Jabman
JF-Expert Member
- Jul 27, 2016
- 1,005
- 1,337
Wapi huko?Mkuu uku kwetu kuku 1 anauzwa 15000 na jogoo 20000 ad 25000
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wapi huko?Mkuu uku kwetu kuku 1 anauzwa 15000 na jogoo 20000 ad 25000
0766728326. Naomba uniunge mkuu.Tupia namba yako au we unaweza ukaanzisha mkuu tupo wengi Sana mkuu
0766728326Pamoja mkuu watu tunapeana ujuzi lukuki huku
Duh asantee Kwa elimu nzuri mkuuLEO TUANGALIE MCHANGANUO WA TSHS
300,000/= (LAKI TATU) KWA KUANZISHA MTADI
WA UFUGAJI KUKU WA KIENYEJI.
Hapa tuta hitaji kuku 11 tu wakubwa wanao taga
yani majike 10 na Jogoo 1 tu. Kwa kutumia kuku
hao 11 baada ya miezi mitatu unaweza ukawa
na kuku mia Tatu 300 au na zaidi kama unataka.
Nunua kuku wako katika chanzo cha kuaminika
kuepuka magonjwa usinunue kuku sehemu za
masokoni au kwenye mabanda ya njiani au kuku
wanao safirishwa kutoka mkoa mmoja kwenda
mwingine.
Unapo nunua kuku wakubwa kwanza unapo
wafikisha wape chanjo ya mdondo (Newcastle
vaccine) ili kuweka rekodi yako ya chanjo maana
chanjo hii hurudiwa kila baada ya miezi 3.
Ukumbuke tarehe uliyo wachanja na tarehe
utakayo wachanja tena baadae.
Usinunue kuku kabla hujaandaa banda na
Chakula.
Katika sh. 300000 toa sh.69500 ambayo
utanunua Chakula cha kuku, kuku hawa hawana
formula ya Chakula hivyo unaweza kununua
material ukachanganya Chakula mwenyewe
ampapo utaokoa pesa nyingi pia.
Mchanganuo Wa 69500 ni:-
Pumba gunia 1. Shs.20000 gunia la pumba lina
kilo 70.
- paraza kilo 25 = 700x25 =17500. Paraza ni
mahindi yaliyo vunjwa vunjwa kwaajili ya
Chakula cha kuku.
-mashudu ya alizeti kilo 15. 700x15=10500
- layer's consetraite
Kilo 25 kifuko. = 21500.
Ukijumlisha utakuwa umepata kilo 135 kwa shs
69500. Ambapo kila kilo moja ya Chakula
utakuwa umenunua kwa shiling 514.8.
Chakula hicho kichanganye kwa kutumia chepe
kichanganye vizuri kichanganyike pumba lazima
iwe kavu kabisa ikaushe usiwape kuku pumba
mbichi.
Kumbuka kuku anayetaga anakula Gram 130 kwa
siku
Hivyo kuku 10 watakula kilo 1.3 kwa siku
ambayo ni gram 1300.
Hivyo tutaweza kuona Chakula chetu kitatupeleka
zaidi ya siku 100 ya zaidi ya miezi mitatu.
TOA SHS 170000 AMBAYO UTANUNULIA KUKU.
Mchanganuo wake
Kwa kila kuku mzuri ambaye ajazeeka anayetaga
utampata kwa shilingi 15000 na Jogoo nzuri
utampata kwa shilingi 20000.
Jogoo 1 = 20000
Majike 10 x15000= 150000 jumla 170000.
Itakuwa imebaki shs. 60500
-Hii pesa iliyobaki ni kwa ajili ya kununu material
ya bei nafuu na kutengeneza banda la kuku 10
hadi 20. Kuku hawa hawaitaji banda Kubwa
kwasababu hawashindi ndani wataingia ndani
wakati Wa kulala jiaoni na mchana wakati
wakutaga
Kuku wachiwe eneo la kutosha na lenye mchanga
watakao itumia kuoga kuondoa wadudu km
papasi na utitiri sehemu wanayopenda kuoga
nyunyizia Dawa ya utitiri.
Banda tengeneza la kuhamisha la futi 4x8x4 yani
urefu kwenda juu futi 4 upana futi 8 kipenyo futi
4. Tumia materio yaliyo karibu nawe kama
mirunda, mabanzi, Mabati reject au yaliyochakaa
chicken wire au wire mesh, fito mbao 2x2 au 4x2
n.k. Kama ni sehemu za mjini litakugharimu
kama Tsh 50,000-60,000.Vijijini au nje ya mji
ambapo miti ni mingi litakugharimu Tsh 25,000
hadi 35,000.
Haya jinsi ya kuwaendeleza hao kuku ili kupata
kuku wengi hadi utakao wataka. Hapa itabidi
ukubali kupeleka Mayai sehemu ambapo
wanatotolesha ambapo trey 1 ni shilingi 10000.
