Poultry Sayuni
Senior Member
- Sep 6, 2011
- 125
- 36
Ahsante Reti , Nami nimeanza kupatwa wasiwasi wa chakula ninatumia zaidi concentrate nachanganya na pumba za kawaida. Je ni sahihi?
Ok, Layers concentrate ni sawa, inashauriwa 25kg C.L/40-50kg za pumba, unaweza ongeza na DCP kidogo. say vijiko 10 vya chakula kwa kg 70 za chakula.
Ahsante Mkuu RETI, DCP nini nini?
Kaka mkuu Kubota, naomba unipatie websites tofauti tofauti za uchinani na sehemu nyingine ulizo na ujuzi nazo juu ya bei za Incubators. Pamoja.
Kaka mkuu, hali yako kwanza? Mi swali langu lita diverge kidogo, ni kuwa ningependa kujua njia tofauti tofauti juu ya kuliface tatizo kubwa la kuku wa kienyeji, la ugonjwa ambao husababisha vifo vyao kwa wingi, je kuna njia gani mbadala huwa zinatumika? Asante.
Ni kweli kuku wa kienyeji ni dili sana lkn ingekuwa vyema ungenieleza the whole process from begin mpk kukuwa kwake kitaalamu kwani huwa wanakufaga sana kwa ugonjwa wa "Mdondo" huu ugonjwa ni adui mkubwa sana kwa maendeleo kwa kuku wa kiswahili!
usipate shida ........... dawa ya MDONDO kwa kuku wa kiswahili ni UGORO ...........unawachanganyia kwenye maji
na yule anayeumwa .... unamshika na kumnywesha. Atapona.
Pia anayeumwa mpe dozi ya pilipili .......nzima asubuhi .........nzima mchana .......... na nzima jioni. I tell you within a day or two kuku wako atakuwa mzima.
Mimi nime - experience hivi vyote na niliwapa kuku wangu WAKAPONA!!!
Shukrani Kubota kwa kuanzisha huu uzi, na wachangiaji wengine mliochangia mbarikiwe!!!!!
Mie na swali kidogo,
nina kuku alitaga nje ya banda lao, alivyoanza kutamia nilimuhamisha usiku kumpeleka ndani ya banda(mahala nilipotengeneza kwa ajili ya kutania (kulalia), HAKULALIA yale mayai, kesho yake nikamrudisha pale alipokuwa ametaga/ametamia, aliendelea kutamia.
tatizo linakuja hiki ni kipindi cha mvua nilijaribu kumuwekea bati ili mvua ikinyesha asiloane, ila na wasiwasi endapo mayai yakipata maji yataharibika???
swali la pili, najitahidi kufuga ila kuku wanapoanguliwa ni kwa nini wiki ya pili tu wanakuwa wanapata viuvimbe machoni, na kwenye pua zao?? nilijaribu kuuliza nikaambiwa ni ndui, so napenda kujua kuna kinga ya ndui?? na kama ipo natakiwa niwape kuku wakiwa na umri gani??
ndui dawa yake ni mafuta ya alizet
mafuta ya alizet nayafanyia nini?? nawapaka kwenye vile viuvimbe?, naweka kwenye maji/chakula au?? naomba ufafanuzi tafadhali!
Shukrani Kubota kwa kuanzisha huu uzi, na wachangiaji wengine mliochangia mbarikiwe!!!!!
Mie na swali kidogo,
nina kuku alitaga nje ya banda lao, alivyoanza kutamia nilimuhamisha usiku kumpeleka ndani ya banda(mahala nilipotengeneza kwa ajili ya kutania (kulalia), HAKULALIA yale mayai, kesho yake nikamrudisha pale alipokuwa ametaga/ametamia, aliendelea kutamia.
tatizo linakuja hiki ni kipindi cha mvua nilijaribu kumuwekea bati ili mvua ikinyesha asiloane, ila na wasiwasi endapo mayai yakipata maji yataharibika???
swali la pili, najitahidi kufuga ila kuku wanapoanguliwa ni kwa nini wiki ya pili tu wanakuwa wanapata viuvimbe machoni, na kwenye pua zao?? nilijaribu kuuliza nikaambiwa ni ndui, so napenda kujua kuna kinga ya ndui?? na kama ipo natakiwa niwape kuku wakiwa na umri gani??
Mkuu Ankojei kesha kudokeza ipasavyo juu ya tatizo la ndui. Chanjo ya ndui kiutaalamu ipo ila sijawahi kuona ikiuzwa Tanzania! Kinachofanyika ni kutibu dalili zinapojitokeza. Suala la ndui nimeliongelea tayari huko kwenye post zilizopita kuhusu magonjwa fuatilia upate simulizi kwa mapana na marefu yake.
Kuku anaeatamia kama maji ya mvua yakiyafikia mayai yanaweza yasitotolewe kwa vile huwa ni rahisi kushambuliwa na vimelea vya magonjwa. Jitahidi umwekee bati! Kuku wengi hukubali kuhamishwa usiku, lakini kuna wachache huwa wanakataa, ni budi uwatambue kuku wanaokubali kuhamishwa kirahisi na endeleza kizazi chao, kuku wakorofi uza!
Asante mkuu RETI kwa elimu hii. Ila ni vizuri ukatupa hata jina la hiyo dawa, ili iwe rahisi kuitafuta humo madukani. Funguka RETI!Asante.
Inapatikana kwenye maduka ya dawa za mifugo, waambie tu "CHANJO YA NDUI". bei ni kati ya 10,000-12,00.
asante