Ufugaji wa kuku chotara na kienyeji kwa mijini ni hasara tupu

Asali inauzwa Kwa Lita au Kwa kilo!!??
 
Ni ukweli mtupu, tulishafuga hao Chotara na kienyeji, wanakula sana na chakula chao ni cha gharama kubwa ilihali wanachukua muda mrefu kufikia kuwauza

Ukiangalia cost ya kuwatunza na profit unayopata utagundua ni hasara tupu

Labda uwafuge kwaajili ya chakula yaani mayai na nyama ya kula Nyumbani.
 
Hapo kwenye kuku kutoka sijui Singida umedanganya na hauna ujuacho.Igunga pekee inatoa zaidi ya kuku 10000 wa kienyeji kila wiki kupitia minada ifuatayo:
J3 ni mnada wa Iborogero,J5 ni mnada wa Nsimbo,Alhamis ni mnada wa Ndala,Ijumaa ni mnada wa Kinga na Jmos ni mnada wa Igunga mjini.
Narudia tena,idadi hiyo ni kwa wiki tu.
 
Umeeleza post au umeanza ba comment kwanza then utarudi kusoma baadae? Point yangu umenielewa?

Kwenye hio minada hai kuku 10, 000 ni wa mfugaji mmoja? Rudi soma upya utaelewa
 
Umeeleza post au umeanza ba comment kwanza then utarudi kusoma baadae? Point yangu umenielewa?

Kwenye hio minada hai kuku 10, 000 ni wa mfugaji mmoja? Rudi soma upya utaelewa
Nimeeleza kulingana na ulichosema kuwa kufuga kuku wa kienyeji ni hasara na ukaonesha uchache wa upatikaniji wake.Sasa nikuambie usichokijua ni wewe kutoa mtazamo wako wa mazingira jumlishi ili hali haujafika sehemu nyingine.
Mimi nipo Igunga na ninafuga kuku wa kienyeji.Nina wastani wa kutoa kuku 100 hadi 150 kwa mwezi.Sasa nawezaje kukubali hicho ulicho kiongea juu ya kuku wa kienyeji?.
 
Mkuu 'KING KIGODA', mi naona ni kukosa kuelewana tu kati yako na mleta mada.

Ukisoma mada yake kwa makini utaelewa kuwa kaweka ushahidi kabisa wa anayoyazungumzia. Ukitaka, piga hesabu kabisa, utaona hasara inayotokana na ufugaji wa hao chotara na kuwategemea kuwa chanzo cha pato.

Wewe, kama ni mfugaji wa hao kuku, na unadai unao uwezo wa kuuza kuku 100 hadi 150 kwa wiki. Itapendeza sana nawe ukiweka ushahidi kama alivyoweka yeye, yaani, katika kuwahudumia hao kuku, hadi uwauze, hivi ni kweli kwamba unapata faida?
Hili ndilo swali linalotaka ushahidi

Kwa wafugaji wadogowadogo kifamilia, wenye uwezo wa kuuza kuku mmoja, wawili au hata watano kwa wiki, hawa hawana habari ya faida wala hasara, kwa vile, kwanza hata gharama za ufugaji hawana habari nazo, na kuku wenyewe hawahitaji kulishwa kama wanaofugwa kwa kuuza kwa faida.

Weka hesabu zako hapa, tuone unavyomudu biashara yako hiyo na kuifanya iwe endelevu.

Ukifanya hivyo sote tutaelewa na tutanyamaza, au tutakuunga mkono na kukupongeza kwa njia zako hizo.

Nikwambie ukweli mtupu: kama njia zako umeweza kufuga kuku hao na kuingiza faida, basi jipange vizuri kuwa mfugaji wa mfano/kuigwa, siyo Tanzania pekee, bali Africa kote, na pengine duniani kote.
 
Ila pia kuna angalizo katika andiko la chacha,chacha amebase ktk ufugaji wa mjini,ufugaji unaoutolea macho kama chanzo pekee cha mapato kwa mjini.
Ndugu wa igunga yeye si mfugaji wa mjini,hivyo moja kwa moja anakuwa nje ya andiko la chacha maana wengi wa wafugaji wasio mijini wana access nyingi za kuwatunza ndege hawa mfano mtu anaweza Kuwa na mradi wa kunenepesha ngombe ambao unakuwa huko pembezoni huyu Kama ni mbunifu anaweza pia akawa na ufugaji wa kuku zaidi ya wale wanaofugwa majumbani kule ingawa kwa kuweza kutoa zaidi ya kuku 100 kwa week nadhani ni mtihani kidgo na si kwamba haiwezekani.
 
