Sifa za eneo:-
1. Miti, uoto wowote wa asili na mimea mbalimbali kama mazao ya chakula na biashara (alizeti, mahindi etc)
2. Maji ni muhimu kwan hutumika kama sehemu ya chakula cha nyuki pia nyuki hutumia maji kurekebisha hali ya hewa ndan ya mzinga
3. Eneo la shamba la nyuki lazima liwe ni salama kwa mizinga, mazao yake, mifugo, binadamu na mahali kusiko na maadui wa nyuki. (Kuthibiti hayo yote kujengea nyumba ya nyuki ni njia nzuri na salama zaidi)
4. Kivuli cha kadri na kinga ya upepo ili kuwapunguzia nyuki kazi ya ubebaji maji kwaajili ya kupunguza joto.
Sent from my iPhone using JamiiForums