Ufaransa: Kwanini walinzi wa Rais Samia wanavaa Barakoa ya Zanzibar kwenye ziara ya Tanzania?

Hoja zenye nguvu kama hizi watu wanajifanya kama hawazioni na tunajua wanapita humu kimya kimya!! Hoja hizi tano hapo juu zinadai majibu yenye akili!! Hasa hoja namba 3 inauma sana!!
 
Zanzibar ni sehemu ya Tanzania.

Kuna ubaya gani?

Wewe ni maamuma! Point ya mleta mada ni kuwa hakuna taifa Zanzibar, kuna serikali ya Zanzibar. Kukipaswa kuwa na serikali ya Tanganyika. Ikiwa huu ni muungano wa nchi mbili, iko wapi bendera ya Tanganyika?? Kwa kinachoendelea kinachozuiliwa ni bendera na alama za serikali ya Tanganyika!! Tanganyika imefichwa katika jamhuri ya muungano wakati Zanzibar ikiruhusiwa kujitambulisha!!

Anazungumzia jambo la maana sana lakini unaleta mzaha. Hakuna ubaya kwa Serikali ya Zanzibar kutambulika, isiwe vibaya ya Tanganyika kutambulika pia na this has nothing to do with Zanzibar au Tanganyika kuwa sehemu ya Tanzania. This is “identity”!!!
 
Mcheza kao hutunzwa. Ndio maisha yetu chini ya jua. Cha muhimu atende haki tu na kukumbuka sisi sote ni wamoja
 
Yule msemaji wa timu ya wananchi anasemaje
 
Nadhani walinzi walitakiwa kuvaa Barakoa zenye bendera ya Tanzania siyo Zanzibar, kwani hii ni ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Siku wakiambatana na Mwinyi ndio wavae hizi barakoa au ni Utalii wa Uchumi wa Bluu?
Kuna kila dalili watu watasema bi mkubwa kawashinikiza wenzake wavae hata kama siyo, maana huyu mama anaandamwa sijui kwanini watz tuko hivyo
 
Kuna kila dalili watu watasema bi mkubwa kawashinikiza wenzake wavae hata kama siyo, maana huyu mama anaandamwa sijui kwanini watz tuko hivyo
Hapana! kuna dhana potofu. Washauri wake walitakiwa walione hilo japo ni jambo dogo.
Rais akiwa na msaidizi nyuma yake pia angeweza kuhoji, akakaa kimya

Alikaa kimya kama ilivyokuwa Zbar kwa Rais wa Zbar kukabidhiwa bendera ya Zanzibar.
Na Rais SSH anajua kuwa yeye ni wa JMT hata kama ni Mzanzibar, hivyo uwepo wa alama nje ya za muungano ni tatizo.

Ukishaanza kuushabikia Uzanzibar lazima Utanganyika utarudi tena kwa nguvu.
Nyerere aliita Tanzania visiwani na Tanzania bara.

Kwanini kudai Tanganyika ni ''jinai'' lakini kujitambulisha kwa Uzanzibar ni halali?

Viongozi wa Zanzibar wanachagiza sana hisia, na muda si mrefu watajikuta wanashindwa kutuliza hisia wanazochochea! Ukiwa na identity ya Zabar ya Tanganyika haikwepeki

Nyalali, Kisanga na Warioba pamoja na Wananchi wote wanasema serikali 3 hazikwepeki.
 

Mwigulu hajaachana na huu ujinga wa kuvaa tai yenye rangi za bendera kumbe!?
 
He made a very good point
Yes, enzi hizo tulikuwa wamoja. Viongozi wa leo wanaendekeza sana Uzanzibar
Maana yake ni kuwa yale yenye manufaa kwa Zanzibar ni ya Wazanzibar. Mfano, ajira za SMZ, Mafuta na gesi waliyokimbiza baada ya kuambiwa kuna mapipa machache.

Yale wanayotaka kufaidika nayo wao ni Watanzania. Kwa mfano, wakitaka ardhi wanasema ni nchi moja. Wakitaka kupitisha bidhaa kwa uchochoro wanasema ni nchi moja. Wakitaka misaada na mikopo ni nchi moja, lakini madeni ni ya JMT si ya Zanzibar

Hapa ndipo hoja isiyojibiwa inakuja.
Ni yapi ya muungano yaliyoitwa kero? na yalitatuliwaje? Mbona hatuambiwi imekuwa siri?

Tanganyika iliwakilishwa na nani katika kero za Zanzibar na JMT?

Hoja inakuja, Zanzibar inachangia nini katika muungano?
Mbona tuna formula ya kugawana hatujui formula ya kuchangia au kulipa madeni?

Ukizungumzia Uzanzibar wewe ni mtu mwema, ukizungumzia Utanganyika hilo ni kosa.

Serikali 3 ni jibu la matatizo vinginevyo ipo siku atakuja Rais na sera nyingine itakuwa tabu
Wanaotaka serikali tatu ni hawa
1. Wazanzibar kupitia katiba ya 1984 toleo la 2010 sura ya kwanza ibara ya 2.
2. Tume ya Jaji Nyalali
3. Tume ya Jaji Kisanga
4. Tume ya Jaji, VP na PM J.Sinde Warioba
4. Wananchi wa Tanzania kupitia tume ya Warioba
 
"Formula ya guwana ipo lakini hamna formula ya kuchangia."
Kwa mara ya kwanza kero za muungano zinatatuliwa na kufanywa siri.
 
Tanganyika ilianzishwa rasmi kama koloni la Mwingereza mwaka 1922 ikauliwa na mchonga meno mwaka 1964. Ilikuwa ni nchi huru miaka 3 tuu (1961-1964) katika historia yake. Sasa kweli hiyo ndiyo nchi mnayotaka irudishwe? Nchi bandia iliyoundwa na mkoloni? Hata ikirudi wala haiwezi kubaki kama nchi muda mrefu, itasambaratika kikabila na kiukanda.

Nyerere alijua hilo na ndiyo maana alivamia Zanzibar. Zanzibar ndiyo nchi ya kweli na yenye historia kabla ya wakoloni hawajafika hapa. Kabla ya kinyang'anyiro cha bara la Afrika, Zanzibar ilikuwepo kama nchi. Na siku huo mnaouita muungano ukivunjika Zanzibar itarudi kuwa nchi huru.
 
Msije huku bara wapuuzi nyie
 
Kukosa Washauri...,

Kuna mambo usipoyafanya hupungukiwi lolote na huenda kuyafanya kwako huvunji sheria ila yanapelekea maneno ambayo yanakutoa kwenye reli au kuongeza shutuma siziso na Afya kwa Taifa
Nakubaliana na wewe kabisa. Mimi naamini katika philosophy inayosema "Just because you can do it, doesn't mean that you should".
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…