Ufugaji wa kuku chotara na kienyeji kwa mijini ni hasara tupu

Ushazoea broiler anaiva na viungo vyote vya upishi pamoja
 
Na ukaandika tena
Duuuh umefukua kaburi uzi wa kitambo kidogo, of course nilitaka kuandika kitu in regards to ufugaji kuku nikafuta nikabaki kuwa mpenzi msomaji.....kwahiyo hapo nimewaza kwa Sauti nika-reply ili uzi usipotee ili niendelee kuwa mpenzi msomaji wa comments pindi wanapoweka comments nakuta kialama cha notification
 
Kuku wa kienyeji kuwafuga kwa kulenga zaidi matumizi ya familia kiafya ni bora sana kibiashara watakugharim. Epuka kula broilers fuga nyumbani kuku wa kienyej watoto wako pia wale mayai ya kienyeji. Wale kuku wa wiki6 achana nao.
Nimezingatia hili sikuhzi nikijisikia namwambia Wife andaa mazingira natoa kitu

Ni muda mrefu sijakula broiler na siwataki
 
Hao broiler pia ni pasua kichwa...

My experience tangu nikiwa mdogo nasoma primary mzee alifuga layers na baadae nikiwa mtu mzima akafuga broilers....kote huko hakuna alichoambulia zaidi ya hasara na eventually miradi yote ilikufa.

Nimekuwa nikijaribu kuelewa kwanini small scale poultry farmers hawatoboi na observation yangu ni hii: Supply chain ya poultry inadhibitiwa na two major key players: watengezaji/wasambazaji wa vyakula na wauza vifaranga.

Wauza vifaranga
Hawa wanazalisha vifaranga in batches...kwa hiyo wafugaji nao wanapata vifaranga in batches, implying kuna kipindi fulani maalum wafugaji wa eneo fulani watapelekewa vifaranga kwa wakati mmoja...mkianza kufuga kwa wakati mmoja, mtatoa kuku mfano broilers kwa wakati mmoja na kulijaza soko la eneo lenu kwa wakati mmoja. Supply inapozidi demand kama ilivyo wakati wa mavuno ya mazao mengine tuyajuayo, bei huanguka...

Ili uweze kuishinda changamoto hii ni aidha uwe na uwezo wa kuzalisha vifaranga wako ili upishane na wenzio(hii ni investment inayojitegemea kwa resources na know how) au ikiwa utachukua vifaranga sawa na wenzio basi uwe na uwezo wa kuchelewesha kuingiza product sokoni mfano unachinja na kuhifadhi(freezing) kisha kuingiza sokoni baadae.

Kwa kuwa hawa players hawana ushindani, wanaweza kuongeza bei kadiri watakavyo lakini small scale farmer akashindwa kwa kuwa supply ipo controlled na kila anapoingiza product sokoni anakuta soko limefurika...maumivu yake ni mateso endelevu kwa small scale farmers(majority).

Watengezaji/wasambazaji wa vyakula
Hawa nao wanadhibiti bei, wanaweza kuichezesha wanavyotaka. Farmers don''t have much choices kwa kuwa suppliers ni wachache na pengine wana cartels za kuchezesha bei.

Conclusion
Hizo key areas mbili kwenye supply chain ndiyo zinawaumiza na kuwamaliza poultry famers walio katika small scale level.
Ili utoboe ni sharti uweze kudhibiti hizo areas mbili: uzalishe chakula chako na uzalishe vifaranga wako. Hayo mawili siyo mepesi kwa wafugaji wadogo wanotafuta pesa ya kujikimu.

Wasalaam.
 
Utafiti perfect kabisa huu
 
Najiuliza sana mkuu unafanyaje ufugaji? Mbona nafuga kroiler na profits ipo ya kutosha sana tu?
 
Ahsante sana comrade wewe ni jembe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…