Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji na Masoko yake

Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji na Masoko yake

Kubota,
LiverpoolFC
Mama joe
Mama Timmy
guta
asigwa,
ANKOELI
mutuwa wali
Micah 28
Raisi wa walala hoi
Ugolo wa bibi
Poutry sayuni
Reti
Chamilitary
na wengine wengi....

Heshima kwenu wote.

Kwanza kabisa nichukuwe fursa hii kipekee kumsukuru bw. Kubota kwa kazi nzuri ya kuelimisha na kutoa on practical experience ya ufungaji wa kuku. nimefarijika sana na elimu yake. [ Ingawa sikubaliani naye katika biashara ya Mikaa]

Pili niwashukuru wadau wote hata wale niliowasahau majina kwa michango mingi mizuri na ya kusisimua yenye kuelimisha jinsi bora ya kufuga kuku wa kienyeji.

Tatu napenda kuwajulisha kuwa kazi yenu haijaenda bure kwangu kwani nimetengeneza vitabu 42 vyenye kurasa 12-14 kila moja kutokana na michango yenu. Nilichofanya nilisave kila page kwa page zote 42 mpaka sasa kwenye pdf . kisha nika print vitabu 42 nilivovi baind na kuviita " Kubota local poutry farm hands experience " .

Nimeaanza mradi wa kuku wa kienyeji kwenye plot yangu nikiwa na kuku 10 mitetea 5 na jogoo 5" lengo likiwa kutengeneza project kwenye Farm yangu ya ekali 5.

Napenda tu kujua Tangu nimewachukuwa mwezi wa 4 mpaka sasa ni mwezi na sioni dalili ya kuku yoyote kuanza kutotoa ... nini inaweza kuwa Tatizo... Kuna watu wanasema kipindi cha baridi kuku hawatotoi je ni kweli?

wadau leteni michango yenu ... huku nikiendelea kusoma taratibu vitabu vyangu...

Kila la heri

Muonamambo


Lakini mkuu mbona umenunua majogoo wengi sana?

Ngoja niwaite
@Kubota , LiverpoolFC Mama Joe Mama timmy guta asigwa, AnkoELI Mutuwa wali micah 28 raisi wa walala hoi ugolo wa bibi
@Poutrysayuni
@Reti chamilitary
 
Kuku wangu katoka na watoto nje huku wengine wakiwa hawajiwezi maana wamevunja wenyewe mayai na kutoka. Mama yao hawapi joto kama inavyotakiwa na nimeamua kuwawekea taa kuona kama itasaidia.
 

Attachments

  • 1432473194720.jpg
    1432473194720.jpg
    18.1 KB · Views: 498
Kama kutakuwa na mtu wa kunisaidia kuokoa vifaranga vyangu maana vipo kumi na tano jamani.

"Nlikuwepo":bolt:
 
Pia ili uwe na mafanikio ni lazma lazma ujitahidi kusafisha vifaranga wengi na speed kali, TUMIA incubator yenye ubora mkubwa ili kuepuka kaharibu mayai na incubator zisizo na ubora... Nina incubator za kiwango cha juu sana,yenye uwezo wa kutotolesha 100%....na yenye uwezo wa kutumia battery ya gari, solar power na umeme wa kawaida... Zipo za mayai kuanzia 28, 42,84 na 210
...Check out 0717169816 whatsapp only na isayasalathiel@gmail.com au ni PM
 

Attachments

  • 1432615425692.jpg
    1432615425692.jpg
    37.7 KB · Views: 632
Nina banda LA ukibwa wa ft 17x24
Litaingiza kuku wa kienyeji wangapi.....
 
Habari ndugu wafugaji wenzangu.

Naomba msaada wa kuelekezwa dawa kabambe ya kuua viroboto katika banda la kuku wa kienyeji na viroboto vilivyowapamba kuku wenyewe.

Asanteni sana
 
Amani iwe nanyi!Nikitambo sijachangia uzi huu sio kwa sababu sikuwa na interest nao la hasha!Kwa kipindi kile uzi huu ulikuwa kama functionless kwangu kutokana na mazingira yangu hayakunuruhusu kabisa kufuga kibiashara ingawa nilikuwa natamani kufuga.Nikaona ni busara niweke uzi huu mkuu kama hazina hivyo kuamua kujiweka bize kutafuta njia za kujikwamua na mazingira yale,katika njia za kufanikisha hilo nimejukuta kwa miaka miwili iliyo pita nimepitia katika wakati mgumu na maisha yakukatisha tama sana ndugu wana jf hatahivyo,namshukuru MWENYEZI MUNGU kwa sasa ninavyo andika hii post nipo mahali ambapo naweza kufuga na kuwekeza katika miradi mingine,na nimeanza kufanya hivyo kwani hivi sasa nina kuku wakubwa kumi na nne na vifaranga kumi na tatu napia natarajia mnamo tarehere mbili mwezi huu kuwa na vifaranga wengine 25-30 kwani kuna kuku watatu wamelalia mayai thelathini.Nafikiri huu ndio umekuwa wakati wangu muafaka wa kutafuta hazina yangu ambayo ni hii thread,nashukuru kwa sasa uzi una michango mingi tofauti na hapo awali nilipo ishia ulikuwa na pages 13 ila kwa sasa una pages 43 naomba niwapongeze kwa hilo na naomba msikate tamaa kutuelimisha.Nimesomo pages zote na sasa nitaendelea kutoa mrejesho wa maendeleo ya ufugaji wangu ingawa ni mvivu kidogo kuandika ila nitajitahidi kadri ya uwezo kwa hili kuhakikisha nami natoa nilichokipata kwa manufaa ya wenzangu.MUNGU akubariki Kubota MUNGU awabariki Mama Joe,Chasha, Liverpoolfc,MamaTimmy,Guta,Fidel80,Aza,Asigwa,Chamilitary,Ankoeli,Poutry Sayuni na wengine wote ambao nimewasahau.
 
Back
Top Bottom