Ufugaji wa kuku chotara na kienyeji kwa mijini ni hasara tupu

Sawa boss naamini wataelewa.
 
Kaka wengine hatuna matrilion mzee.tumeanza kidogo kidogo mpaka hapo tulipofika tunaona ni nafuu kaka.wengine hatuna profile kubwla Kama zako hivyo kidogo tukipatacho tunakutunza ili kikue zaidi kisaidie jamii tutokazo.
 
Reactions: Tsh
A
Alafu wakati wewe umeshupaza shingo na hao 78..ujue tu Sasa ni 91 idadi ya wanaotaga imeongezeka huku...
 
Bado upo Mana dawa inakuingia kaka.walio kwenye line yangu hawapo kwa ushawishi Wala maneno wapo kwa take wanayoyaona mzee..kataa miradi ya mtandaoni twende field kaka
 
Kaka wengine hatuna matrilion mzee.tumeanza kidogo kidogo mpaka hapo tulipofika tunaona ni nafuu kaka.wengine hatuna profile kubwla Kama zako hivyo kidogo tukipatacho tunakutunza ili kikue zaidi kisaidie jamii tutokazo.
Nitoe tahadhari, pamoja na kwamba nilishamalizana na mtiririko wa hoja zako.
Lililojadiliwa hapa ni "kupata faida" itokanayo na ufugaji wa kuku wa kienyeji 78; huko ndiko tuliko anzia na mjadala huu.

Hakuna mahali popote nilipokataa watu kupambana kadri wawezavyo katika kazi nyingine yoyote kwa matumaini ya siku moja kutoboa.

Kwa hiyo, tafadhari sana, tusichanganye haya mambo mawili, na kutaka kuonyesha kana kwamba ninakataa watu wapambane kadri wawezavyo.

Lakini tusiwape matumaini kwa kuwapa mifano ambayo siyo halisi, kama huo wa ufugaji wa kuku 78 na kuweza kuufanya uwe ndiyo tegemeo lako kuendeshea maisha yako.
 
Bado upo Mana dawa inakuingia kaka.walio kwenye line yangu hawapo kwa ushawishi Wala maneno wapo kwa take wanayoyaona mzee..kataa miradi ya mtandaoni twende field kaka
Hujui ninafanya nini mimi, sasa kama sio bangi hizo ni kitu gani kinachokufanya uone kwamba mimi sifanyi kazi hiyo!
Imetosha.
 
Naamini bange unazozishupalia ni wewe ndie mtumiaji Mana unajikoroga kweli..Mara useme mi dalali Mana useme ninategemea kuku 78 tu.acha bange mbichi hiyo tuna vyanzo vingine vya napata na mwanzo wa bandiko nilisema mradi huu umenisogeza kimaisha..means sikuanzia hapa
 
Hujui ninafanya nini mimi, sasa kama sio bangi hizo ni kitu gani kinachokufanya uone kwamba mimi sifanyi kazi hiyo!
Imetosha.
Mi naona unapoteza muda wako tu..hi ni shida ya graduated wasio na ajira hiii.
 
Kwani post hii haikukuonesha idadi ya mayai tagwa na jike?.
Haikukuonesha madhara ya kuwa na jogoo wengi?

Code:
Unaweka stori za kijiweni hapa, wakati mimi ninakupa sayansi ya utagaji mayai wa kuku aina yoyote ile, bila kujali wa kienyeji au wa kizungu.

Acha kuleta mambo yako ya kukaririshwa darasani mbele ya watu tuliyopo kazini kabisa.
Unazijua sifa za jogoo bora?Ukizijua ndiyo utaelewa kwa nini ni hizo.
Pili,tafuta mtetea wa kuku wa kienyeji na usimpe jogoo,wewe mpe tu chakula uone kama atataga.Na hapa ninaposema kuku wa kienyeji simaanishi hao kuku wenu wa kutoka mataifa mengine.
 
"Ukiwa na jogoo wengi unapata mayai mengi toka kwa kuku wa kienyeji"; huu upuuzi sina muda nao.
 
"Ukiwa na jogoo wengi unapata mayai mengi toka kwa kuku wa kienyeji"; huu upuuzi sina muda nao.
Kumbe naongea na dogo wa 2000 hapa.Maana nilikuonesha madhara ya kuwa na jogoo wengi kupitia sababu ya mayai kutokuwa na mbegu.Sasa upoleta habari ya ya eti majogoo wawe wengi ndiyo kuku wa kienyeji atage mayai mengi!Hiyo ni habari yako wewe,hakuna sehemu nimeongea hivyo.

Mimi nilikueleza hiki:

Kuku wa kienyeji utofautiana katika idadi ya utagaji kulingana na maumbo yao.Mitetea yenye maumbo madogo utaga kati ya mayai 15 hadi 20 na mitetea yenye maumbo makubwa utaga kati ya mayai 8 hadi 12.
 
Mkuu 'KING KIGODA', haya unayoeleza hapa hayana msingi wowote katika sayansi ya viumbe, na hasa ndege, kama kuku walivyo.

Kuku hahitaji mbegu za jogoo ndipo atage yai, awe kuku wa kienyeji, chotara hawa hawa 'hybrid' wa mayai.

Jogoo uhitaji wake ni wakati unapotaka kuzalisha vifaranga, basi, hakuna zaidi ya hapo.

