KING KIGODA
JF-Expert Member
- Dec 28, 2018
- 3,893
- 3,145
HEeeenHeeee. Inabidi kucheka tu, kwa mawazo kama haya.
Kwa hiyo unategemea faida kutokana na ufugaji wa kuku wa kienyeji hao 200, huku ukiwalisha pumba za mahindi, pumba za mchele laini na mtama katika hiyo miezi mingapi 6?
Nenda kawadanganye wasiojua kitu kuhusu ufugaji wa kuku.
Hizo pumba pekee utazipata wapi, na kwa bei gani unajua?
Umechanganua gharama za ufugaji huo, na mwisho wa siku ukaona unabaki na faida?
Kwanza, ni kuku gani wa kienyeji utamuuza katika miezi 6, na kwa kuwalisha lishe kama hiyo unayobainisha hapo?
Miezi sita kuku wa kienyeji hujapata yai la kutotolesha, wewe tayari unadai kuwazalisha?
Hiyo miti shamba, huko bustanini kwako inaota tuu, kienyeji, hahitaji kamwe gharama yoyote?
Tena nikwambie, usilogwe, ukadhani kuku wa kienyeji hadhuriki na magonjwa yanayowadhuru hao unaowaita "kuku wa maabara" Salmonella hachagui kuku wa maabara wala wa kienyeji, coryza inafyeka kila aina ya kuku, halafu unakuja hapa na kutalka kudanganya watu?
Kama wewe ni mfugaji wa kuku wa kienyeji, usidhani unayo nafuu yoyote kuhusu magonjwa yanayoangamiza kuku wengine wote.
Code:
Kama wewe ni mfugaji wa kuku wa kienyeji, usidhani unayo nafuu yoyote kuhusu magonjwa yanayoangamiza kuku wengine wote.
Unasema mitishamba inakawia kukua,lakini uzingatii ni mitishamba ipi!!.Hivi muarovela unahitaji muda gani hadi uanze kutumika?,mpampai unahitaji muda gani hadi uanze kutumia majani yake?,Mtunguja (ntulantu),mpilipili kichaa,majani ya maboga,nayo yanahitaji muda mrefu kukua?
Kwani kipi uanza katika ufugaji kati ya kuandaa mazingira ya kufugia na kununua kuku hata uone kuwa mitishamba itakuwa bado kukua?