Mbali na hilo wahtimu wenyewe hujiona kama ni watu wakubwa saaaana
Kuna mashamba kibao ya watu binafsi na wawekezaji ambao wao kama wao wangeenda kujitolea kwa muda ili kupata mtaji wa kuanzisha mashamba yao madogo na uzoefu kutokana na viposho.
Wengi wamekimbilia mjini na ukiwauliza makwao huko wameacha mashamba tena ya bure ya familia zao,sasa wanataka kuishi Dar ili walime lami?
Hivi nani hapa ambae familia yake haina shamba kwao huko,na naninani anataka kurudi kwao,utumwa wa akili.
Hata Raisi afanye vipi,akama akili zetu wenyewe hazitabadilika na usomi kuwa kwa uhalisia basi tutafeli,na hatimae wale wasio na elim ndio wanaonekana sana kufanikiwa kwenye kilimo kwa kuelekezana wao kwa wao