Hapa kuku hawa 10 watakupa wastani Wa Mayai
8 kwa siku ambapo kwa mwezi ni Mayai 240.
Kila baada ya siku 7 peleka Mayai kwenye
Mashine yakutotolea (incubator). Hivyo kwa
mwezi utapeleka Mayai 240 utapata wastani Wa
Vifaranga 200. Hivyo baada ya mwezi nakushauri
usitotoleshe tena hao Vifaranga 200 ni wengi
sana kwa kuanzia kwa kuwa tayari tunenunua
Chakula cha kuku cha kutupeleka miezi mitatu
basi Mayai utakayo endelea kuokota utayauza
kwaajili ya kupata hela ya Chakula cha Vifaranga
watakao toka hao zaidi ya 200. Hivyo mradi huu
utakuwa unajiendesha wenyewe. Nikiwa na
maana kama kuku 10 watakupa wastani Wa
Mayai 8 kwa siku na Mayai 240 kwa mwezi ni
wazi kwamba kuku hao wanakuingizia 120000
kwa mwezi ambaya sasa hela Hii itatumika
kununua Chakula cha kulea hao Vifaranga
ambapo Mayai ya mwezi tu yataweza kununua
Chakula ambacho Vifaranga 200 watakula mwezi
pamoja na chanjo na Dawa zote.
Hivyo baada ya miezi mitatu utakuwa na
Vifaranga wakubwa Wa miezi miwili na Chakula
cha kuku wakubwa ndo kitakuwa kinaishia hapa
utachanganya Chakula cha aina moja tu wale
Vifaranga watakuwa wameshakuwa kiasi cha
kula Chakula chochote.
mkuu kuna siku kuku wa kienyeji huwa hawatagi, halafu pia Nina majike ambayo yameanza kutamia mayai so yanakua hayatagi tena, nimeyanyang'anya mayai Ila yanalalia kichanja kikiwa empty, vp hapo nafanyaje ili waendelee kutaga?Walipotaga waliatamia 2 tu na wakawalea wao, mwingine akabaki na jogoo sikuwa hata na banda kubwa, wakakua 30 mara 3, nikawa na kuku 90 ndo nikajenga banda, ilichukua muda mrefu lakini, niliuza majogoo nikabakisha 5 jike 50, ndo nikaanza kufuga kibiashara, Sasa hivi natotolesha mara 1 kwa miezi 2, muda mwingi nauza mayai, kwa kweli nilianza kikawaida sana bila gharama kubwa, huu mwaka wa 5 sasa
Wape lishe inayostahili mkuu, watataga baada ya muda mfupi ila majogoo yawepomkuu kuna siku kuku wa kienyeji huwa hawatagi, halafu pia Nina majike ambayo yameanza kutamia mayai so yanakua hayatagi tena, nimeyanyang'anya mayai Ila yanalalia kichanja kikiwa empty, vp hapo nafanyaje ili waendelee kutaga?
Wape lishe ya kutosha...wape nafasi ktk banda mwisho wakate midomokuku wangu wanakula mayai sana msaada tafadhali
Tafta dawa ya mafua then wape otcDawa gani ndugu yangu unatumia kama kuku akiwa anajikunyata na kama ana mafua fulani....yaani anakoroma naomba msaada...
Dawa ya mafuaWakuu kuku wangu wanajikunyata na wanatoa sauti kama wamekwama na kitu je tatizo nini naomba msaada wenu kabla sijawakosa wote....nimenunua sehemu tofauti na since wakutane sikuwapa kitu chochote ndio makosa nimefanya
LEO TUANGALIE MCHANGANUO WA TSHS
300,000/= (LAKI TATU) KWA KUANZISHA MTADI
WA UFUGAJI KUKU WA KIENYEJI.
Hapa tuta hitaji kuku 11 tu wakubwa wanao taga
yani majike 10 na Jogoo 1 tu. Kwa kutumia kuku
hao 11 baada ya miezi mitatu unaweza ukawa
na kuku mia Tatu 300 au na zaidi kama unataka.
Nunua kuku wako katika chanzo cha kuaminika
kuepuka magonjwa usinunue kuku sehemu za
masokoni au kwenye mabanda ya njiani au kuku
wanao safirishwa kutoka mkoa mmoja kwenda
mwingine.
Unapo nunua kuku wakubwa kwanza unapo
wafikisha wape chanjo ya mdondo (Newcastle
vaccine) ili kuweka rekodi yako ya chanjo maana
chanjo hii hurudiwa kila baada ya miezi 3.
Ukumbuke tarehe uliyo wachanja na tarehe
utakayo wachanja tena baadae.
Usinunue kuku kabla hujaandaa banda na
Chakula.
Katika sh. 300000 toa sh.69500 ambayo
utanunua Chakula cha kuku, kuku hawa hawana
formula ya Chakula hivyo unaweza kununua
material ukachanganya Chakula mwenyewe
ampapo utaokoa pesa nyingi pia.
