Shukrani Kubota kwa kuanzisha huu uzi, na wachangiaji wengine mliochangia mbarikiwe!!!!!
Mie na swali kidogo,
nina kuku alitaga nje ya banda lao, alivyoanza kutamia nilimuhamisha usiku kumpeleka ndani ya banda(mahala nilipotengeneza kwa ajili ya kutania (kulalia), HAKULALIA yale mayai, kesho yake nikamrudisha pale alipokuwa ametaga/ametamia, aliendelea kutamia.
tatizo linakuja hiki ni kipindi cha mvua nilijaribu kumuwekea bati ili mvua ikinyesha asiloane, ila na wasiwasi endapo mayai yakipata maji yataharibika???
swali la pili, najitahidi kufuga ila kuku wanapoanguliwa ni kwa nini wiki ya pili tu wanakuwa wanapata viuvimbe machoni, na kwenye pua zao?? nilijaribu kuuliza nikaambiwa ni ndui, so napenda kujua kuna kinga ya ndui?? na kama ipo natakiwa niwape kuku wakiwa na umri gani??