Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji na Masoko yake

Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji na Masoko yake

Asante ndugu. Tatizo lingine ni utunzaji wa vifaranga. Mimi nina banda kubwa lakini vijana wanaoangalia kuku wameshindwa kulea vifaranga. Kuku akitotoa vifaranga 15 vinavyokuwa ni 5 au hata chini yake.
 
Pia mkuu Kubota kadri navyorudia kusoma soma huu uzi kuna maswali mengine yanazidi kujitokeza utanisamehe kwa hilo.

Kuhusu suala la JELA, kuku wanaokuwa wamekwisha atamia na kutotoa vifaranga nao unaweza kuwapeleka JELA ili kuwaachisha vifaranga?

Vifaranga vikishafika wiki nne au mwezi mmoja unaweza kuviachisha kwa mama yao kwa nguvu, je hapa napo JELA hutumika kuviachisha au kuna mbinu mbadala?
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Kubota naomba kukuuliza swali ambalo litakua linarudi nyuma kidogo....

Mfano nikiamua kuwalaza kuku wakubwa kwenye banda moja na wakawa wanatumia banda hilo hilo katika utagaji, wakimaliza kutaga nakusanya mayai na kuyahifadhi sehemu tofauti na yalipotagiwa na nikigundua kuku ameanza kuatamia namwekea mayai kwenye kiota cha kuatamia halafu namuhamisha banda na kumuweka kwenye banda la pili maalumu kwa kuatamishia je huyo kuku muatamiaji hawezi kuyasusia mayai kama akikuta alipozoea kutagia mayai yake yamehamishiwa kwenye banda jingine??

Au anaweza kuvamia viota vingine vya kuku wengine ambao bado wanataga na kuanza kuyatia joto mayai ya kuku wengine??

Thanks in advance

Mkuu Asigwa, swali lako ni zuri na jibu lake litanufaisha wasomaji wengi. Ukigundua kuku ameanza kuatamia iwapo mayai ulikuwa unayakusanya, unapoamua kumwekea mayai, mimi nilikuwa moja kwa moja ninamhamishia na kumwekea mayai kwenye chumba atakakoatamia. Na shughuri hii niliifanya usiku.

Kwa hiyo vyovyote utakavyofanya, zoezi la kumhamisha lifanyike usiku asishuhudie anavyohama na ili kufikia asubuhi awe amenogewa kuatamia asijisikie kuyaacha mayai. Ukisoma kwenye maelezo yangu utaona niliandika kwamba kwenye ile staili yangu, kuku niliowaweka kwenye chumba cha kuatamia walikuwa hawatoki nje kabisa. Nilikuwa nawawekea humo humo maji na chakula. Usipofanya hivyo, ukimhamisha kuku usiku, kesho yake asubuhi akienda kula akishiba ni rahisi yeye kurudi kwenye banda la zamani kwenye kiota chake cha kutagia alichozoea. Alishaji-condition hivyo. Kuzuia hilo ndo maana nilikuwa siwaruhusu kutoka nje nikiwahmishia kwenye chumba cha kuatamia.

Pia niseme hapa kwamba bado kuna kuku wajanja au tuwaite wakorofi, ukiwahamishia kwingine ukawawekea mayai wanashituka hawakalii mayai. Inakuwa imekula kwako! Hizo mara chache zilikuwa zinatokea, nilichokuwa ninafanya kama ikitokea hivyo kwa vile kunakuwa kuna kuku aliyekosa mayai na nimeshamsweka JELA ninamtoa na kumpa fursa aatamie hayo mayai ambayo mchizi mwingine ameyakataa. Ni juu ya mfugaji kuwatambua kuku wapole na wakorofi ili kujua jinsi ya kuwatumia au kuwaepuka kila mmoja kulingana na tabia yake. Mimi hili halikunipa shida nilikuwa naona raha tu. Kama kuna kitu hujaelewa hapa usisite kuulizia tena. Karibu.
 
Asante ndugu. Tatizo lingine ni utunzaji wa vifaranga. Mimi nina banda kubwa lakini vijana wanaoangalia kuku wameshindwa kulea vifaranga. Kuku akitotoa vifaranga 15 vinavyokuwa ni 5 au hata chini yake.

