Tetesi: Ufisadi: Inasemekana kila mwanakikundi wa ngoma kutoka Bagamoyo walioenda Marekani matumizi kwa siku ni milioni 3!

Hizi fikra hizi tabu tupu. Mil 3 ni kitu gani kwa ziara ya nje? Hebu tupe mchanganuo wako, ulitaka walipweje? Mbona unakuwa na roho ya kimaskini na kishirikina namna hiyo?
 
Kuna kuidhinishwa kwa kiasi na kupatiwa wahusika hicho kiasi. Kwa watanzania tulivyo usikute hiyo mil. 3 ipo kimaandishi tu kuhalalisha upigaji wa hizo pesa.

Ukute wacheza ngoma wa watu wamelazwa hostel na kuambulia $20 kwa siku kila mmoja wao. Anaekunja baki ya hiyo Mil. 3 ni mwingine kabisa.
 
NB: Karibu Tanzania nchi ambayo bodaboda ukimtazama tu anawasha pikipiki 😄
 
Kama ni watoto wa masikini sawa tu
Ila kama wacheza ngoma ni watoto wa mawaziri Basi tuandamane
 
at least wanakula maskini wenzetu kuliko wangekula mafisadi ya ccm
 

Sasa milioni tatu kwa kikundi cha watu tena Marekani hiyo nayo hela?

JPM alikuwa anaenda Chato na watu kibao wanaenda nae bado wanaoenda kuapishwa chato mbona hukuandika?

Acheni nongwa kila analofanya SSH mnaona ni kosa mbona kwa JPM hamkuandika kila kitu?
 
Umeshawahi kufika New York ukaishi japo siku 3? Jiji la New York ni miongoni mwa majiji Ghari zaidi.

milioni 3 ni hela ya kawaida tu; hawajaenda kufanya kazi ya bure wamekwenda kwa malipo, ulitaka apewe nani hiyo fedha?
 
They deserve it though..
 
Kwanini uzinduzi usingefanyikia Tanzania kwenye bunga zenyewe?
 
Ila hii awamu sijui ya 6 ni kama hamna kitu kabisa, yaani watu wanajipandishia bei za vitu na nauli (hasa bajaj) kiholela kana kwamba hakuna mamlaka za kudhibiti!.

Hivi Waziri Mkuu yupo kweli??!?!
Makamu wa Rais je??!!

Halafu eti wanapita barabarani na misururu ya magari halafu wananchi tunasimamishwa kuwapisha wapite!!!.

Sent from my SM-J530F using JamiiForums mobile app
 

Kama mwanakikundi wa ngoma kutoka Bagamoyo walioenda Marekani na JK yuko huko.​

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…