Kuna vijiji Tsh elf 40 aliyouza kuku 4 inamtunza mfugaji mwezi mzima. Ndo maana nikasema labda umuulize anaposema anafanya maisha kwa kuku anamaanisha maisha yapi?
LOOOooo!
Hakika hili linawezekana.
Lakini mjadala ni huu.
Huyu mfugaji kule kijijini aliwanunua hawa kuku 10 wakiwa vifaranga, au siyo? Kwa hiyo hapo tayari anahesabu gharama ya kuwanunua.
Tokea siku hiyo aliyowanunua hao vifaranga, kuna gharama za kuwahudumia, ambazo wengi huwa hawapendi kuziainisha ili zijulikane; kwa mfano kuwapa ujoto katika siku na wiki za mwanzo. Hapa utasema sijui anatumia jiko la mkaa analopikia chakula yeye mwenyewe, lakini kiuhakika hapo kuna gharama zinazotakiwa kuwekwa kwenye hesabu ya ufugaji wa hao vifaranga hadi watimize umri wasiohitaji joto la nje.
Wakati huo huo, limesemwa kwenye mada hii kwamba hawa kuku wanatakiwa wapewe chakula stahiki, na siyo matakataka tu wakati wakiwa wachanga, ili wakishafikia umri fulani waweze kuendelea vizuri, hata wakipewa mabaki ya chakula na matakataka mengine. Hii gharama ya chakula cha awali ni kubwa kwa hali ya sasa. Hiyo 40,000/ uliyoweka hapo juu kwa mauzo ya kuku 4, bado itakuwa haitoshelezi kununua mfuko mmoja wa chakula hicho.
Kwa hiyo utaona kwamba, hii elfu 40,000/ atakayoipata mfugaji wa hao kuku 10, tayari siyo faida, bali hapo sasa anakula mtaji wake wa awali!
Na bado, hao kuku pengine watahitaji chanjo, kuzuia magonjwa, na hata dawa wakati wanapopata maradhi wakati wa ufugaji.
Sasa baada ya yote haya, na bado yapo mengine tu juu ya gharama za kuwatunza hawa kuku hadi kufikia umri wa kuwapeleka sokoni, hiyo 40,000/ kweli unadhani ndiyo hela inayopatikana kama faida, juu ya mtaji ambayo mfugaji huyu anaweza kuitumia "kumtunza mfugaji"?
Tafadhali, mkuu wangu 'Tsh', hebu niambie ukweli wako.
Hii ndiyo sababu watu wengi sana huko vijijini hushindwa kujua kama wanapata manufaa katika kazi zao wanazozifanya, kwa sababu hawatofautishi pesa yao waliyowekeza, na faida inayotokana na kazi yenyewe.