Ufugaji Mbuzi wa kienyeji (Asili) kibiashara


Chukulia kenya kama wapo Uganda wana ushuru mkubwa mno
 
Hata kama kuna ukweli lakini kauli yako ni ya kukatish tmaa
 
Nawasalimuni kwa jina la Mungu naomba niwataarifu nyote MAVUNO FARM wamesha leta mbegu za Mbuzi Red kalahare toka south afrika ukihitaji karibu sana 0713 544411 Mwenyekiti TAGOFA. 0713 282 715 MD mAVUNO FARM.
Karibuni sana .
 
Mimi pia NAOMBA muongozo nipo Geita MWAKA wa tatu bado Kuna Elimu ninakosa hasa nimesikia ishu ya vitamins na chokaaa pamoja na jiwe ingawa mbegu nishaanza kufahamu je hiyo ya mbuzi kumpanda mama ake ikoje
 
Hivi najiuliza wizara ya Kilimo na mifugo wameshindwa kutuletea mbegu ya Boer ya sampo hata wakachukue mabeberu na majike 2000 wayalete na kuyapeleka pale SUA ili waanze kuyabreed na kutengeneza mbegu za kusambaza kwa wafugaji?!
 
Hivi najiuliza wizara ya Kilimo na mifugo wameshindwa kutuletea mbegu ya Boer ya sampo hata wakachukue mabeberu na majike 2000 wayalete na kuyapeleka pale SUA ili waanze kuyabreed na kutengeneza mbegu za kusambaza kwa wafugaji?!
Nimefuatilia sana na kuangalia insta na YouTube
Nimefanikiwa kuwaona baada ya mdau kunipa mwanya kidogo
Wapo na wanauzwa sasa kwenye ranch
Hata Dodoma wapo pia
Wengine hawauzi Boer bali wanakupa cross breed yao ila ni wakubwa pia

Kwa sasa nikihitaji ntawapata Tz
Nimehangaika sana kuuliza mpaka nikawaona YouTube
Unaweza kuangalia YouTube
Boer goats in Tanzania utawaona sehemu nyingi hata Dar pia

Ila ni kupata wafugaji bora na wataalamu na kufika mwenyewe kuwaona usije ukauziwa kwenye gunia
 
Nikweli ulicho kisema TALIRI MPWAPWA walikuwa wanafanya utafiti wa mbegu na walikuwa na Boer walimcross na hawa wakienyeji na walizalisha mbegu nzuri sana ila kumbuka kituo ni cha serekali hapo sasa kuna wakati waliporomoka vibaya sana. Walizalisha Mbuzi gogo white, blended, malia, hao wote walikuwa wazuri sana. Ukienda TALIRI TANGA wao wanafanya utafiti wa Mbuzi saa nene wale wa maziwa wakiwa cross na wakienyeji ili waweze kutoa maziwa bila shida kwenye ukanda wa pwani, sasa shida inakuja hapa ukihitaji kupata hizo mbegu ndio shida unalipia na kusubiria kwa miezi 3 mpaka 4 na siku ukienda kuchukuwa hawakuruhusu kuchagua unaletewa mbuzi basi wewe ni kumchukuwa hata akiwa mzee, kwa ujumla sasa TZ bado tupo nyuma tukiwategemea hawa vituo vya serekali nazungumza kwa uzoefu wangu.
 
Hivi wakilishwa chakula kizuri hakuna uwezekano wakaongezeka ukubwa na uzito na wasiwe na udumavu?
Hata siku moja hawaongezeki hawaongezeki kwasababu ya vinasaba vyao vya uasilia, wao hata ukiwa cross bado ukuwaji wao hauendi kama hawa wenye vinasaba ya miili mikubwa. Ninawafuga hao na ukuwaji wao ni tofauti kabisa na kama isiolo/Galla, au wengine wa kisasa.
 
Hivi najiuliza wizara ya Kilimo na mifugo wameshindwa kutuletea mbegu ya Boer ya sampo hata wakachukue mabeberu na majike 2000 wayalete na kuyapeleka pale SUA ili waanze kuyabreed na kutengeneza mbegu za kusambaza kwa wafugaji?!
Mkuu ni kweli walishawahi kuleta lakini shida iliyopo ni moja tu Mbegu zinaletwa ila usimamizi unakuwaje? tulikuwa na SKU Mbeya, sasa ukienda utalia kisa usiamamizi mbovu walio lianzisha walipotoka basi tulio baki tukalimaliza, ukienda hizo NARCO RANCHESE ndio balaa kabisa, sasa ili kujikomboa ndio maana tukajikusanya na kuanzisha TAGOFA na miunganiko kwaajili ya kujiletea mabadiliko ktk ufugaji, kuna baadhi ya wanachama wa TAGOFA sasa wanaleta hizo mbegu bora kabisa toka huko Afrika ya kusini na zina patikana hapa hapa nchini bila shida kabisa. Rejea post zangu zilizo pita nilitoa taarifa na mawasiliano ya jinsi ya kupata hizo mbegu bila shida.
 

Mambo ya hovyo kabisa yani ulipie wakucheleweshe kisha siku ya kuchukua mbuzi wanakupa yeyote?
 
Mambo ya hovyo kabisa yani ulipie wakucheleweshe kisha siku ya kuchukua mbuzi wanakupa yeyote?
Ndio hivyo wanavyo fanya, ukiwapigia watakupokea vizuri nakukupatia number fasta ya kulipia ngoma inakuja kupata huyo mfugo sasa duh!
 
Dar upo sehemu gani mkuu?
 
Hata mimi ndani ya mwaka huo nina mipango kama yako.
 
Mkuu uliwapata?
Kama bado nikuunganishe na jamaa yupo hapa Masaka anao wengi tu.
 
Ushauri wangu jitahidi baba asipande mwanae yaani uchanganye damu usirudie uzao ukapanda uzao unaofuta utapata wanyama bora sana. Japo sio lazima ni wewe na uwezo wako
Je ? Wakipandana uzao wa pili?
 
MUBENDE na wadau wote habarini??

Nimesoma uzi wote sijaona mahali palipozungumzia kuwa mbuzi toka anazaliwa mpaka kufikia kuwa mkubwa na mzuri wa kuliwa ni muda gani?? Natamani nijue hasa hawa wetu wa kienyeji!!
 
MUBENDE na wadau wote habarini??

Nimesoma uzi wote sijaona mahali palipozungumzia kuwa mbuzi toka anazaliwa mpaka kufikia kuwa mkubwa na mzuri wa kuliwa ni muda gani?? Natamani nijue hasa hawa wetu wa kienyeji!!

..kwa mbuzi wa kienyeji inaweza kuchukua mwaka mmoja, mpaka mmoja na nusu.

..mbuzi wa kisasi pure breed, au mbuzi chotara, inaweza kuchukua miezi sita mpaka miezi minane.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…