Tafadhari Mkuu Mabaghee iwapo vijana wameshindwa kulea vifaranga kwa sababu wanakosa maarifa hebu pitia thread hii kwa makini chukua yale utakayoona umeyaelewa waelimishe na uwasimamie kuhakikisha wanajenga mazoea kufuata utaratibu huu. Uzembe wa vijana unatokana na mambo mengi sana tumia ubunifu wako kuona kuwa wanavutiwa kujishirikisha na mambo ya uzalishaji mali. Hakuna asiyeweza kujifunza jambo. Wape motisha waone watakavyonufaika na ufugaji huo. Saa zingine tunadhani kwa vile ni vijana wetu basi watajituma tu la ni lazima uweke namna ya kuwafanya wawe na sababu ya kujituma. Hapo ni ubunifu wako sasa. Lakini kama ni utaalamu hapa JF ni choka mwenyewe!!
 
Pia mkuu Kubota kadri navyorudia kusoma soma huu uzi kuna maswali mengine yanazidi kujitokeza utanisamehe kwa hilo...

Kuhusu suala la JELA, kuku wanaokuwa wamekwisha atamia na kutotoa vifaranga nao unaweza kuwapeleka JELA ili kuwaachisha vifaranga??,

Vifaranga vikishafika wiki nne au mwezi mmoja unaweza kuviachisha kwa mama yao kwa nguvu, je hapa napo JELA hutumika kuviachisha au kuna mbinu mbadala???

Swali lako Mkuu Asigwa linadhihirisha kuwa umeamua kufanya kitu na kwa hiyo uko makini ili kila kitu ukakifanye kwa ukamilifu. Nakupongeza kwa umakini wako.

Kama kuku ametotoa vifaranga na vifaranga umeshawahifadh mahali ambapo hawezi kuwafikia na hatoi bughudha huna haja kumsweka JELA. Isipokuwa unaweza kuwa umehifadhi vifaranga sehemu ambayo Mama yao ameshaifahamu na hivyo watoto wanamsikia Mama akilia nje na yeye Mam anawasikia watoto wakilia kwa ndani hapo itabidi huyu Mama umpige JELA maana bila kufanya hivyo watoto huko ndani hawatakula na Mama huku nje hataondoka nae pia hatakula, lakini wakati mwingine unaweza kumpuuza tu muda ukienda sana pengine anaweza kuishia zake. Akiendelea kusumbua piga JELA tu.

Vifaranga wakati wa kuvitenganisha na Mama yao nimebatiza tuwaite VINYOYA maana wanakuwa wameota manyoya ya ukubwani, mara nyingi hutokea baada ya wiki 4 hadi sita. Mimi nilikuwa nimetengeneza banda la kwa ajili ya vinyoya tu. Kwa hiyo vinyoya wakiwa tayari kutenganishwa na Mama yao niliwahamishia kwenye banda la vinyoya. Mama yao sikumfunga JELA. Uzuri vinyoya ni wakubwa kwa hiyo watapiga kelele kwa muda fulani baadae mama yao anaisha zake na vinyoya wanaendelea kula chakula. Zikipita wiki mbili ndani ya banda la vinyoya unaweza kuwaachia kuanza kuzurula na hapo Mama yao anaweza kuwa ameshaanza kutaga mayai kwa hiyo JELA haitumiki kabisa.
 
Habari ya siku nyingi wadau, Kubota nashukuru kw amichango zaidi hasa ya matumizi ya mbwa na mitego ya panya itanifaa sana. Nilipotea kidogo majukumu si unajua ajira.

Kuhusu kutengeneza chakula bado kwa kweli mimi kuku wangu wote ni chotara hivyo nitategemea zaidi incubator wakianza kutaga maana sasa hivi ndio vinyoya wale pilot 10 ni wachache sana kuwatafutia incubator. Lakini bado nafuatilia kwa ukaribu mafunzo ya kutengeneza chakula, kisha nitaanza kuwazoea wenye mashine wanaotengeneza ili niibe maujanja kwao. Ninategemea itachukua muda tuwe na subira, Nimemsoma Chasha kuhusu kupeleka sample Naivasha ingawa nami niliiona kwa mtandao, nataka nijue kama hawa watengenezaji wengine wanafanyaje. Kazi njema wadau wote wa kuku.
 
