Habarini za mchana wapendwa, natumaini kuwa mu wazima wa afya njema kabisa,
niende moja kwa moja kwenye maada;-
Nahitaji kufanya biashara ya ufugaji wa nyuki kwa kuanza na mizinga 100, kutokana na ufinyu wa eneo nililo nalo pamoja na mtaji nilio nao na hapa kuna mtaalamu wa kutengeneza mizinga pamoja na kuita nyuki ameshapatikana.
Kwa kuwa sina elimu yoyote ya ufugaji wa nyuki nimekuja kwenu kuomba ushauri kwa yeyote mwenye utaalamu kuhusiana na biashara hii anisaidie hatua ninazotakiwa kuzifuata ili niweze kufanya biashara hii kihalali.