Mchanganuo Wa 69500 ni:-
Pumba gunia 1. Shs.20000 gunia la pumba lina
kilo 70.
- paraza kilo 25 = 700x25 =17500. Paraza ni
mahindi yaliyo vunjwa vunjwa kwaajili ya
Chakula cha kuku.
-mashudu ya alizeti kilo 15. 700x15=10500
- layer's consetraite
Kilo 25 kifuko. = 21500.
Ukijumlisha utakuwa umepata kilo 135 kwa shs
69500. Ambapo kila kilo moja ya Chakula
utakuwa umenunua kwa shiling 514.8.
Chakula hicho kichanganye kwa kutumia chepe
kichanganye vizuri kichanganyike pumba lazima
iwe kavu kabisa ikaushe usiwape kuku pumba
mbichi.
Kumbuka kuku anayetaga anakula Gram 130 kwa
siku
Hivyo kuku 10 watakula kilo 1.3 kwa siku
ambayo ni gram 1300.
Hivyo tutaweza kuona Chakula chetu kitatupeleka
zaidi ya siku 100 ya zaidi ya miezi mitatu.
TOA SHS 170000 AMBAYO UTANUNULIA KUKU.
Mchanganuo wake
Kwa kila kuku mzuri ambaye ajazeeka anayetaga
utampata kwa shilingi 15000 na Jogoo nzuri
utampata kwa shilingi 20000.
Jogoo 1 = 20000
Majike 10 x15000= 150000 jumla 170000.
Itakuwa imebaki shs. 60500
-Hii pesa iliyobaki ni kwa ajili ya kununu material
ya bei nafuu na kutengeneza banda la kuku 10
hadi 20. Kuku hawa hawaitaji banda Kubwa
kwasababu hawashindi ndani wataingia ndani
wakati Wa kulala jiaoni na mchana wakati
wakutaga
Kuku wachiwe eneo la kutosha na lenye mchanga
watakao itumia kuoga kuondoa wadudu km
papasi na utitiri sehemu wanayopenda kuoga
nyunyizia Dawa ya utitiri.
Banda tengeneza la kuhamisha la futi 4x8x4 yani
urefu kwenda juu futi 4 upana futi 8 kipenyo futi
4. Tumia materio yaliyo karibu nawe kama
mirunda, mabanzi, Mabati reject au yaliyochakaa
chicken wire au wire mesh, fito mbao 2x2 au 4x2
n.k. Kama ni sehemu za mjini litakugharimu
kama Tsh 50,000-60,000.Vijijini au nje ya mji
ambapo miti ni mingi litakugharimu Tsh 25,000
hadi 35,000.
Haya jinsi ya kuwaendeleza hao kuku ili kupata
kuku wengi hadi utakao wataka. Hapa itabidi
ukubali kupeleka Mayai sehemu ambapo
wanatotolesha ambapo trey 1 ni shilingi 10000.
Hapa kuku hawa 10 watakupa wastani Wa Mayai
8 kwa siku ambapo kwa mwezi ni Mayai 240.
Kila baada ya siku 7 peleka Mayai kwenye
Mashine yakutotolea (incubator). Hivyo kwa
mwezi utapeleka Mayai 240 utapata wastani Wa
Vifaranga 200. Hivyo baada ya mwezi nakushauri
usitotoleshe tena hao Vifaranga 200 ni wengi
sana kwa kuanzia kwa kuwa tayari tunenunua
Chakula cha kuku cha kutupeleka miezi mitatu
basi Mayai utakayo endelea kuokota utayauza
kwaajili ya kupata hela ya Chakula cha Vifaranga
watakao toka hao zaidi ya 200. Hivyo mradi huu
utakuwa unajiendesha wenyewe. Nikiwa na
maana kama kuku 10 watakupa wastani Wa
Mayai 8 kwa siku na Mayai 240 kwa mwezi ni
wazi kwamba kuku hao wanakuingizia 120000
kwa mwezi ambaya sasa hela Hii itatumika
kununua Chakula cha kulea hao Vifaranga
ambapo Mayai ya mwezi tu yataweza kununua
Chakula ambacho Vifaranga 200 watakula mwezi
pamoja na chanjo na Dawa zote.
Hivyo baada ya miezi mitatu utakuwa na
Vifaranga wakubwa Wa miezi miwili na Chakula
cha kuku wakubwa ndo kitakuwa kinaishia hapa
utachanganya Chakula cha aina moja tu wale
Vifaranga watakuwa wameshakuwa kiasi cha
kula Chakula chochote.
Dawa gani ndugu yangu unatumia kama kuku akiwa anajikunyata na kama ana mafua fulani....yaani anakoroma naomba msaada...
Mkuu tupia namba uungwe Kwa group wasap