Ufugaji wa kisasa wa Nyuki: Faida, Utaalam na Masoko

Ufugaji wa kisasa wa Nyuki: Faida, Utaalam na Masoko

Ndugu wataalamu wa nyuki hebu tupe maelezo kidogo ya maswali yangu haya hapa chini.

  1. Wapo nyuki wadogo na nyuki wakubwa. Je ni aina ipi hasa ina faida nyingi na rahisi kufuga?
  2. Ni maeneo gani ya nchi yetu yenye malisho mazuri na mengi kwa kufuga nyuki?
  3. Je gharama za kufuga nyuki hadi kuvuna asali ziko vipi?
  4. Mizinga ya aina gani inahitajika kwa nyuki wakubwa na nyuki wadogo na inapatikana wapi na kwa gharama gani?
  5. Soko la asali liko vipi hapa nchini?
  6. Ni changamoto zipi wanazokabiliana nazo wafugaji wa nyuki?

Karibu FBY 2013
 
Habari,

Kampuni yetu ya Central Park Bees Limited inakuja na Starter KIT iliyokamilika ya kukuwezesha wewe kuingia katika biashara ya ufugaji wa nyuki kwa njia ya kisasa na yenye mafanikio makubwa.

Kwa wateja wetu tutaweza kutoa msaada kwa mwaka mzima pale utapoitajika pia kuhakikisha mizinga yako iko katika hali nzuri wakati wote na mteja hatotakiwa kuwaza kuhusu soko kwasababu kampuni yetu itahusika na kununua asali yote toka kwa mteja na kufanya malipo mara moja bila kuchelewesha.

KIT yetu itakua na orodha ya vitu vifuatavyo:-
  1. Langstroth bee hives
  2. Bee smoker
  3. Protective bee suits with gloves
  4. Hive tool
  5. Bee brush
  6. Fork
  7. Stainless steel sieve
  8. 3 frame manual honey extractor
  9. Practical training in our farm

Kupitia training yetu utaweza kujifunza jinsi ya kutumia vifaa vyote hapo juu na pia kujifunza ufugaji bora wa nyuki kwa vitendo katika shamba letu na jinsi gani utajiingizia pesa nyingi kupitia hii biashara.

Sababu za kutuchagua sisi:-
  1. Uhakika wa soko
  2. Vifaa vya kisasa hivyo kupekea asali yenye kuhitajika katika soko la kimataifa
  3. Bei za ushindani za vifaa

NB: Kwa sasa shamba letu la mfano lipo Dodoma ila tuko katika mchakato wa kuanzisha katika mikoa tofauti.

Gharama ya KIT nzima nimeainisha katika PDF hapo chini na marejesho ya mtaji wako ni ndani ya mwaka mmoja tu, miaka inayofuata ni faida kwako.

Mizinga yetu ina guarantee ya kuishi zaidi ya miaka 20 bila shida yoyote.

Mawasiliano:
0689 658811
info@centralparkbees.co.tz
 
Attachments

  • CENTRAL PARK BEES COMPLETE STARTER KIT.pdf
    CENTRAL PARK BEES COMPLETE STARTER KIT.pdf
    347.9 KB · Views: 766
  • IMG_3081.JPG
    IMG_3081.JPG
    454.3 KB · Views: 753
  • CENTRAL PARK BEES - PRICE LIST.pdf
    CENTRAL PARK BEES - PRICE LIST.pdf
    339.4 KB · Views: 619
Ni mradi mzuri sana. Hayo mafunzo kwa vitendo utaratibu wake ukoje kwa watu ambao hawapo Dodoma!
 
Kwa ambao hawako Dodoma tutajitahid kufika shambani kwako ila itakua vizuri zaidi ukifanikisha kuja kupata mafunzo katika shamba letu. Tunafanyia kazi suala la kuwa na shamba darasa katika mikoa mingine.

Hebu nisaidie mkoa wa pwqni wilaya kisarawe naweza kufuga nyuki?
 
Hebu nisaidie mkoa wa pwqni wilaya kisarawe naweza kufuga nyuki?

Unaweza kufuga nyuki mkoa wa Pwani, kwani Tanzania tuna nyuki wa aina tatu. Nyuki wa Pwani, wa nyanda za juu kusini na nyuki wa mikoa ya kati kama Dodoma, Singida n.k.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Unaweza kufuga nyuki mkoa wa Pwani, kwani Tanzania tuna nyuki wa aina tatu. Nyuki wa Pwani, wa nyanda za juu kusini na nyuki wa mikoa ya kati kama Dodoma, Singida n.k.

Sent from my iPhone using JamiiForums[/QUOTE

Nimepitia attachment yako umeeleza kuwa mzinga mmoja unatoa kilo 12 kwa mvuno mmoja na umesema unavuna mara tano. Kweli inawezekana kuvuna mara tano?je ujazo wa hiyo mizinga ni kiasi gani?Ukiacha hiyo starter kit je bei ya mzinga mmoja ni sh ngapi kama mtu anataka kununua mizinga peke yake?
Mimi naishi dodoma,je nawezaje kuja kuona shamba darasa lenu?
Ninataka kuanza huu mradi mwaka huu mwishoni.
 
Ndiyo inawezekana kuvuna kiasi hicho na pia kuvuna mara tano au zaidi inawezekana. Kwasababu mizinga inayotumika ni ya kisasa ambayo ina Brood box na Super box na wewe utakua ukivuna sehemu ya super box pekee hivyo kuwezesha mzinga wako kuwa na nyuki muda wote kwani hutokua ukiwafukuza wakati wa kulina asali.

