VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,137
- 17,908
Baada ya miaka kadhaa, leo nimeingia na kuwemo Ofisi Ndogo za CCM Lumumba kikazi. Katika kupitiatia nyaraka za haraka zisizo na baraka, nikanusa ufisadi ndani ya chama changu pendwa. Ni ufisadi uliofanyika kupitia uhamisho wa Maktibu wa Wilaya wa CCM. Kama kada mbobevu, mwerevu na mzalendo mpingaufisadi ni vyema niibue jambo hili ili lishughulikiwe kichama haraka.
Makatibu wa Wilaya wa CCM walihamishwa vituo va kazi. Wakalipwa mamilioni ya pesa kufanikisha uhamisho wao. Huko walikohamishiwa hawakukaa hata miezi sita. Karibu wote wakahamishwa tena (wengine wakirejeshwa kwenye vituo vyao vya awali). Wakalipwa tena pesa za uhamisho kutoka chamani. Sasa wamerejea palepale walipokuwa awali wakiwa wamelamba pesa za uhamisho mara mbili.
Mfano wa haraka kwenye nyaraka nilizoziona ni Katibu wa CCM Wilaya ya Kinondoni. Huyu alihamishiwa Wilaya mjawapo huko Katavi. Na amerejeshwa tena Kinondoni palepale na kwa cheo kile kile. Haya ni matumizi mabaya ya fedha za chama. Huu ni ufisadi. Nani hasa chamani mwetu yuko nyuma na ufisadi huu? CCM kama chama tawala tunapaswa kuwa mstari wa mbele kupambana na wizi na ufisadi. Tujitenge na ufisadi.
UVIKO-19 upo, tuendelee kuchukua hatua!
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam