Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji na Masoko yake

Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji na Masoko yake

Wiki 2 zinatosha, unaweka mfumo wa joto, mama ni kwa ajili ya joto tu kama huwezi kuwatunza, jifunze kuwatenganisha wanapototolewa tu
Nashukuru Agynasa umezungumzia juu ya mfumo wa joto.. Labda nipende kujua namna ya kuweka huo utaratibu..
 
naomba mwenye grup la wasap la ufugaj wa kuku ani-PM....nimeanza ufugaji wa kuku wa kienyej...banda langu lina ukubwa wa 5m x 15m na vifaranga ni croiler 150
 
Sawa.. Vipi Kuna madhara gani ya kuwaacha waatamie wote? Au pia Kuna faida gani za kuwaatamisha wachache?
Hakuna madhara ila chagua kuku wakubwa waatamie mayai 20-25 kuku 1, hivyo kwa kuwa kuku wanataga mayai machache, basi yachanganye wakati huo wengine wakiendelea kutaga mayai unakula au unauza, usiatamishe kiholela, wakitotolewa kaa mwezi 1-2 ndo unaatamisha tena, fuga kisasa
 
Mkuu vipi Kwa usalama wa watoto si watakua bado hawajaawa na nguvu ya kujitegemea?
Kifaranga ndani ya siku 2 paka 3 toka aanguliwe kina uwezo wa kujitegemea atakachomisi kwa mama yake ni joto tu, cha kufanya nikuwaandalia maisha ya joto tu.
 
Hakuna madhara ila chagua kuku wakubwa waatamie mayai 20-25 kuku 1, hivyo kwa kuwa kuku wanataga mayai machache, basi yachanganye wakati huo wengine wakiendelea kutaga mayai unakula au unauza, usiatamishe kiholela, wakitotolewa kaa mwezi 1-2 ndo unaatamisha tena, fuga kisasa
Nimekuelewa mkuu. Vipi Kwa upande wa chakula unawapa aina gani ya chakula
 
Kifaranga ndani ya siku 2 paka 3 toka aanguliwe kina uwezo wa kujitegemea atakachomisi kwa mama yake ni joto tu, cha kufanya nikuwaandalia maisha ya joto tu.
Mkuu Sawa lakini hayo maisha ya joto unayaandaa vipi
 
Ulitumia njia gan mkuu
Walipotaga waliatamia 2 tu na wakawalea wao, mwingine akabaki na jogoo sikuwa hata na banda kubwa, wakakua 30 mara 3, nikawa na kuku 90 ndo nikajenga banda, ilichukua muda mrefu lakini, niliuza majogoo nikabakisha 5 jike 50, ndo nikaanza kufuga kibiashara, Sasa hivi natotolesha mara 1 kwa miezi 2, muda mwingi nauza mayai, kwa kweli nilianza kikawaida sana bila gharama kubwa, huu mwaka wa 5 sasa
 
Mkuu Sawa lakini hayo maisha ya joto unayaandaa vipi
Kuna ile njia ya kiasilia unaweka moto wenye majivu kwenye chungu nadhani chungu kikipata moto hutoa joto basi vitoto vitasogelea pale kupata joto. Nyingine ni ya kawaida unawafungua taa kwenye banda lao ile taa iwe karibu nao.
 
Hakuna pesa ya chapchap, lazima usote kwanza,hadi kuku afikie kuuzwa hiyo bei ni miezi kadhaa, nafuga pia
na akitaka faida nzuri auze mayai ya kienyeji kuliko kuuza kuku mzima. inabidi ajifunze kila siku atumie mbinu bora na zenye tija kwenye uzalishaji.
 
Nnao pure kienyeji kabisa hapa mbezi ya kimara wa miezi 4 na 5 wako 10 tu wana chanjo zote wote nauza 120000 bei haipungui kwako mfugaji nicheki 0787429104
 
Mimi napatikana mtwara ila soko zuri lipo dar na zanzibar kwenye zile hotel kubwa kubwa ukiwa na shida ya soko nitakupa maelekezo mkuu ukapige pesa.
mkuu naomba unipe michapo ya soko la znz mimi nipo znz lakini naona kiza nipe michapo nifaidike
 
Back
Top Bottom