Ufaransa: Afungwa miaka 20 Kwa kumbaka mkewe na kualika wanaume wengine 50 wambake mkewe

Ufaransa: Afungwa miaka 20 Kwa kumbaka mkewe na kualika wanaume wengine 50 wambake mkewe

Ndiyo jamaa kafungwa miaka 20 yeye na wenzake.

Kilichoshangaza watu ni kuwa kundi hilo la wabakaji halitokani na watu wa aina Moja ya jamii au umri.

Ni watu wenye historia tofauti tofauti.
Jamaa alikuwa anakutana nao kwenye internet kwa ku-chat. Hivyo ni kama alikuwa anakuambia hali halisi, ukikubali unapewa masharti ya jinsi ya kwenda kwake na kufanya huo unyama. Na amefanya kwa muda mrefu kweli, zaidi ya miaka kumi. Na wala asingegundulika ila alishikwa shopping center anamrekodi mwanamke mwingine clip ya video kwa kuweka simu chini ya miguu yake ili anase sehemu za ndani ya gauni. Polisi walipoenda kufanya search nyumbani kwake ndiyo wakakutana na hizo clips nyingi za mke wake alizorekodi. Wanaume 50 ndiyo waliweza kujulikana na kufuatilia mawasiliano yake na ´clips alizorekodi. Wengine kama 20 hivi hawajatambulikana. Kweli duniani kuna mambo. Wakati sisi wengine mpenzi wetu akipitiwa na hata mwanamme mmoja tu tunatoa talaka, yeye anatafuta watu wa kumfanyia unyama. Nadhani huu ni ugonjwa mbaya sana.
 
Mwamanaume mmoja huko Ufaransa amefungwa miaka 20 kwa kosa la kumbaka aliyekuwa mkewe na kualika wanaume wengine 50 kumbaka mkewe kwa muda wa miaka 10.

Mwanaume huyo aliyefahamika kwa jina la Dominique Pelicot alikuwa anambaka mkewe Giselle Pelicot (Mrs) baada ya kumpa dawa za usingizi kwa kipindi cha miaka 10 mfululizo.

Pia Dominique akaanza kuwaalika wanaume wengine kuja kumbaka mkewe akiwa hajitambui na kuchukua picha za video wakati mkewe akibakwa na yeye mwenyewe alijichukua video wakati akimbaka mkewe akiwa hajitambui.
duh hii ni balaa sasa
 
Huyo si Mke, alikuwa changudoa wake aliyeshindikana
 
Amefanya hivyo vitendo kwa miaka 10 na ameishi naye kwenye ndoa Kwa miaka 10, ina maana lengo la kumuoa ni hovyo vitendo; kwa hiyo sio mke
Mke hapimwi kwa lengo la kuoa au unamfanyia nini wakati wa ndoa. Huyu ni mke wake ila alikuwa anamfanyia unyama.
 
Huko si ndio tunaambiwa kwenye wastaarabu, mabingwa wa democrasia, walioelimika nk
Ndio.

Au unadhani hao watu 50 ndio pekee wanaoishi huko? Au ulipoambiwa Kuna ustaarabu, demokrasia na elimu Bora basi ukajua ni kwa 100% na hakuna udhaifu hata kidogo? Huoni kuna walioandamana kumsapoti huyo mama na hatua zikachukuliwa?

Njoo huku shithole sasa:

Polisi ndiye anaagiza wahuni wakabake na hachukuliwi hatua yoyote, na ni 'wananzengo' wachache sana wanaoguswa na kupaza sauti kulaani na kutaka haki itendeke.

Utekaji unafanyika mchana kweupe huku 'wananzengo' wakishangaa kama nyumbu, mateka wanateswa wakiwa vituo vya polisi na baadaye kutupwa maporini wakiwa aidha wamekufa au wapo mahututi, na hakuna hatua yoyote inayochukuliwa.

Mtu anapigwa risasi mchana kweupe katika eneo lenye ulinzi wa serikali 24/7 huku CCTV camera za serikali zikimulika, lakini kabla ya tukio ulinzi unaondolewa, camera zinaondolewa baada ya tukio na hakuna uchunguzi wowote unaofanyika!

Viongozi wa vyama pinzani wanaohubiri na kuact kupambania demokrasia hawataki upinzani kwenye nafasi zao, bado hujaja kwenye vituko vya dola kwenye chaguzi katika kukibeba chama twawala kishinde kwa 100/99.9% dhidi ya vyama pinzani.
 
yaani mke wake alikuwa anakataa mpaka anambaka au ilikuaje? na ikawaje akaalika wanaume wengine huyo ni mke wake kabisa??
 
am i missing somethng here?

kwa hyo huyo mwanamke baada ya kutoka kwenye hzo dawa baada ya kubakwa alikuwa hajihisi kitu/tofauti kwenye mwili wake (to be precise kwenye sehemu zake za siri)?
 
Mwamanaume mmoja huko Ufaransa amefungwa miaka 20 kwa kosa la kumbaka aliyekuwa mkewe na kualika wanaume wengine 50 kumbaka mkewe kwa muda wa miaka 10.

Mwanaume huyo aliyefahamika kwa jina la Dominique Pelicot alikuwa anambaka mkewe Giselle Pelicot (Mrs) baada ya kumpa dawa za usingizi kwa kipindi cha miaka 10 mfululizo.

Pia Dominique akaanza kuwaalika wanaume wengine kuja kumbaka mkewe akiwa hajitambui na kuchukua picha za video wakati mkewe akibakwa na yeye mwenyewe alijichukua video wakati akimbaka mkewe akiwa hajitambui.
Siyo mabhangi kweli hayo?
Kwaakili za kawaida linawezekanaje hilo jambo!
 
Back
Top Bottom