Mkuu 'KING KIGODA', mi naona ni kukosa kuelewana tu kati yako na mleta mada.
Ukisoma mada yake kwa makini utaelewa kuwa kaweka ushahidi kabisa wa anayoyazungumzia. Ukitaka, piga hesabu kabisa, utaona hasara inayotokana na ufugaji wa hao chotara na kuwategemea kuwa chanzo cha pato.
Wewe, kama ni mfugaji wa hao kuku, na unadai unao uwezo wa kuuza kuku 100 hadi 150 kwa wiki. Itapendeza sana nawe ukiweka ushahidi kama alivyoweka yeye, yaani, katika kuwahudumia hao kuku, hadi uwauze, hivi ni kweli kwamba unapata faida?
Hili ndilo swali linalotaka ushahidi
Kwa wafugaji wadogowadogo kifamilia, wenye uwezo wa kuuza kuku mmoja, wawili au hata watano kwa wiki, hawa hawana habari ya faida wala hasara, kwa vile, kwanza hata gharama za ufugaji hawana habari nazo, na kuku wenyewe hawahitaji kulishwa kama wanaofugwa kwa kuuza kwa faida.
Weka hesabu zako hapa, tuone unavyomudu biashara yako hiyo na kuifanya iwe endelevu.
Ukifanya hivyo sote tutaelewa na tutanyamaza, au tutakuunga mkono na kukupongeza kwa njia zako hizo.
Nikwambie ukweli mtupu: kama njia zako umeweza kufuga kuku hao na kuingiza faida, basi jipange vizuri kuwa mfugaji wa mfano/kuigwa, siyo Tanzania pekee, bali Africa kote, na pengine duniani kote.