Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji na Masoko yake

We hapo umeshatobozea, jitahidi dawa tu, mimi niliwahi kufuga kuku wakafika 57, nikajisahau kuendeleza dawa, kilicho nikuta kila siku nikawa nakula kuku tatu hadi nne nanyingine kutupa, toka hapo hadi leo sijajipanga kufuga ingawa moyo ninao,pia kama una alovela wapatie uwezavyo ila isichukue zaidi ya siku nne mwaga na weka tena, pia otc ya unga inasaidia, pia dawa ya viroboto hakikisha viroboto haviwapati, safisha banda kila siku, hapo watasema unadawa, pamoja mkuu
 

Asante sana mkuu kwa kunitia moyo na ushauri wako nitaufanyia kazi.
 

Usituletee mambo ya jukwa la mapenzi na facebook huku tafadhali. huku ni serious brains tu.
 
Hongera sana kwa mada nzuri. lakini mimi nina sikitika sana mazingira ninayoishi hataufanyeje huzi kupata kitu kama pumb
 
Habari wafugaji!
Naitaji mayai ya kuku wa kienyeji kwa ajiri ya kutotolesha nipo dsm,naitaji tray 10.
Kama unayo ni pm tufanye biashara.
 
Usituletee mambo ya jukwa la mapenzi na facebook huku tafadhali. huku ni serious brains tu.

Ndo maana watoto huwa hawaruhusiwi kuchangia mijadara ya wakubwa. Umefanya jambo la maana kumpa ukweli wake.
 
Habari wafugaji!
Naitaji mayai ya kuku wa kienyeji kwa ajiri ya kutotolesha nipo dsm,naitaji tray 10.
Kama unayo ni pm tufanye biashara.
Vipi mayai ya kienyeji ya kula tu huitaji??
 
Kifaranga wangu mmoja wa wiki 3 alitoka njee ya uzio akaenda kuzurura, nliporudi jion nkamrudisha ndani. Kesho yake narudi jion tena namkuta anasinzia then akafa the next day. Sasa naona wale wengine aliokua nao banda moja nao wameenza kusinzia, no vidonda wala mafua. Ni ugonjwa gani huu.
 
Jamani mimi niko kigoma yote mnayosema kusu sijui dawa,vyakula hapa nilipo havipatikani na mm nina ham ya kufuga ushauri
 

Mimi ni mtalaamu wa mifugo niko kisarawe nitafute tusaidiane...0764717755
 

Itakua mdondo kitalaam ni new castle angalia dalili zingine ili upate uhakika wa jinsi ya kulikabiri....ila mara zote kumbuka kuwachanja kuku wako hata kama unawafungia
 
Eti wadau yai likichafuliwa na kinyesi halifai tena kutotolewa?na je likisafishwa kwa maji litafaa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…