Hivi mkuu wale wadudu wanaokula mayai mfano .vicheche au kenge dawa yao ni nini maana wamenitia hasara sana mayai km ishirini waliyala yote karibu wiki waweze kuangua iliniuma sana
MI nimeanza na kuku 11 jike 10 dume moja mwezi sasa umeisha,
wamekufa wawili kwa ugojwa na mmoja kaliwa na mbwa.
wamebaki 8 mmoja tu ndio anataga.
Pata super gro kwa ajili ya kurutubisha kuku na kuondoa maradhi,soma Uzi wa Wafugaji na wakulima wote soma hii kupata data kamili za matumizi ya super gro View attachment 149518
Hivi mkuu wale wadudu wanaokula mayai mfano .vicheche au kenge dawa yao ni nini maana wamenitia hasara sana mayai km ishirini waliyala yote karibu wiki waweze kuangua iliniuma sana
Hakuna kitu kipya hapa JF, nenda kwenye links hapa chini utapata unalolihitaji bila shaka!!!!
1. https://www.jamiiforums.com/ujasiri...wongozo-kwa-wafugaji-wa-kuku-wa-kienyeji.html
2. https://www.jamiiforums.com/ujasiri...ugaji-wa-kuku-wa-kienyeji-na-masoko-yake.html
3. https://www.jamiiforums.com/ujasiriamali/117756-kwa-wafugaji-wa-kuku-wa-kisasa.html
4. https://www.jamiiforums.com/ujasiri...i-na-bata-mzinga-pia-kuku-aina-ya-kenbro.html
5. https://www.jamiiforums.com/ujasiriamali/649794-mbinu-za-kuangua-vifaranga-kwa-njia-ya-kienyeji.html
6. https://www.jamiiforums.com/ujasiriamali/400316-zijue-mbinu-zangu-ufugaji-kuku-wa-kienyeji.html
Asante kwa kutudondoshea vyanzo mbalimbali vya kuelimisha kuhusu ufugaji wa kuku, kwangu mimi natanguliza shukrani ukinidokezea bei za vifaranga ili kuanda vema business plan kabla ya kuanza mradi wa majaribio.
Katika swala zima la ufugaji wa kuku inategemeana na eneo ulilopo na nini malengo yako kwa baadae.
- Kuna Aina kama 3 hivi za kuku
1. Wa kizungu au kisasa
2. Pure kienyeji
3. Chotara au hybreed
Mara nyingi hawa hawafanani na watu wanawafuga kulingana na maeneo waliopo na upatikanaji wa soko, Kuna meneo ukifuga kuku wa kisasa pure hutapata soko kwa sababu walaji wengi wanatumia kuku wa kienyeji au chotara na kuna maeneo wao hawataki kusikia kuku wa kienyeji wao wanataka kuku wa kisasa tu hasa kwenye mahoteli makubwa ya kitalii.
Hivyo ni lazima ujiulize unataka kufuga aina ipi na kwa sababu gani? na wateja wako unao taka kuwatageti ni wapi hasa?
Natanguliza shukrani kwa majibu yako yenye kuelimisha na kunipanua akili, labda kwa uzoefu wako bei za vifaranga kwa wastani ni kiasi gani? Sidhani kama bei zinatofautiana sana ingawa hasa kwa
- Kuku wa nyama wa kisasa
- Kuku wa mayai wa kisasa
- Kuku chotara wa mayai na nyama
Mara nyingi bei kwa vifaranga wa Nyama huwa kati ya 1500 hadi 1900 kwa vifaranga wa mayai huwa ni 2000 hadi 2300 kutegemeana na kampuni kwa Chotara huwa ni 2000 hadi 2500 na hapa ni kwa DAY ONE OLD CHICK

View attachment 155748 View attachment 155749 View attachment 155750
Kwa mtazamo wangu kwa waanzaji wanaotaka kupata
uzoefu kufanya majaribio kwa kuanza na kuku wachache
kutosha ili kujua mbinu na mambo muhimu ya kuwa makini
ni bora kuliko kuanza mradi mkubwa bila uzoefu na mambo
yakishindikana ni kuingia hasara kubwa ya pata
maumivu ya siyotarajiwa kichwani.
Asante kwa taarifa, pengine ningeweza kufikiria kwa waanzaji wengi vema wakashika mpango mzima wa kuanza na kiwango cha kima cha chini kwa kununua kuku wachache tetea kadhaa na majogoo kama wawili au watatu na mpango mzima wa kuangulisha vifaranga kwa kuku mchanganyiko au wa kienyeji. Kwa kuku wa kisasa ambao huhitaji mtangao wa kuangulisha hakuna jinsi ni bora tu kuyavulia maji nguo yaogwe.
Kwa bei hiyo dhahiri ufugaji kuku kibiashara bora kuanzia kiwango cha chini na 500 vinginevyo hakutakuwa na faida ya kutosha chini ya hapo.
Hata hivyo kama nilivyosema hapo juu bora kuanza na kuku wachache kama mabanda yalivyo hapo juu kupata uzoefu namna ya kuwatunza na kuwatibu hali kadhalika kujenga mazoea ya kuandaa mchanganyiko wa chakula wewe mwenyewe. Uzoefuu huo utasaidia kujua mbinu muhimu unapoamua kupanua mradi huo.
Kuna ndugu yangu mmoja alianza hivyo na banda nyumbani kwake kwa kuku 50, alipofanikiwa akawa na 100, kisha akafikisha mia tatu. Ameshapata uzoefu sasa anahamishia mradi shambani kwake ambako analo eneo kubwa na hewa safi kwa kuku.
Mpango mzima wa mradi mkubwa kwa mara ya kwanza unahitaji kujipanga sana na pia kuwa na capital ya kutosha si mradi kuwa na kuku, na pengine kuwa karibu na wataalamu ambao watasaidia kwa ushauri na mengineyo na hao wataalamu si bure ni biashara kwa kwenda mbeleee..
Asante kwa taarifa, pengine ningeweza kufikiria kwa waanzaji wengi vema wakashika mpango mzima wa kuanza na kiwango cha kima cha chini kwa kununua kuku wachache tetea kadhaa na majogoo kama wawili au watatu na mpango mzima wa kuangulisha vifaranga kwa kuku mchanganyiko au wa kienyeji. Kwa kuku wa kisasa ambao huhitaji mtangao wa kuangulisha hakuna jinsi ni bora tu kuyavulia maji nguo yaogwe.
Kwa bei hiyo dhahiri ufugaji kuku kibiashara bora kuanzia kiwango cha chini na 500 vinginevyo hakutakuwa na faida ya kutosha chini ya hapo.
Ila mimi nashauri mtu aanze na vifaranga hapo ndo unapata elimu vizuri na unaweza kuwa contro mwenyewe,