Kecha Boksi
Member
- Nov 5, 2010
- 55
- 109
Kuna njia mbalimbali za kuwavutia nyuki waweze kuinhabit mizinga mipya. Njia kubwa kabisa na ya kisasa ambayo mimi huwa natumia ni matumizi ya nta (wax sheets). Hapa huwa naweka wax sheets kwenye vibao vya ndani ya mizinga yangu na harufu yake huwavutia nyuki na kuwafanya waingie kwenye mzinga. Njia nyingine ambayo pia husaidia nyuki waingie kwenye mzinga ni matumizi ya majani ya mchai chai (unapaka kidogo sehemu ya mlango wa mzinga na ndani ya mzinga). Pia unaweza tumia "majani ya kufukuzia mbu" na kuyasmear ndani ya mzinga, harufu yake inavutia sana nyuki.
Kama unakuwa na mzinga mingi na ufugaji wa kisasa, ukipata makundi kwenye mzinga michache unaweza kufanya colony division na kumultiply makundi yako kwenye mizinga mingine. Mfano, kama una mizinga kumi na umepata nyuki kwenye mitano, colony division itakusaidia kupata makundi kwenye mizinga mitano liliyobaki ndani ya muda mfupi. Hii njia inahitaji utaalam kidogo ila ni rahisi na haina gharama.

alan unafanyaje ili nyuki waweze kuinhabit mzinga mpya?