Haya mambo tunayazungumzia hapa kwa maneno tu kinadharia, kumbe ni rahisi kabisa kuonyesha uhalisia wa ukweli kwa njia rahisi kabisa kwa kutumia maneno machache na hesabu rahisi kabisa kuonyesha ukweli ulipo.

Kutoa kuku 100 kila wiki, kwa hao chotara na kupata faida iwe mjini au vijijini nakataa katakata. Hesabu hazikubali.

Huyo kuku huko kijijini huwezi kumuuza akiwa chini ya wiki 13, kutokana na chakula unachomlisha. Ukitegemea ajilishe kwa kutafuta wadudu na matakataka, hata uwe na eneo kubwa kiasi gani ni lazima umwongezee mlo uliotengenezwa/changanywa, ambao gharama yake ni kubwa na kukuondolea hiyo faida unayotegemea kuipata.
Ukimlisha pumba, usitegemee awe tayari kwa soko katika muda huo.
 
Ushauri wako upi sasa ?
Tuache kufuga au tufanyeje
Au tufugeje...
Je bata,kware,njiwa,kanga wasemaje hapo hawana soko?
 
Tuache kufuga au tufanyejeUshauri wako upi sasa ?
Au tufugeje...
Je bata,kware,njiwa,kanga
hapo hawana soko?
LOooo, mkuu 'Munari', unanipa mzigo mzito sana wa kutoa ushauri jinsi ya kufuga na kupata faida na hao kuku wanaoitwa 'chotara'.

Hilo halikuwa lengo langu, mimi nilikuwa najibu hoja iliyopo hapa, kwamba kuna jamaa anauza kuku 100 kila wiki kwa faida, kwa kuwafuga kienyeji, jambo ambalo si kweli.

Ndiyo, inawezekana kabisa kufuga na kuuza kuku 100 kila wiki kwa faida, lakini siyo kwenye soko hili tulilonalo hapa nchini.
Gharama za ufugaji ni kubwa sana, hasa kwenye upande wa chakula kinachowezesha kazi hiyo ifanyike kwa faida au hasara.

Mbona watu wanafuga kuku wa mayai na nyama, mkuu 'Munari', na wanapata faida. Mimi sijasema watu waache kufuga, ila unapoingia kwenye ufugaji, hata wa hao wa mayai na nyama, ni vyema uwe umejiandaa vizuri kuifanya hiyo kazi, na ufahamu vyema uwepo wa soko.
Usikimbilie tu kufuga kwa kusikia tu watu wakisema wanafuga.
 
Tatizo lenu mnawafuga kwa gharama mno mimi huwa nawapa stater tu ule mwezi 1 halafu miezi miwili nawapa mabaki ya msosi na wanakuwa fresh na sokoni wanauzika na faida ni ya kutosha tu mbona

Sent from my CPH1823 using JamiiForums mobile app
 
Tatizo lenu mnawafuga kwa gharama mno mimi huwa nawapa stater tu ule mwezi 1 halafu miezi miwili nawapa mabaki ya msosi na wanakuwa fresh na sokoni wanauzika na faida ni ya kutosha tu mbona

Sent from my CPH1823 using JamiiForums mobile app
Dah!

WaTanzania bhwanaah, hatuna jambo tunalowekea umakini. Ni kama kila kitu ni mzaha mzaha tu!

Bandiko lako hapa limenifanya nicheke kwa jinsi ulivyorahisisha ufugaji wa hawa kuku.

Ni wazi kabisa wewe siyo mfugaji. Kuwa na vikuku viwili , tano au hata mia tano siyo ufugaji huo wa kuingiza faida. Siyo ufugaji wa kibiashara unaozungumziwa kwenye mada hii.

Nikwambie wazi kabisa, ulivyoandika hapa, wewe siyo mfugaji. Hata gharama zako za ufugaji, huzijui.

Kwa hiyo usipotoshe watu tu kudhani kwamba ufugaji ni kazi rahisi.
 
Umechelewa sana kujua hili. Fuga kuku wa mayai au nyama. Hawa broiler ni watamu sana, ila bahati mbaya watu hawawafugi hadi wakakomaa..Wengi wanauza kwa wiki 4, badala ya 8 zinazopendekezwa.

Na hii inachangiwa na kuku kuuzwa kama kuku na siyo kwa kilo. Nadhani ifike wakati sasa kuku wauzwe kwa kilo ili flwafugaji wawalishe vizuri.
 
Hakuna ufugaji mkubwa wa kuku chotara acha uchizi

Sent from my CPH1823 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…