Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
mimi nnazalisha makundi yangu mwenye ya nyuki na muda si mrefu ntaanza uza kwa yeyote anaehitaji,ishu ya kutundika mizinga miezi 6 unagoja nyuki kuingia ndani yake ni mambo ya mwaka 47
WADOGO NA WAKUBWA wakubwa ni mpaka liter 60 mzinga mmoja kwa mwakautauza bei gani mkuu?, nyuki wa aina gani? ukubwa wa mzinga na matarajio ya urinaji wa asali ni kiasi gani kwa lita?
Hongera mkuu kwa kuelimisha kuhusu Nyuki,Natumai elimu hii wangeipata pia wale jamaa wa kwa PM kule Zuzu - Dom ingewasaidia sana.Shamba lina zaid ya mizinga 100 lakin ni mizinga mi 5 tu ndo ina Nyuki.
Wadau (wataalamu) naomba ushauri wenu kuhusu hii biashara.
Nataka ni-invest 25,000,000 Tshs ktk mradi wa ufugaji wa nyuki wa kisasa.
Je, ufugaji huu unafaa ktk mikoa ya Pwani km vile Bagamoyo (Fukoyasi/ Kiwangwa)?
Nahitaji nitafute eneo la kama ekari 25 ambapo nitatumia ekari 5-15 ktk mradi huu.
Kama inawezekana, naweza kuweka mizinga mingapi kwa hiyo 25M (hii haihusishi gharama za kununua shamba na kupata hati miliki.
mkuu Malila napenda kujua jinsi ya kuwafanya nyuki waingie kwenye mzinga mpya,na pia wakati wowote katika mwaka nyuki wanaweza kuhamia kwny mzinga mpya au huwa wana kipindi chao maalum.....naomba msaada juu ya hayo japo bado nina maswali
Asante sana Malila.Si mtalaam wa nyuki, ila kwa kiasi ninachojua, mikoa ya pwani huwezi kupata mavuno mazuri, yaani hata asali inayopatikana inaweza isitoshe hata kuwalisha nyuki wenyewe, pili unaweza pata taabu kupata makoloni ya kutosha mizinga yako kwa sababu deswarming haifanyiki.
Mkoko Bagamoyo kuna nyuki wengi, sijui uzalishaji wake, pia nimeona mizinga mipya ya kisasa michache Madesa Msata juzi hapa.Sijui kama imepata nyuki au la.
Morogoro/Iringa/Tanga, hii ni mikoa ya karibu kama uko Dar ambako unaweza kuwekeza kwa mafanikio sababu chakula cha nyuki ni kingi. Lindi pia nimewahi kuona mitaa ya Malendego. Ila kama unataka kupata asali organic nenda Uvinza Kigoma,Mkinga tabora nk.
mkuu Malila napenda kujua jinsi ya kuwafanya nyuki waingie kwenye mzinga mpya,na pia wakati wowote katika mwaka nyuki wanaweza kuhamia kwny mzinga mpya au huwa wana kipindi chao maalum.....naomba msaada juu ya hayo japo bado nina maswali
Nyuki kuhamia kwenye mizinga kuna nta maalumu ya kuwaita .Kikubwa shambani kwako unatakiwa ulime mzao ya maua kama alizeti pia kuwepo ma bwawa la maji karibu .Kama unahitaji elimu zaidi ya nyuki pm
Kuna njia tatu zinazowafanya nyuki wahamie ktk mzinga mpya.
1. Deswarming, hii ni njia ambayo hutokea kwa sababu nyuki wamekuwa wengi hivyo hujigawa nusu kwa nusu, koloni moja huhamia sehemu nyingine na malikia mpya.Njia hii mara nyingi iko sana ktk maeneo ambayo chakula cha nyuki ni kingi.
2. Njia ya pili ni ya kuwawekea nta au pro polis ktk mzinga mpya. Watahamia mzinga huu kwa deswarming au kutafuta usalama zaidi.
3. Kutafuta usalama wao. Pamoja na ukali wao wote, lakini nao wanaogopa kufa. Kama kutakuwa na mazingira mabovu na yasiyo salama nyuki watahama na kuhamia airtel !!!!!!!. Hapa kuna mambo kama ukosefu wa chakula,vurugu,maji hakuna,moto, wanyama kama paka pori nk.
Kwa ufupi hizi ndio njia zilizozoeleka kwa wengi.
Kuna maua gani mengine ya kupanda zaidi ya alizeti?
Na mizinga inatakiwa kuwa iwe na umbali gani toka ardhini?
Vipi kama shamba lina kisima, inaweza kuwa mbadala wa bwawa?
Inachukua muda gani mpaka mavuno ya kwanza?