Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji na Masoko yake

Pole ila imarisha banda lako. Sasa mayai tu wanaingia na kula vifaranga vitakuwa salama? Tafuta hata bati used na chicken wire jenga simple na ufunge mlango saa zote. Ukiwa porini vicheche, ukiwa mjini paka na mbwa wa majirani. Jitaidi ukivuka hii changamoto utafanikiwa
Hivi mkuu wale wadudu wanaokula mayai mfano .vicheche au kenge dawa yao ni nini maana wamenitia hasara sana mayai km ishirini waliyala yote karibu wiki waweze kuangua iliniuma sana
 
Mkuu Marire pole ila usikate tamaa, kuna wenzio wananunua wanakufa banda zima hata alfu, songa mbele. Kuhusu kutaga umri wamefikia? Ulikowatoa kama walifikia muda wa kulalia watasimama kidogo. Vipi chakula chao? Pia kama wote waliumwa hasa mafua hukata kutaga kwa muda hivyo imarisha afya zao kwa lishe kwanza.
MI nimeanza na kuku 11 jike 10 dume moja mwezi sasa umeisha,
wamekufa wawili kwa ugojwa na mmoja kaliwa na mbwa.
wamebaki 8 mmoja tu ndio anataga.
 
Kwenye mimea unamtumia je sasa

Sent from my iPhone using JamiiForums mobile app
 
Hivi mkuu wale wadudu wanaokula mayai mfano .vicheche au kenge dawa yao ni nini maana wamenitia hasara sana mayai km ishirini waliyala yote karibu wiki waweze kuangua iliniuma sana

mi kenge ndo tatizo kubwa, nimejaribu kuwatega kwa mayai yaliyochemshwa lakini wapi, wanadonoa tu hawamezi lote, utadhani wametumwa! natamani nijue sumu yao niwaue wote
 
Habari wapendwa,

Niko katika mchakato wa ufugaji wa kuku.Bado nafanya utafiti upi ni ufugaji wenye tija zaidi kati ya kuku wa kienyeji,wa mayai na wa nyama wa kizungu.Kwa ambao tayari wako katika ufugaji naomba wanisaidie yafuatayo;

  • Kunipa mchakato mzima wa mtaji na faida kati ya aina ambayo unafuga.
  • Kama kuna sehem naweza kupata mkopo rahis kwa kutumia majengo niliyojenga kwa ajili ya mradi japo yapo katika eneo ambalo halijapimwa na serikali

