Ndugu wadau wa jukwaa hili nawasalimu nyoote.
Mm ni mtanzania, kijana ninayejitahidi kutumia nguvu zangu kujiwezesha kiuchumi kwa njia halali.....baada ya kukaa na kuwaza nn cha kufanya katika mazingira yangu, nimeona fursa kubwa na nzuri ya kufuga nyuki baada ya kudokezewa kiduchu na mtu mmoja katika mazungumzo yetu.
.
Naomba mnipe msaada wa mawazo namna ya kuanzisha ufugaji huu na uendeshaji wake na kiujumla masuala ya msingi yanayohitajika katika ufugaji wa nyuki.
.
Asanteni.
UFUGAJI WA NYUKI
Hatua zinazostahili kufuatwa unapoanzisha mradi wa ufugaji wa nyuki.
Hatua ya kwanza katika mikakati ya mradi wa ufugaji wa nyuki ni kupata ufahamu wa uhusiano baina ya nyuki na mwanadamu katika eneo lako.Zungumza na wale wanaojihusisha na nyuki.Andamana nao wakifanya kazi na nyuki.
Ikiwa hauna ujuzi wa kufanya kazi na nyuki,kuna uwezekano wa kujifunza mengi kutoka kwa wafugaji wa nyuki katika eneo lako.Kwa kufahamu jinsi wanavyofanya kazi,unaweza kutoa maoni ya kuboresha kwa kustahilika,na itakuwa rahisi kutumia teknolojia ya ufugaji wa nyuki inayofaa katika eneo lako.
Pia unafaa kupitia visa kadhaa vya kung’atwa kabla ya kujitolea kufuga nyuki.Kung’atwa na nyuki ni sehemu muhimu katika ufugaji wa nyuki.Mfugaji wa nyuki anapaswa kukabiliana nayo.
Pindi tu unapoelewa uhusiano baina ya nyuki wa kienyeji na mwanadamu,mawazo ya kuanzisha utaratibiu ulioboreshwa unaweza kuundwa.Yafuatwayo ni maswali yanayofaa kutiliwa maanani:
1. Ni nani wa kufanya kazi naye?
2. Vifaa gani vinafaa kutumiwa?
3. Ni wapi pa kuuza bidhaa za mzinga?
Ikiwa ndio unaanza na nyuki itakuwa bora ikiwa unafanya kazi na mtu mmoja ama wawili katika eneo lako.Kwa kuchagua wakulima wanaoheshimika na uhusiano mzuri na jamii juhudi zako zitaongezeka maradufu.Ukifuga nyuki mwenyewe na kutumia utaratibu tofauti na ule unaotumiwa katika sehemu yako ni hatua katika mwelekeo unaofaa. Habari zitasambaa na punde ama baadaye utakuwa ukizungumza na marafiki ama majirani zako kuhusu ufugaji wa nyuki.
Mara kwa mara anza ufugaji wa nyuki na angalau mizinga miwili.Hii itakupatia fursa kulinganisha maendeleo baina ya mizinga na la muhimu zaidi, inaruhusu mradi kuendelea ikiwa koloni moja itaangamia. Pia udhibiti wa mizinga yote badala ya mzinga mmoja binafsi unaweza kusisitizwa.
Mabadiliko huchukua muda.Ni lazima kuanza na wazo. Utoaji wa kufanikiwa wa wazo ni matarajio yanayoweza kutimilika ili kuanzisha utaratibu bora kwa uhusiano baina ya nyuki na binadamu katika maeneo mengine.
Katika kupanga mradi, weka malengo yanayoweza kutimilika. Mradi mdogo, unaofaulu, una maana kuliko mkubwa uliojaribiwa na haukufaulu.
Vifaa vitakavyotumiwa kwenye mradi hutugemea hali iliyoko. Unafaa kutathmini uwepo wa vifaa vinavyohitajika vile vile pia msaada wa kiufundi uliopo katika kuchagua aina ya ama aina za vifaa vya mzinga vinavyofaa.
Tambua watu katika sehemu yako wanaoweza kutengeneza vifaa vya ufugaji wa nyuki ujenzi wake unaweza kuwa mafanikio kivyake.Inawza kuhitaji uvimilivu unaporatibu kupata vifaa pamoja.
Milango ya uuzaji iliyopo kwa bidhaa za mzinga katika maeneo mengi. Tafuta watu ambao tayari wanatumia asali ama nta ya nyuki. Mara kwa maara wana hamu ya usambazaji thabiti wa bidhaa za hali ya juu. Ikiwa hawatumii asali, waoka mikate na watengenezaji wa peremende wana uwezekano wa kutoa soko.Watafute pia wale ambao wanaweza kutoa soko kwa nta ya nyuki.
AINA ZA MIZINGA.
