Ufugaji wa kuku chotara na kienyeji kwa mijini ni hasara tupu

Umechelewa sana kujua hili. Fuga kuku wa mayai au nyama. Hawa broiler ni watamu sana, ila bahati mbaya watu hawawafugi hadi wakakomaa..Wengi wanauza kwa wiki 4, badala ya 8 zinazopendekezwa.

Na hii inachangiwa na kuku kuuzwa kama kuku na siyo kwa kilo. Nadhani ifike wakati sasa kuku wauzwe kwa kilo ili flwafugaji wawalishe vizuri.
Sometimes huwa napita pale Shekilango asubuhi nakuona kuku wa nyama wanavyouzwa pale... Yani ni hovyo sana..

Vikuku vidogoo wiki 3 a4 na wamevilisha madawa sana. Wanavijaza kwenye magunia mtu anabeba kama mzigo. Ni ukatili na kulishwa vibudu tu.
 
Umechelewa sana kujua hili. Fuga kuku wa mayai au nyama. Hawa broiler ni watamu sana, ila bahati mbaya watu hawawafugi hadi wakakomaa..Wengi wanauza kwa wiki 4, badala ya 8 zinazopendekezwa.

Na hii inachangiwa na kuku kuuzwa kama kuku na siyo kwa kilo. Nadhani ifike wakati sasa kuku wauzwe kwa kilo ili flwafugaji wawalishe vizuri.
Ninakubaliana kabisa nawe kuhusu huo mstari wako wa mwisho. Biashara ya kuku sasa itatoka kwenye kuuzwa kama kuku, na kuuzwa kibiashara kwa kilo.

Kuhusu ufugaji wa kuku wa mayai, hata huko usidhani kuna nafuu sana. Gharama za ufugaji zinapanda sana bila ya mpangilio wowote, hasa gharama za chakula.
Na hapo hapo, ni muhimu, watu waelewe kwamba ufugaji, uwe wa kuku wa nyama au mayai, usitegemee faida kama unafuga kuku 100, 200, nakadhalika.
Ukitaka kuwa mfugaji kwa faida, fuga 1,000, 5,000, 10,000 na kuendelea. Lakini hili nalo litategemea uwepo wa soko la kutosha. Unafuga kuku wa mayai 10,000, na unapata tray za mayai maelfu kwa siku, mayai utayauza wapi?
Hali ni hiyo hiyo, hata kwenye kuku wa nyama.
 
Yani ukifuga kuku wa kisasa wa nyama kamwe hurudii kufuga wa kienyeji. Chotara wenyewe utawafuga kwa ajili ya familia tu.
Ufugaji wa kuku wa kienyeji ni kwaajili ya familia kumchinjia mgeni au kuchinja kwaajili ya sikukuu mbalimbali,.
 
jirani yangu ana chotara wake jogoo anauza 35,000 mtetea 20,000 mpk 25,000. Nikamuuliza, hiyo bei ya hao kuku wana nini cha maana mpk mteja atoe misimbazi mitatu kisa ananunua kuku hata kilo tatu hajafikisha. Kwenye kuku 100 ashauza wawili
 
Dah!

WaTanzania bhwanaah, hatuna jambo tunalowekea umakini. Ni kama kila kitu ni mzaha mzaha tu!

Bandiko lako hapa limenifanya nicheke kwa jinsi ulivyorahisisha ufugaji wa hawa kuku.

Ni wazi kabisa wewe siyo mfugaji. Kuwa na vikuku viwili , tano au hata mia tano siyo ufugaji huo wa kuingiza faida. Siyo ufugaji wa kibiashara unaozungumziwa kwenye mada hii.

Nikwambie wazi kabisa, ulivyoandika hapa, wewe siyo mfugaji. Hata gharama zako za ufugaji, huzijui.

Kwa hiyo usipotoshe watu tu kudhani kwamba ufugaji ni kazi rahisi.
Mkuu ufugaji wa mjini ni kama alivyokujibu huyo mchangiaji na wengi wanatumia njia hiyo kupunguza gharama za kuhudumia mifugo.
Baada ya kubainika chakula ni gharama kubwa wengi hununua vyakula kwaajili ya hatua za mwanzo za kukuza vifaranga, kisha mfugaji hujenga urafiki na mama ntilie au wenye hotel na migahawa ya chakula kuhifadhiwa mabaki ya chakula kwaajili ya mifugo.
Hata wafugaji wa mbuzi utakuta anahifadhiwa maganda ya viazi na wakaanga chips ambao wapo wengi hapa mjini na ana uhakika wa kupata maganda kila siku.
Pia kwa wafugaji wa ndege na nguruwe wengi huchukua mabaki ya wali, ugali, na mboga za majani zinazopatika kwa wauza chakula kwaajili ya kulisha mifugo yao.

