa kulikuwa na haja gani ya kupeleka kwenye bunge.
Watu wenye heshima zao na wasio na tabia ya kupinga vitu hadharani wameongea, wamezawadiwa matusi na kejeli. Prof. Shivji aliibuka nyakati zile kuweka hoja kinzani dhidi ya tume ya Warioba kwenye bunge la katiba wote mlishangilia,leo amekosoa mkataba wa bandari anazomewa,sasa kwa nini hata mjinga asitilie shaka hizi jitihada za kuukingia kifua huu mkataba. Hatujachelewa kuchukua hatua za kuisaidia nchi yetu, tuachane na mambo ya kitishana sijui kuitana kwa DCI, vyeo ni vya muda bali Tanzania itaendelea kuwepo.
 
Mkuu umeongea points sana aisee. Yaani umewaza kama mimi. Walioko madarakani kama wanajua wanachokifanya ni sahihi wanaona ugumu gani kuwakabili wanaoupinga?

Katika wanaopinga wako ambao ni wataalam wazuri tu wa mikataba au sheria au vyote. Wakitumika hawa itasaidia hata pengine kurekebisha vipengele kadhaa ambavyo vinaonekana sio sawa.

Shida kuna wenye wanaona mdahalo au kikao cha aina hii ni cha kuwaumbua hivyo bora wasikae. Narudia kauli yako tukifaidika tutafaidika wote na tukiumia pia tutaumia wote, sababu ya wachache.
 
Back
Top Bottom