Asantee mkuu, japo umejibu kwa kuchelewa lakini ninasaidiwaje Mimi ninayetoka mkoani(Moro)?Naomba nikutoe hofu,
Gharama zetu za mafunzo ni rahisi kabisa.
Utapewa Mafunzo kwa vitendo, chakula, cheti, Kitabu kwa bei kati ya 50,000/= - 75,000/= kulingana na muda.
Kumbuka sisi ni Shirika lisilo la faida, hivyo lengo letu mi kusaidia jamii.
Sent using Jamii Forums mobile app
Pole sana kwa kuchelewa kujibu;Asantee mkuu, japo umejibu kwa kuchelewa lakini ninasaidiwaje Mimi ninayetoka mkoani(Moro)?
Daima toa bila kukumbuka na Pokea bila kusahau
Pole sana kwa kuchelewa kujibu;
Mizinga yetu inakufikia hapo ulipo.
Aidha kama Tenda ni kubwa, tutaandaa vifaa vyote na kuja kuvionganishia hapo site kwako.
Kuna huduma ya Starter Kit kwa Wafugaji wapya;
Kwa huduma hii utalipia 3.5M.
Utapewa;
- Mizinga 10 ya kisasa iliyo na nyuki.
- Mavazi pair 2 yaliyo kamili kwanzia juu hadi chini.
- Vifaa vyote vya kulinia asali; brush, folk and hive tools.
- Bomba la moshi (Smoker)
- Tutakupatia Mtaalamu wa kuusimamia mradi wako kwa mwezi mmoja akikupatia mafunzo.
- Vifaa vya kuhifadhi asali
- Package za asali.
Na ushauri na saha.
Pia, tutakupatia soko la asali.
Sent using Jamii Forums mobile app
Ahsante,Naomba kuuliza yafuatayo
1. Unaweza kuelezea matumizi ya hizo bidhaa mfano chamvua? Na jelly
2. Naweza kutumia nyumba ambayo walikuwa wanaoshi watu kisha wakahama ikiwa ina madirisha yenye nondo tu na iko porini?
3.sehemu ya kufugia Nyuki ni lazima iwe na maua yanayoonekana au likiwa pori tu, tuna assume hapo maua yapo?
Kwenye chumba kimoja kama cha kuishi inaweza kuwekwa mizinga mingapi ya kisasa?
Asante
Sent using Jamii Forums mobile app
Ahsante kwa Maswali Mazuri,
1. Elimu ya Kuzalisha, Kugawa, Kuunganisha na Kuhamisha Makundi ya Nyuki, ni muhimu sana kwa mfugaji. Kundi moja la nyuki linaweza kuzalisha makundi mengi ndani ya muda wote wa mradi wako. Jitahidi uwasiliane nasi kupata elimu hii katika Program zetu mikoa yote Tanzania.
Sent using Jamii Forums mobile app
Ahsante kwa jibu zuri,Nitajitahidi kuwepo kwenye mafunzo yatakayo fanyika Zanzibar mwezi ujao, japo mda unaonekana kuwa tatizo kwangu.
kabla ya kuhudhulia kwenye mafunzo ninahitaji kuamua kwanza kama nafanya mradi huu ama lah; ili kufanya uamuzi sahihi nahitaji uafafanuzi zaidi kutoka jibu lako namba moja.
Kwa uzoefu wako, unadhani ianweza kuchukua mda gani kwa kundi moja kujaza mizinga 10+ kama elimu ya kuzalisha na kugawa na kuhamisha imetumika? ukizingatika kuwa sehemu mradi utakapofanyika kuna maji ya kutosha na chakula (pembezon mwa mto ambapo panalimwa matikiti, migomba na mahindi N.k
Asante sana.
Ahsante sana.Mkuu , Asante kwa maelezo mazuri na yenye tija.Nina maswali machache;
1. Uhakika wa masoko wa bidhaa za nyuki upoje?
2. Ipi bidhaa ghali zaidi katika bidhaa za nyuki?
3.Kwa mtu ambaye hana eneo lake binafi mna mpango gani wa kumuwezesha ili awekeze hapo.Kwa mfano, tumeona kampuni nyingine zinatoa maeneo yao halafu wateja wanawekeza kwenye mradi kwa makubaliano maalum
4.Kwa mtu mwenye eneo lake ,je huwa mnafanya survey na kumshauri kama linafaa au halifai?? na kama halifai mnaweza mkalifanya lifae?
Basi naomba tuwasiliane kupitia simu 0758789956 nipe namba yako
Ahsante kwa jibu zuri,
Mambo matatu ya muhimu;
1. Sisi tukikupatia Mzinga, tunakupatia na nyuki wake. Ilikuondoa tatizo la Ukosefu ma Makundi ya nyuki kwenye Mizinga iliyopo shambani.
2. Kuwepo na kila kitu shambani sio sababu tosha ya kasi ya ugawaji wa makundi, pamoja na mambo yote elimu itakusaidia kupata ujuzi ambao utakusaidia kufanya maamuzi.
- kundi moja linaweza kugawanywa na kutosha Mizinga Mipya mitatu, miwili au mmoja, hivyo hakuna kanuni Maalumu Bali ni kwa kutumia ujuzi.
3. Hata hivyo kwa kawaida nyuki wanaweza kutengeneza Malkia wapya kati ya 11 - 49. Na kila Malkia anatakiwa awe na kundi jipya la nyuki.
Tafadhali, ni muhimu kufika kwenda mafunzo
Sent using Jamii Forums mobile app
Mizinga ipo ya bei tofauti tofauti, ukinunua Mizinga yetu nyuki tunatoa kama huduma.Maswali mengine kutokamajibu namba 2 na 3
-- Garama zenu za mzing apamoja na Nyuki ni shilingi ngapi?
- Je inatumia mda gani kwa nyuki kuzalisha malkia 11 - 49 (wastani)
Asante.
Habari yako mkuu, nimevutiwa ma kichwa cha habari hapo nje, sasa nimeingia ndani ili nipate hiyo elimu kuhusiana na mzee nyuki na asali yake lakini nimeambua patupu sasa bado hijaiweka au mpaka tubadilishane namba za sim au tukutane pm?.Karibu RAFIKI ASALI ujipatie elimu ya ufugaji na kilimo Nyuki kutoka kwa wataalamu na wenye elimu ya sayansi na teknologia ya ufugaji Nyuki na mazao yake
Bosi wangu nta tunatumia katika kuwavutia nyuki lakini ufugaji wa nyuki unahitajika kwanza kua na eneo ambalo ni sahihi la Ufugaji. Kama utahitaji tungeweza kuwasiliana ili niweze kutembelea eneo lako na kukushauri cha kufanya. 0758789957 kwa mawasiliano zaidiBoss mi nina Mizinga kama 40 but nyuki wanasuasua kuingia niliwawekea nta lakini nimeambulia patupu nitumie njia gani waingie??
Nimekuelewa xana mkuu ila kama nivyoandika katika Uzi wangu lakini ukitaka kujua mengi naomba tuwasilianeHabari yako mkuu, nimevutiwa ma kichwa cha habari hapo nje, sasa nimeingia ndani ili nipate hiyo elimu kuhusiana na mzee nyuki na asali yake lakini nimeambua patupu sasa bado hijaiweka au mpaka tubadilishane namba za sim au tukutane pm?.
Naomba itendee haki heading ya uzi wako
Ni hayo tu mkuu.
Wasalaam.
Sent using Jamii Forums mobile app