Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji na Masoko yake

kwa ufugaji wa huria kila mita moja mraba kuku kumi hadi kumi na tano na kwa ufugaji wa nusu huria kwa kila mita ya mraba kuku wanne hadi watano
 
Ngoja nipambane niingize bandani kama ishirini 25 au 30.
 
Tuko umenigusa, naomba uniambie products zenye vitamin majina yake nizitafute dukani, maana nataka kuku wangu wawe na kiini cha njano.... please please please!!

majani mzazi yanasaidia sana kiini cha mayai
njano
 
Eligi,
Dawa inaitwa neoxyvital.
Nenda duka la dawa za mifugo utapatiwa, ni bora uwaeleze wauzaji wakupe ushauri kama kuna ingine.
Hiyo tajwa ina cost 6000/= in Arusha.
 
Nina banda LA ukibwa wa ft 17x24
Litaingiza kuku wa kienyeji wangapi.....
 
Mkuu Kubota na wengine wanajamii, kiukweli nimepata degree ya ufugaji kupitia hii thread!! nimetenga pesa kiasi cha 500000 kwa ajili ya kuanza kujenga banda la kawaida maana bati ninazo km 20 na nitakapokamilisha nahtaji kuanza na kuku 12 tu ilhali nimepata somo kubwa sana hapa. Nitarudisha feedback humu jamvini muda ukifika maana kwa sasa bado nipo chuo nashika kesi na vifungu vya sheria lkn ufugaji its my hobby i MUST make sure naifanya kuwa business idea yngu! Shukran sana wakuu.
 
Kubota,
LiverpoolFC
Mama joe
Mama Timmy
guta
asigwa,
ANKOELI
mutuwa wali
Micah 28
Raisi wa walala hoi
Ugolo wa bibi
Poutry sayuni
Reti
Chamilitary
na wengine wengi....

Heshima kwenu wote.

Kwanza kabisa nichukuwe fursa hii kipekee kumsukuru bw. Kubota kwa kazi nzuri ya kuelimisha na kutoa on practical experience ya ufungaji wa kuku. nimefarijika sana na elimu yake. [ Ingawa sikubaliani naye katika biashara ya Mikaa]

Pili niwashukuru wadau wote hata wale niliowasahau majina kwa michango mingi mizuri na ya kusisimua yenye kuelimisha jinsi bora ya kufuga kuku wa kienyeji.

Tatu napenda kuwajulisha kuwa kazi yenu haijaenda bure kwangu kwani nimetengeneza vitabu 42 vyenye kurasa 12-14 kila moja kutokana na michango yenu. Nilichofanya nilisave kila page kwa page zote 42 mpaka sasa kwenye pdf . kisha nika print vitabu 42 nilivovi baind na kuviita " Kubota local poutry farm hands experience " .

Nimeaanza mradi wa kuku wa kienyeji kwenye plot yangu nikiwa na kuku 10 mitetea 5 na jogoo 5" lengo likiwa kutengeneza project kwenye Farm yangu ya ekali 5.

Napenda tu kujua Tangu nimewachukuwa mwezi wa 4 mpaka sasa ni mwezi na sioni dalili ya kuku yoyote kuanza kutotoa ... nini inaweza kuwa Tatizo... Kuna watu wanasema kipindi cha baridi kuku hawatotoi je ni kweli?

wadau leteni michango yenu ... huku nikiendelea kusoma taratibu vitabu vyangu...

Kila la heri

Muonamambo
 
Napenda kuchukua frusa hii kumushukuru Mungu kwa kunipa uwezo wa kusoma na kuelewa! pia naushukuru uongozi wa jamii forum na members wote! nieleze kwa nn nimeamua kutoa shukrani zangu. Mwaka jana tar 8/4/2014 nilikutana na mada inayo zungumuzia kuhusu ufugaji wa kuku wa kienyeji. nilihamasika sana! tar 15/4/2014 nilianza kufuga kuku. nilianza na kuku 15 lakini hadi sasa ninapoandika habari hii! nina kuku mia 200 wakubwa. pia nimenunua mashine ya kutotoresha vifaranga yenye uwezo wa kuchukua mayai mia 900. kwa sasa nauza vifaranga. asanteni sana wadau wa jamii forum wakimo akina Gazeti na wengine Mungu wa mbinguni awabariki sana!
 
Ahsante kwa mrejesho mkuu.
 
hongera sana mkuu na mimi najiandaa kufuga kuku wa kienyeji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…