Mzinga wa langstroth
Mzinga wa Langstroth ni mfano wa mzinga wenye fremu inayosonga na ndio hutumiwa kwa sana.Fremu zimetenganishwa kutoka kwa ukuta wa mzinga na kwa fremu zingine na nafasi ya nyuki. Mizinga mingi ya Langstroth ina masanduku ya kuweka fremu kumi,lakini mizinga ya fremu nane na kumi na mbili pia hutumiwa. Kama kigezo ukubwa na baadhi ya michoro hutofautiana kutoka kwa nchi hadi nchi ni muhimu kununua mizinga na vifuniko vya mizinga kutoka kwa muuzaji mmoja.
Mzinga wa Langstsroth una:-
Kifuniko cha juu ama paa , Kifuniko cha ndani, Chumba cha asali, Chumba cha uzazi, Ubao wa chini, Ubao wa kushukia na stendi.
Mzinga wenye ubao wa juu
Mizinga hii hutengenezwa kupunguza gharama na kama mbadala kwa mitambo na mizinga ya Langstroth.Ni maarufu kwa saababu ya urahisi wake na bei yake isiyo ghali,katika nchi zinazoendelea.Miziwnga yenye kibao cha juu pia ina fremu zinazosonga na hutumia wazo la nafasi ya nyuki.
Mzinga mwenye kibao cha juu unaitwa hivyo kwa sababu fremu za mzinga huu zina tuu kibao cha juu,na sio kibao cha kando ama cha chini.Mfugaji wa nyuki hatoi msingi(hutoa tu msingi mdogo)kwa nyuki kuanzia ujenzi.Nyuki hujenga sega kwa hivyo huning’inia chini kutoka ubao wa juu .
Tofauti na mzinga wa Langstroth, asali inaweza kutolewa kwa mwendo unaoenda nje kwa sababu fremu ya mziniga mwenye kibao cha juu hauhitaji msingi madhubuti ama fremu kamili.Kwa sababu nyuki hawana budi kujenga sega baada ya kila vuno,mzinga mwenye kibao cha juu huzalisha nta nyingi na asali chache.Hata hivyo kama mzinga wa Langstsroth,nyuki wanaweza kufanywa wahifadhi asali kando na sehemu wanayolea nyuki wachanga ili nyuki wachache wauawe wakati wa kuvuna asali kutoka kwa mzinga wenye kibao cha juu.
KUVUNA ASALI NA NTA.
Asali huvunwa mwisho wa msimu wa maua. Mfugaji wa nyuki huchagua masega yenye asali iliyokomaa, iliyofunikwa na rusu laini ya nta. Sega linaweza kukatwa katika vipande na kuuzwa kama sega bichi la asali ama kuvunjwa na kuchungwa na kichungi kutenganisha asali kutoka kwa nta.
Sega ambalo nyuki hutengeneza kiota limetengenezwa kwa nta na linaweza kuuzwa.Nta inaweza kuhifadhiwa hadi ya kutosha imekusanywa kuyeyuka juu ya maji kutengeneza pande kubwa.Wafugaji wengi wa nyuki hutupa lnta bila kujua,thamani yake.Inaweza kutumiwa kama njia ya kuzuia maji kupita na kuimarisha ngozi na pamba, katika batiki,kutengeneza mishumaa na katika mafuta kadhaa ya nywele na krimu za ngozi. Mingi ya nta kwenye soko la dunia hutolewa Afrika.
Vifaa
Vingi vya vifaa vinavyohitajika kwa ufugaji mdogo wa nyuki vinaweza kutengenezwa na mafundi vijijini.
Smoker
Mfugaji wa nyuki anahitaji chanzo tulivu cha moshi kuwatuliza nyuki anapovuna asali. moshi huu hutengenezwa na smoka.Smoka ina sanduku la chanzo cha kawi lenye kinyesi cha ng’ombe kinachoungua polepole, kadibodi,lenye viriba. Mfugaji wa nyuki hutumia smoka karibu na lango la mzinga kabla ya kufunguliwa, na polepole huziwekea nyuki moshi ili ziondoke kutoka sehemu moja ya mzinga hadi nyingine. Nyuki hukabiliana na moshi kwa kujaza asali kwa hivyo kupunguza uwezekano wao wa kung’ata.
Sanduku la chuma lina faneli yenye mwelekeo iliyotegemea juu, hivyo kuruhusu chanzo cha kawi kuingizwa ndani.
Chanzo cha kawi huwekwa sehemu ya chini na rafu ya chuma yenye matundu juu ya shimo la hewa.
Viriba, vilivyo katika sehemu ya kulia, hutumiwa kupulizia hewa hadi kwenye sanduku la moto kupitia mashimo yaliyo mkabala.