Sasa haya unayoyasema kuhusu utagaji wa mayai 15 au 20, au n8 hadi 12, mbona huelezi utagaji huo ni katika muda gani?
Hata kama ingekuwa ni katika mwezi, kiwango hicho cha utagaji huoni kwamba hakuna faida ya kufuga kuku hao?
Hili ndilo linalojadiliwa hapa tokea mwanzo wa mada.
Mfugaji awe na kuku 78 wa kienyeji, na wamtagie mayai 8 kwa kila kuku kwa mwezi, bado unaona kuna faida ya ufugaji hapo?

Na bado hujataja tabia za kupenda kulalia mayai waliyonayo kuku hao, wakati wote huo utaqkuwa hupati kitu chochote, unalisha tu!
 
Kwanza hapa tukubaliane kwamba,ufugaji wa kuku wa kienyeji siyo lasmi kwa ajili ya biashara ya mayai.Pili mfumo wa ufugaji wa kuku wa kienyeji ni tofauti kabisa na ufugaji wa kuku wa maabara.Kuku wa kienyeji ukimfuga kwa taratibu za kisasa,hutapata matokeo chanya na lawama hazitaisha.
 
Endelea kufuga, unajiona mtaalamu sana
 
Ukishatambua hayo uliyoandika hapo juu, sasa rudi kwenye mada yenyewe inayojadiliwa toka mwanzo imelenga kitu gani.

Kwa hiyo, kama unataka tujadili sifa za kuku wa kienyeji, bila kujali faida inayotokana na ufugaji huo, weka hiyo mada tutaijadili kwa kina hapa.

Sielewi una maana gani na "matokeo chanya", katika ufugaji wa kuku wa kienyeji. Unamfuga kujifurahisha tu, kama 'hobby', au kuna matokeo gani chanya unayoyalenga wewe!
 
Ukizingatia asili ya kuku wa kienyeji utagundua ni ndege pori aliyeandaliwa tangu mwanzo mazingira ya kuwa huru.
Lakini kutokana na mazingira mkusanyiko wa watu katika mazingira yetu,basi kuku afugwe katika nusu huria kwa kuzingatia ukubwa wa eneo.
Tiba ya kuku wa kienyeji ni majani wanaojitafutia wenyenye,tiba za mitishamba utakazo zipanda katika eneo la kufugia na dukani utanunua chanjo za aina 2 tu,kideli na ndui basi.Chakula chao unatakiwa uwalishe mchanganyiko wa pumba za mahindi na pumba laini za mchele zilizochanganywa na mtama na kunde.Utawalisha asubuhi uwafunguliapo na jioni karibu na kuingia ndani kulala.

Mpaka hapo utaona ni kwa jinsi gani gharama itakavyokuwa kidogo ukilinganisha na huduma za hao kuku wa maabara a.k.a Chotara.

Mkuu!Hauhitaji kuwa na kuku 10000 kwa wakati mmoja kama kweli umedhamilia kufanya maisha kwa kuku hao.
Unahitaji kuwa na majike 200-300 tu wazazi na jogoo wako 20-30.
Ndani ya miezi 6-8 tu, unakuwa na uhakika wa kuwa na jumla ya kuku zaidi 600 wakubwa ambao utaweza kuuza kati ya kuku 200-300 kila mwezi.

N.B
Kwa mjini ni kweli huwezi mudu kuwafuga kuku hawa wa kienyeji kwa faida.
Mkuu,naomba niishie hapa.
 
HEeeenHeeee. Inabidi kucheka tu, kwa mawazo kama haya.

Kwa hiyo unategemea faida kutokana na ufugaji wa kuku wa kienyeji hao 200, huku ukiwalisha pumba za mahindi, pumba za mchele laini na mtama katika hiyo miezi mingapi 6?

Nenda kawadanganye wasiojua kitu kuhusu ufugaji wa kuku.

Hizo pumba pekee utazipata wapi, na kwa bei gani unajua?

Umechanganua gharama za ufugaji huo, na mwisho wa siku ukaona unabaki na faida?

Kwanza, ni kuku gani wa kienyeji utamuuza katika miezi 6, na kwa kuwalisha lishe kama hiyo unayobainisha hapo?

Miezi sita kuku wa kienyeji hujapata yai la kutotolesha, wewe tayari unadai kuwazalisha?

Hiyo miti shamba, huko bustanini kwako inaota tuu, kienyeji, hahitaji kamwe gharama yoyote?
Tena nikwambie, usilogwe, ukadhani kuku wa kienyeji hadhuriki na magonjwa yanayowadhuru hao unaowaita "kuku wa maabara" Salmonella hachagui kuku wa maabara wala wa kienyeji, coryza inafyeka kila aina ya kuku, halafu unakuja hapa na kutalka kudanganya watu?

Kama wewe ni mfugaji wa kuku wa kienyeji, usidhani unayo nafuu yoyote kuhusu magonjwa yanayoangamiza kuku wengine wote.
 
Huyu hapa ni jogoo wa miezi 9,iliyotolewa mwaka jana mwezi 3 na ndiyo kwanza kaanza kuwika.Matemba aliozaliwa nao,wengi kwa sasa wanalea vifaranga.
Mkuu!Mimi nazungumza ninacho kifanya na siyo kusikia.
Mtetea uanza kutaga kati ya miezi 6-7 na wakati huo jogoo uanza kujifunza kuwika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…