Mfano kwa Dodoma kuna misimu ya maua mara mbili kwa mwaka, kipindi cha msimu nyuki hujaza Super box ndani ya muda wa week tatu, kwahiyo kila baada ya week tatu una uhakika wa kuvuna Super box yako na kuirejesha katika mzinga.

Ni ruksa kutembelea shamba letu na utapata maelezo zaidi tena kwa vitendo kabisa.
Kuhusu bei ya mzinga mmoja mmoja naweka Price List hapa kwa ajili yako na wengine watakao fuata. Ahsante sana
Unaweza kufuga nyuki mkoa wa Pwani, kwani Tanzania tuna nyuki wa aina tatu. Nyuki wa Pwani, wa nyanda za juu kusini na nyuki wa mikoa ya kati kama Dodoma, Singida n.k.

Sent from my iPhone using JamiiForums[/QUOTE

Nimepitia attachment yako umeeleza kuwa mzinga mmoja unatoa kilo 12 kwa mvuno mmoja na umesema unavuna mara tano. Kweli inawezekana kuvuna mara tano?je ujazo wa hiyo mizinga ni kiasi gani?Ukiacha hiyo starter kit je bei ya mzinga mmoja ni sh ngapi kama mtu anataka kununua mizinga peke yake?
Mimi naishi dodoma,je nawezaje kuja kuona shamba darasa lenu?
Ninataka kuanza huu mradi mwaka huu mwishoni.
 
Unaweza kufuga nyuki mkoa wa Pwani, kwani Tanzania tuna nyuki wa aina tatu. Nyuki wa Pwani, wa nyanda za juu kusini na nyuki wa mikoa ya kati kama Dodoma, Singida n.k.

Sent from my iPhone using JamiiForums

Nashukuru kwa maelezo yako. Ni vitu gani muhimu vinahitajika ili kufuga nyuki?
 
Nashukuru kwa maelezo yako. Ni vitu gani muhimu vinahitajika ili kufuga nyuki?

Sifa za eneo:-
1. Miti, uoto wowote wa asili na mimea mbalimbali kama mazao ya chakula na biashara (alizeti, mahindi etc)
2. Maji ni muhimu kwan hutumika kama sehemu ya chakula cha nyuki pia nyuki hutumia maji kurekebisha hali ya hewa ndan ya mzinga
3. Eneo la shamba la nyuki lazima liwe ni salama kwa mizinga, mazao yake, mifugo, binadamu na mahali kusiko na maadui wa nyuki. (Kuthibiti hayo yote kujengea nyumba ya nyuki ni njia nzuri na salama zaidi)
4. Kivuli cha kadri na kinga ya upepo ili kuwapunguzia nyuki kazi ya ubebaji maji kwaajili ya kupunguza joto.

Mkuu ili ufugaji uwe wa kibiashara ninatakiwa nianze na mizinga mingapi? Vile vile utupe bei ya mzinga wa nyuki wa kisasa
 
Kuna swala naona limekua likichanganya watu, naomba niliweke sawa.

Tunaposema Kgs12/hive haina maana mzinga mzima ndo una uwezo wa kutoa kilo hizo. Mzinga wa Langstroth umegawanjika katika sehemu kuu mbili; 1. Brood box 2. Super box, wakati wa kulina asali utatoa Super Box pekee kwani ndo huwa na asali ambayo haina matoto ya nyuki na mayai ya nyuk kwan kuna kifaa kinaitwa Queen Excluder huwekwa katikatika ya Brood box na Super box ili kumfanya malikia wa nyuki asifike sehemu ya juu.

Maana ya Brood box ni kuwezesha mzinga wako kuwa na nyuki wakati wote hata baada ya kulina asali na pia huwapa nyuki akiba ya chakula kwa ile asali iliyo katika brood box.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Nimeona mapori mengi yanayofaa kwa ufugaji wa nyuki ila nahofia moto. Ni kawaida kwa haya mapori kuchomwa moto kila mwaka. Hii haiwezi kuwa ni kikwazo kikubwa kwenye ufugaji wa nyuki?.
 
Mkuu ili ufugaji uwe wa kibiashara ninatakiwa nianze na mizinga mingapi? Vile vile utupe bei ya mzinga wa nyuki wa kisasa

Kwa ufugaji wa kibiashara nashauri angalau mtu kuwa na mizinga kuanzia 50 kwenda mbele.

Hesabu yake:
1hive = 12kgs/harvest (Minimum)
Ndani ya mwaka 1 unaweza kuvuna mara 5, hivyo;

50 Hives = 600kgs

600Kgs * 5 harvest = 3000Kgs

Wholesale price:
1kg = 7000 Tshs
3000Kgs = Tshs 21,000,000/=

NB: Katika mahesabu hayo tumefanya katika range ya chini sana.

Bei ya mzinga mmoja ni Tshs 150,000/=

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Nimeona mapori mengi yanayofaa kwa ufugaji wa nyuki ila nahofia moto. Ni kawaida kwa haya mapori kuchomwa moto kila mwaka. Hii haiwezi kuwa ni kikwazo kikubwa kwenye ufugaji wa nyuki?.

Labda kama utakua umefika na kuvamia pori bila kufuata taratibu, lakini nnavojua mikoa mingi na vitongoj vyake ukienda kuomba eneo kwaajili ya ufugaj wa nyuki huwa sio tatizo. Kikubwa uwe na uhakika eneo unalopewa halijaachwa kwa matumizi ya baadae kama ujenzi n.k

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Back
Top Bottom