Ufanyike mdahalo (Debate) kumaliza utata kuhusu Bandari

Sasa kama Kuna vipengele ambavyo wanajua wazi sio vizuri, nini kinawazuia wasivibadilishe au kurekebisha wakaweka vilivyo vizuri? Sio msahafu huu Wakuu.
Wanaogopa kuongea wazi kisa ni agizo😂
 
NAKUSHAURI utafute MKATABA uusome ACHA uvivu.

Upo WA kiingereza.

Upo WA kiswahili.

Ushindwe wewe?
 
Okay,

Nimekuelewa KADA
 
Sasa kama Kuna vipengele ambavyo wanajua wazi sio vizuri, nini kinawazuia wasivibadilishe au kurekebisha wakaweka vilivyo vizuri? Sio msahafu huu Wakuu.

Ilisikika sauti ikisema Wanangu kwa hili nimeziba masikio. Mwisho wa kunukuu.
 
Pale una debate nini katika kitu kibovu namna ile.
 
Mjadala kama huu utakuwa sawa na maandamano CCM hawawezi kuukukubali
 
Debate ndo itakuletea maendeleo?

Tatizo Watanzania mnaoenda sana kupiga mdomo alafu kazi zero.

Hakuna cha debate wala nini. Uwekezaji uendelee maana tumechelewa sana na muda hauko upande wetu
Tukikaa kimya ndio tutapata maendeleo? Tumechelewa wapi? Nani katuchelewesha? Aliyechelewesha maendeleo NDIO Huyu huyu anayetaka kutuwahisha? Hii akili hata Bata wangu hanayo Mpwa
 
Hebu tupange list [emoji1]

Ova
 
Sasa ni wakati wa Mkuu wa JWTZ kuingilia kati katiba ifuatwe Kama tunavyo elezwa wakati Makamu wa Raisi alipotaka kuporwa kuwa Raisi baada ya kifo Cha Magu

Hivyo na Sasa Jeshi lisikubali nchi kuja kutaifishwa waingilie kati mapema

Nchi itakapo taifishwa JWTZ watalinda Nini?


Mkuu wa Majeshi wakati ni wako Kwa Jambohili

Utakuja kuachiwa manyoya na Waarabu Kuku watamla wao
Ukicheka na Nyani Utavuna mabua

Kazi kwako!!
 
wazo zuri sana ila sasa ccm sijui kama watakubali
 
Debate ndo itakuletea maendeleo?

Tatizo Watanzania mnaoenda sana kupiga mdomo alafu kazi zero.

Hakuna cha debate wala nini. Uwekezaji uendelee maana tumechelewa sana na muda hauko upande wetu
Na vijembe na taarabu zitakuletea maendeleo? Umechelewa kwenda wapi na ulikuwa unafanya nini mpaka ndo umegundua umechelewa?
Jamaa kaongea point ya maana sana. Hii nchi ni ya watu wote, tukifanikiwa tunafaidika wote na tukifeli tunaumia wote. Makosa hufanywa na wanadamu, ni kawaida, tatizo ni kushupaza shingo.
Kama kuna nia njema yoyote kwenye mkataba huu, hakuna sababu ya kuogopa kuwakabili wanaopinga, kwa kusikiliza hoja zao na kuzijibu.
Lakini unasikiliza mtu kama Waitara eti kwa kuwa hili jambo limeanzishwa na Mwenyekiti wetu lazima tumuunge mkono,sasa kulikuwa na haja gani ya kupeleka kwenye bunge.
Watu wenye heshima zao na wasio na tabia ya kupinga vitu hadharani wameongea, wamezawadiwa matusi na kejeli. Prof. Shivji aliibuka nyakati zile kuweka hoja kinzani dhidi ya tume ya Warioba kwenye bunge la katiba wote mlishangilia,leo amekosoa mkataba wa bandari anazomewa,sasa kwa nini hata mjinga asitilie shaka hizi jitihada za kuukingia kifua huu mkataba. Hatujachelewa kuchukua hatua za kuisaidia nchi yetu, tuachane na mambo ya kitishana sijui kuitana kwa DCI, vyeo ni vya muda bali Tanzania itaendelea kuwepo.
 
Mkuu umeongea points sana aisee. Yaani umewaza kama mimi. Walioko madarakani kama wanajua wanachokifanya ni sahihi wanaona ugumu gani kuwakabili wanaoupinga?

Katika wanaopinga wako ambao ni wataalam wazuri tu wa mikataba au sheria au vyote. Wakitumika hawa itasaidia hata pengine kurekebisha vipengele kadhaa ambavyo vinaonekana sio sawa.

Shida kuna wenye wanaona mdahalo au kikao cha aina hii ni cha kuwaumbua hivyo bora wasikae. Narudia kauli yako tukifaidika tutafaidika wote na tukiumia pia tutaumia wote, sababu ya wachache.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…