Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji na Masoko yake

Mkuu Kubota


Unavyosema soya beans unamaanisha mazao kama mbaazi na maharagwe au nakosea kaka?

Kama ndivyo inamaanisha nikiwa nalima mahindi na mbaazi sina haja ya kununua chakula cha kuku?

Na chakula hicho ni kwa ajili ya kuku wa kienyeji ama wakisasa

Na kama nikitumia chakula hicho kwa kuku wa kisasa wa mayai(layers) bila kununua chakula chochote kinachotoka viwandani, matokeo yatakuwa mazuri kweli mkuu?

Ahsantee
 
hivi nataka kufuga kuku hao wa kienyeji.
mkuu Kubota, wastan kuku mmja kuanzia kifaranga mpaka afikie kuuzwa anaweza kugharimu shingap.
kama chakula nanunua.
 
Kwa dar unapatikana wapi?
 
Bei za makundi ya vifaranga ni kiasi gani kwa kila kifaranga
 
Asante sana kwa maneno yako yanayotia moyo. Kuna wachangiaji walinilalamikia niachane na kuchoma mkaa kutokana na athari zake kwenye mazingira. Kwakuwa nilishajua utamu wa biashara ya mkaa niliamua kutengeneza mkaa kwa kutumia mabua ya mpunga na mabua ya mahindi, kama hujui ingia You Tube Kuna video kibao jinsi unavyotengenezwa.....maisha yanaendelea
 
hivi nataka kufuga kuku hao wa kienyeji.
mkuu Kubota, wastan kuku mmja kuanzia kifaranga mpaka afikie kuuzwa anaweza kugharimu shingap.
kama chakula nanunua.
Sijawahi kufanya huo utafiti maana huwa nanunua starter mash mfuko mmoja tu kuwalisha kuku mia moja kwa mwezi wa kwanza na kisha hununua growers mash mifuko miwili na huwalisha hao kuku mia kwa mwezi mwingine, baada ya hapo kuku huwa wakubwa huwaachia wakapekue na pia huwatengenezea cha ziada mwenyewe
 
Mkuu Soya beans sio maharage ni zao tofauti kabisa ingawa liko jamii moja sawa na maharage, mbaazi na kunde. Soya beans ni maarufu kwa kusheheni protein kuliko mazao mengine jamii ya mikunde. Kwenye kutengeneza vyakula vya kuku source rahisi ya protein huwa ni dagaa. Wataalamu siku hizi badala ya kutumia dagaa wanatumia Soya beans kwa kuwa ina protein nyingi sana kutengenezea chakula cha kuku.

Kasoro ya Soya beans kama ilivyo kwa protein zote zitokanazo na mimea huwa na upungufu wa Amino Acids aina mbili ambazo ni muhimu sana ...... Lysine na Methionine....hizi hazipatikani kwenye mimea....hivyo hutakiwa kununuliwa na kuchanganywa ili kukamilisha mahitaji ya amino acid zote muhimu.

Chakula kinachotengenezwa kwa kutumia Soya beans ni bora sana kwa kuwa kile kinachotengenezwa kwa kutumia dagaa au mabaki ya samaki imeshabainika kwamba mara nyingi husababisha maradhi kwa kuku kwa kuwa dagaa wanaweza kuwa na vimelea vya magonjwa. Na hii ndio sababu watengenezaji wajanja wa chakula cha kuku wanapromote kilimo cha Soya beans na in wanunuzi wakubwa wa zao hili.

Utengenezaji chakula cha kuku huhusisha vitu mbalimbali ikiwamo nafaka, dagaa au soya beans, madini mbali mbali, vitamins, pumba n.k. unapolima mahindi na Soya beans unakuwa umepunguza gharama kwa kuwa ndio yanachukua sehemu kubwa ya chakula cha kuku.

Waweza kutengeneza vyakula vya broiler, layers na kuku wakienyeji ili mradi uwe na formula ya chakula cha aina ya kuku husika na ujuzi wa mbinu za kuchanganya ingredients.
 
Kuchi unawauzaje wa umri wa wiki moja?
 
Tutajie bei ya kuchi tujue maana me mwenyewe nna shida na vifaranga wake
 
Samahani kwa usumbufu ningependa kuhafanmmuu niainagani ya kuku wa mayai ambao hutaga kwaajili ya kutotolesha vifaranga km kibo au interchick na hayo mayai hupatikanaji wake upo vp maana maana nimenunua machine ya kutotoleshea zile kubwa za m 4 Likn bado cjaanza kuitumia bado.0654249906
 
Nahitaji kujikita katika ufugaji wa kuku wa kienyeji ila ninapata shida kujua ni mbegu gani ya kuku ambayo itanisaidia kukuza kipato changu kwanza ni mbegu gani iko vizuri kwenye kutaga mayai yengi na pili ni mbegu ipi hupata nyama nyingi na kuongeza kilo?
 
kaka Kubota umeishia wapi mbona kimya kumbuka watu wengi tulikuwa tanafuatilia saaana maada hii sababu ni muhimu saana na ingetusaidia wengi sana pls endelea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…