NATANGULIZA SHUKRANI....Umoja ni nguvu
 
mkuu,kabla ya kuanzisha huu uzi ungesoma kwanzwa sticky nyuzi kibao hapo juu alafu ndio ungekuja huku.
~~~~~~~~~~~~~~~~
matapeli pia hawakosi uwe makini
 
Asante kwa kutudondoshea vyanzo mbalimbali vya kuelimisha kuhusu ufugaji wa kuku, kwangu mimi natanguliza shukrani ukinidokezea bei za vifaranga ili kuanda vema business plan kabla ya kuanza mradi wa majaribio.

Katika swala zima la ufugaji wa kuku inategemeana na eneo ulilopo na nini malengo yako kwa baadae.

- Kuna Aina kama 3 hivi za kuku

1. Wa kizungu au kisasa

2. Pure kienyeji

3. Chotara au hybreed

Mara nyingi hawa hawafanani na watu wanawafuga kulingana na maeneo waliopo na upatikanaji wa soko, Kuna meneo ukifuga kuku wa kisasa pure hutapata soko kwa sababu walaji wengi wanatumia kuku wa kienyeji au chotara na kuna maeneo wao hawataki kusikia kuku wa kienyeji wao wanataka kuku wa kisasa tu hasa kwenye mahoteli makubwa ya kitalii.

Hivyo ni lazima ujiulize unataka kufuga aina ipi na kwa sababu gani? na wateja wako unao taka kuwatageti ni wapi hasa?
 
Natanguliza shukrani kwa majibu yako yenye kuelimisha na kunipanua akili, labda kwa uzoefu wako bei za vifaranga kwa wastani ni kiasi gani? Sidhani kama bei zinatofautiana sana ingawa hasa kwa
  1. Kuku wa nyama wa kisasa
  2. Kuku wa mayai wa kisasa
  3. Kuku chotara wa mayai na nyama
 
Mara nyingi bei kwa vifaranga wa Nyama huwa kati ya 1500 hadi 1900 kwa vifaranga wa mayai huwa ni 2000 hadi 2300 kutegemeana na kampuni kwa Chotara huwa ni 2000 hadi 2500 na hapa ni kwa DAY ONE OLD CHICK
 
Asante kwa taarifa, pengine ningeweza kufikiria kwa waanzaji wengi vema wakashika mpango mzima wa kuanza na kiwango cha kima cha chini kwa kununua kuku wachache tetea kadhaa na majogoo kama wawili au watatu na mpango mzima wa kuangulisha vifaranga kwa kuku mchanganyiko au wa kienyeji. Kwa kuku wa kisasa ambao huhitaji mtangao wa kuangulisha hakuna jinsi ni bora tu kuyavulia maji nguo yaogwe.

Kwa bei hiyo dhahiri ufugaji kuku kibiashara bora kuanzia kiwango cha chini na 500 vinginevyo hakutakuwa na faida ya kutosha chini ya hapo.
 
Chicken_Coop20.jpg Chicken_Coop19.jpg CHICKEN3.jpg

Kwa mtazamo wangu kwa waanzaji wanaotaka kupata
uzoefu kufanya majaribio kwa kuanza na kuku wachache
kutosha ili kujua mbinu na mambo muhimu ya kuwa makini
ni bora kuliko kuanza mradi mkubwa bila uzoefu na mambo
yakishindikana ni kuingia hasara kubwa ya pata
maumivu ya siyotarajiwa kichwani.

Hata hivyo kama nilivyosema hapo juu bora kuanza na kuku wachache kama mabanda yalivyo hapo juu kupata uzoefu namna ya kuwatunza na kuwatibu hali kadhalika kujenga mazoea ya kuandaa mchanganyiko wa chakula wewe mwenyewe. Uzoefuu huo utasaidia kujua mbinu muhimu unapoamua kupanua mradi huo.

Kuna ndugu yangu mmoja alianza hivyo na banda nyumbani kwake kwa kuku 50, alipofanikiwa akawa na 100, kisha akafikisha mia tatu. Ameshapata uzoefu sasa anahamishia mradi shambani kwake ambako analo eneo kubwa na hewa safi kwa kuku.

Mpango mzima wa mradi mkubwa kwa mara ya kwanza unahitaji kujipanga sana na pia kuwa na capital ya kutosha si mradi kuwa na kuku, na pengine kuwa karibu na wataalamu ambao watasaidia kwa ushauri na mengineyo na hao wataalamu si bure ni biashara kwa kwenda mbeleee..
 
View attachment 155748 View attachment 155749 View attachment 155750

Ni kweli mkuu uzoefu ni wa muhimu, Na sehemu pekee ambapo mtu anaweza pata uzoefu wa kufuga ni kupitia yeye mwenyewe kuanza kufuga, na si vinginevyo, theory na practical mara zote huwa zinapingana.

Hayo Mabanda mbona kama ya kimamtoni vile, Mimi nilipata elimu ya kujenga mambanda ya kuku kutoka Kenya, kwa kweli jamaa wanajenga mabada simple ile mbaya yaani Bnada la kuku 1000 haliwezi hata gharimu 2000000, nilitembelea na ni kaona na nilijilamua sana kuingia gharama kujenga mabanda kumbe kuna njia za gharama fupi na kwa sasa mambanda ni nayo yajenga ni simple sana,
 
Asante kwa taarifa, pengine ningeweza kufikiria kwa waanzaji wengi vema wakashika mpango mzima wa kuanza na kiwango cha kima cha chini kwa kununua kuku wachache tetea kadhaa na majogoo kama wawili au watatu na mpango mzima wa kuangulisha vifaranga kwa kuku mchanganyiko au wa kienyeji. Kwa kuku wa kisasa ambao huhitaji mtangao wa kuangulisha hakuna jinsi ni bora tu kuyavulia maji nguo yaogwe.

Kwa bei hiyo dhahiri ufugaji kuku kibiashara bora kuanzia kiwango cha chini na 500 vinginevyo hakutakuwa na faida ya kutosha chini ya hapo.

Ila mimi nashauri mtu aanze na vifaranga hapo ndo unapata elimu vizuri na unaweza kuwa contro mwenyewe,
 
Mpango wa kuku iwe wa nyama au mayai hasa wa kisasa bora tu kununua vifaranga maana kuanglisha mwenyewe ni ghali kwa vile unahitaji mtambo wa kuangulisha, hiyo kuwa na mtambo wa kuanglisha kwa mtazamo wangu ni mpango wa kibishara zaidi kwa uuzaji vifaranga na unatakiwa uwe na kuku wanaowiana kwa kuwa na majogoo ya kutosha tofauti na wa mayai na nyama mradi una kuku we wakuze na kuuza majira wakishakua au kutaga mayai.

Mabanda niliyoweka ni kama kuleta tu taswira, wengi wetu wanao uwezo wa kujenga mabanda yao binafsi kwa gharama nafuu, uko sahihi kabisa.
 
kwa banda la kuku wa kienyeji 200 linaweza kugharimu kiasi gani na liwe na ukubwa gani @ Candid Scope?
 
Back
Top Bottom