Ni muhimu moshi tuu na sio moto unatoka kenye smoka na moto unafaa kuzimwa pindi tuu unapomaliziwa kutumiwa
Nguo za kujikinga
Nguo za kujikinga zinahitajika katika ufugaji wa nyuki ili kuepuka kung’atwa na nyuki,ambako kunaweza kusababisha majeraha machungu.Sehemu ya mwili iliyo muhimu zadi kuikinga ni uso,haswa macho na mdomo;Kofia ya neti yenye ukingo mpana itafanya hili. Nguo zingine zinaweza kuvaliwa, zikiwemo glovu,viatu na surupwenye. Nguo nyeupe zinashauriwa ,kwani nyuki wana uwezekano mkubwa wa kung’ata nguo nyeusi. Chochote unachovaa, hakikisha nguo haziko wazi na nyuki haziwezi kupitia kwani hii inaweza kuwa chungu.
Vyombo vya mzinga
Chombo cha mzinga ni kipande cha chuma kinachotumiwa kufungua masanduku, kugwaruza vipande vya nta,kutenganisha fremu kutoka kwa vitegemezi na kadhalika.Vinaweza kutengenezwa kutoka kwa vipande tambarare vya chuma cha pua;bisibisi mara kwa mara hutumiwa.Visu vizee vinaweza kutumiwa lakini hunyumbulika na havitoi nguvu ya wenzo ya kutosha.
Kufuga nyuki na kuzalisha asali kwa mtindo wa kisasa kwa kujenga nyumba ya nyuki inamwezesha mfugaji kuongeza uzalishaji pamoja na kipato.
Ufugaji wa nyuki ni kazi ambayo imekuwepo na kudumu kwa karne nyingi sana. Shughuli ya ufugaji wa nyuki nchini Tanzania hasa katika mkoa wa Tabora ambao ni maarufu kwa uzalishaji wa asali, ilianza kutambulika rasmi tangu mwaka 1884, wakoloni kama vile Rebman na Craft walipofika katika eneo hilo.
Katika kipindi hicho, jamii ya eneo hilo walikuwa wanafuga nyuki kwenye magome ya miti, vibuyu, vyungu, mapango, vichuguu na kwenye miamba. Baada ya muda ufugaji ulipiga hatua kidogo na watu wengi wakawa wanafuga kwa kutumia mizinga iliyochongwa kutoka kwenye magogo ya miti. Ufugaji wa aina hii umedumu kwa karne nyingi kote nchini Tanzania.
Kutokana na uhitaji na ongezeko la matumizi ya bidhaa za nyuki, kulifanyika tafiti mbalimbali ambazo ziliweza kuboresha ufugaji wa nyuki kwa kuwa na mizinga ya kisasa ambayo imewezesha uzalishaji wa asali kuwa mkubwa na kuongeza pato la wafugaji tofauti na ilivyokuwa hapo awali. Tafiti hazikuishia kwenye kuboresha mizinga tu, ila siku hadi siku kunavumbuliwa namna bora zaidi za kuimarisha uzalishaji wa nyuki. Katika makala hii, tutazungumzia namna ambavyo unaweza kuwajengea nyuki nyumba ili kuboresha mazingira yao ya uzalishaji, na hatimae kupata ufanisi zaidi.
Nyumba ya nyuki
Hii ni aina mpya ya ufugaji wa nyuki ambapo unaweza kujenga kibanda au nyumba kisha kuweka mizinga idadi unayohitaj
Ni kwa nini kujenga nyumba au kibanda?
• Ni muhimu kufuga nyuki kwenye kibanda au kwenye nyumba kwa sababu inasaidia kudhibiti wizi wa mizinga, pamoja na wanyama wanaokula asali na kudhuru nyuki.
• Inarahisisha utunzaji wa mizinga na kuwafanya nyuki wasihame kwenda sehemu nyingine.
• Inasaidia watu wengi kujifunza namna nzuri ya ufugaji wa nyuki, ikiwa ni pamoja na watoto, jambo ambalo linafanya shughuli hii kuwa endelevu.
• Ufugaji wa aina hii unasaidia kuwak inga nyuki dhidi ya majanga kama vile moto, na mafuriko.
• Inawaepusha nyuki na usumbufu unaoweza kuwafanya wasizalishe kwa kiwango kinachotakiwa.
• Uzalishaji unaongezeka. Hii ni kwa sababu mizinga inayotumika ni ile ya kibiashara. Mzinga 1 unapata asali kilo 30 sawa na lita 20.
Aina ya nyumba
Unaweza kujenga nyumba yenye upana wa futi 3 na urefu wa futi 9. Nyumba hii inaweza kuchukua miz kooinga hamsini. Halikadhalika, unaweza kujenga kibanda chenye ukubwa sawa na huo.
Eneo linalofaa.....
Naomba kuishia hapo asante.