Sent from my TECNO KC6 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu 'ministrant,' asante sana kwa maelezo yako, ambayo si mageni kwangu, hata kidogo.

Kama huo ndio ufugaji unaozungumziwa hapa, sina shida sana nao, kwa sababu huo siyo ufugaji wa uhakika, wa kibiashara kama ulivyoelezwa kule mwanzo kabisa ya mada na mdau mmoja aliyeeleza jinsi anavyopeleka mafungu ya kuku kila wiki sokoni.

Huu unaouzungumzia hapa ni ufugaji wa kienyeji tu, wa kubahatisha, na sana sana ni wa mifugo michache sana.
Hayo mabaki ya chakula huwezi kuwa na mategemeo nayo kwa uhakika, kuwa utayapata kila unapohitaji, na muda si muda nayo utaambiwa ulipie kwa gharama kubwa.
Wewe chukulia mfano wa pumba za mahindi tu, kama mfano. Miaka ya hivi karibuni tu, pumba zilikuwa ni kama uchafu tu wenye gharama kwa wenye mashine za kusaga. Leo hii pumba ni sehemu ya mali ghafi muhimu sana ambayo huwezi kwenda kuzoa tu!

Kwa hiyo hii siyo biashara, ni kama 'hobby' tu wanayofanya watu, na kuchukulia kuwa ni biashara..
 
Hakuna mtu mwenye kuku 10000 yuko humu humu tuko wa kuku 10 mpaka 1000 kama kwako ni wachache na siyo wa biashara sawa ila wengine hao ndiyo tunaendeshea maisha

Sent from my CPH1823 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu, 'msukuma fekero', wewe kweli utakuwa ni 'fake' kwa kila kitu.

Ufuge kuku 10, halafu useme "unaendeshea maisha" na hao kuku 10!

Nikwambie waziwazi bila kukuficha, hata kuku 500, hasa kwa hao chotara, huwezi kuwafuga kwa njia hiyo ya kutegemea mabaki ya vyakula na matakataka, halafu ukaja hapa na kudai umepata faida na "kuendeshea maisha."

Siandiki haya kwa kubahatisha. Ninaandika haya kwa kujua ninachoandika, na kuwa na uzoefu nacho.
 
Labda ungemuuliza anaposema kuendesha maisha anamaanisha nn? Huenda wewe unawaza kodi, usafiri, chakula, matibabu wakati yeye anawaza mambo tofauti.
 
"Kuendesha maisha kwa mambo tofauti", kukoje mkuu wangu 'Tsh', hebu eleza kidogo tujue.

Kupata ada kwa ajili ya watoto shuleni; gharama za kulipia kodi ya pango, au mambo gani?

Hata kama "kuendeshea maisha" ni kuhonga vimada, sioni jinsi gani kiasi hicho cha pesa itokanayo na ufugaji wa kuku 10, unavyoweza kuimudu gharama hiyo!

Kumbuka, hapa tunazungumzia, hao kuku waweze kurudisha gharama zao za kuwanunua, kuwalisha na mambo mengine yooote; halafu pesa ibakie ambayo itakuwa ni faida baada ya kuwauza. Hii faida nayo itakuwa inayo migawanyo yake mingi mingine, na baada ya hapo ndipo upate hicho kiasi unachokiita cha "kuendeshea maisha"! Inawezekana hiyo?

Jameni, tuache utani katika mambo muhimu kama haya. Tunapokuja hapa na kuwadanganya watu waone hii ni kazi rahisi ya kupata pato, kumbe ukweli ni tofauti kabisa!
 
Kuna vijiji Tsh elf 40 aliyouza kuku 4 inamtunza mfugaji mwezi mzima. Ndo maana nikasema labda umuulize anaposema anafanya maisha kwa kuku anamaanisha maisha yapi?
 
Back
Top Bottom