MtamaMchungu
JF-Expert Member
- Apr 10, 2011
- 10,115
- 15,057
Hii kauli nitasema daima...
Ukiweza kukwepa kulipa kodi kwenye serikali ya CCM, kwepa bila kusita.
Ukiweza kukwepa kulipa kodi kwenye serikali ya CCM, kwepa bila kusita.
Kwa nilivyomsikiliza Polepole leo, na ile issue ya wanamtandao kutaka kuichezesha katiba rais aongoze nchi kwa miaka 7 huku wana ccm/chawa wakipigia chapuo hilo wazo kipindi kile, na maneno yakasambaa JPM ni dictator anayetaka kuliongoza taifa kwa miaka mingi kinyume na katiba... wengi tulisikia haya...
Kumbe JPM naye kaita watu wake na kukataa wazo hilo... mmoja wapo ni HP...
Kumbe wanamtandao wakiwa na nia ovu ya kumchafua JPM huku wakisifu uongozi wake ni bora zaidi ndio maana aongoze miaka mingi... huku mioyoni wakijua nia yao ni ipi...
Kama walikuwa wanaweza kufanya smart moves kama hizo, nadhani hata suala la kumshambulia mpinzani TAL kipindi kile ni shinikizo la hao hao wanamtandao ili kuchafua taswira ya JPM..
Na lengo lao inawezekana ilikuwa kuonyesha wanamsaidia JPM katika changamoto za kiuongozi... inawezekana walikaa nae kumshauri jambo hilo akawa mzito...
Nina imani JPM kuna uwezekano alikuwa mzito katika kufanya maamuzi hayo kabla wanamtandao hawajamsukuma na kumlaghai wamalize kazi, au walijichukulia maamuzi mikononi mwao...
Nimekuja kugundua kumbe JPM alikuwa na u soft flani ... hakuwa na roho mbaya kiasi hiko ambacho tunaaminishwa.. bali alikuwa mzalendo....
Urefu wa kamba.Hii nchi kuna haja ya nyie mlioko ndani muipambanie