Yaan hata sijui nianzie wapi kulieleza hili,,ibada ni jambo lolote ambalo Mungu analipenda,iwe ni kwa vitendo au kwa maneno
Sasa kusaidia watu ni ibada na ni jambo ambalo linapaswa kufanywa kila siku katika maisha yetu
Lakini ibada hii ya kuchinja inakuja kwa mwaka mara moja na ni tendo la kukumbuka tukio maalumu lililo tokea enzi za nabii ibrahim pale alipo oteshwa ndoto na Allah kama mtihani wa kutekeleza agizo lake la kumchinja mwane ili kudhibitisha imani yake
Kwahiyo ibrahim alifaulu pale alipokuwa tayar kutekeleza agizo hilo kwa kumchinja mwanae Ismail/ishamael ,ndipo Allah akashusha kondoo toka mbinguni achinjwe badala ya kumchinja mwanae
Sasa ibada hii hufanyika baada ya mahujaji kumaliza kutekeleza ibada ya hija na ndio kuchinja kunafuatia
Kwahiyo naona umepata picha kwamba hii ni ibada maalumu na haihusiani na kufanya matendo mengine nje ya hapo
Kwahiyo nyama inatolewa kama sadaka tu lkn ibada ipo kwenye kuchinja
Asante