Jamani nahitaji kuanzisha biashara wa kuku wa kisasa naombeni ushauri nataka nianze na kuku mia moja.
 
Kubota
Mama Joe
Mama timmy
guta
chasa
Dafo
asigwa
MABAGHEE

Na wadau wengine wote wa jukwaa letu! Niwasalimu wote katika Jina lake Bwana wetu! Hakika nimepotea kama wiki mbili kisa nilikuwa katika mambo ya kilimo kwani ndiyo majira yake huku nilipo. Na kwa uweza wake MUNGU mwenye mamlaka ya yote hakika nimeenda na kurudi salama!

Hakika vinyoa vyote vilivyo totolewa tar 25/02/2013 vyote wana afya njema na viko 45 na vyote vipo kabisa! Na hata hivyo vimeongezeka kama 37 na wote wanaendelea vema kabisa na wanaungana wote wanakuwa 82 na hata hivyo ukiviona unatamani usibanduke hapo walipo kwa afya waliyonayo.
Ila wamekuwa wakitumia starter tu kwani ile Chick marsh niliikosa mahala nilipoenda kutafuta!

Hakika humu jamvini ukizingatia masharti yote utaona mambo yanavyoenda kama unavyotaka!

Ngoja nitarudi muda si mrefu!

LiverpoolFC umepotelea wapi? Ukimaliza kuwanywesha dawa vinyoya wako njoo umwage update mkuu! Ha ha haaa
 
Last edited by a moderator:
Kubota Mama Joe Mama timmy guta chasa Dafo asigwa MABAGHEE Na wadau wengine wote wa jukwaa letu! Niwasalimu wote katika Jina lake Bwana wetu! Hakika nimepotea kama wiki mbili kisa nilikuwa katika mambo ya kilimo kwani ndiyo majira yake huku nilipo. Na kwa uweza wake MUNGU mwenye mamlaka ya yote hakika nimeenda na kurudi salama! Hakika vinyoa vyote vilivyo totolewa tar 25/02/2013 vyote wana afya njema na viko 45 na vyote vipo kabisa!

Na hata hivyo vimeongezeka kama 37 na wote wanaendelea vema kabisa na wanaungana wote wanakuwa 82 na hata hivyo ukiviona unatamani usibanduke hapo walipo kwa afya waliyonayo. Ila wamekuwa wakitumia starter tu kwani ile Chick marsh niliikosa mahala nilipoenda kutafuta! Hakika humu jamvini ukizingatia masharti yote utaona mambo yanavyoenda kama unavyotaka! Ngoja nitarudi muda si mrefu!
Dah mkuu unanitamanisha sana na hao vinyoya wako aisee natamani na mie niwaone naweza kupata shule nzuri sana practically. Mkuu huezi kutupia picha angalau moja mbili mkuu?? Halafu nomba kutupia kijiswali, hivi mfuko mmoja wa starter au chicken marsh weye unautumiaga siku ngapi mkuu?
 
Last edited by a moderator:
Aisee hii sred nimeipenda sana, nimetumia almost siku nzima kusoma kila kitu, ila naamini imelipa kwa upande wangu. Nimejifunza mambo mengi sana. Namshukuru sana mleta mada Kubota na wachangiaji wote, pamoja sana!
 
Naaaaaam! asigwa hakika nakwambia ya kwamba mfuko wa starter nanunua kg 25 na natumia kwa mwezi Kama mmoja na hata na nusu
asigwa umenipata?
 
Last edited by a moderator:
Niko sehemu mbaya mtandao unasumbua. Darasa linanipita sana ila bado tuko pamoja sana.
 
Aisee hii sred nimeipenda sana, nimetumia almost siku nzima kusoma kila kitu, ila naamini imelipa kwa upande wangu. Nimejifunza mambo mengi sana. Namshukuru sana mleta mada Kubota na wachangiaji wote, pamoja sana!

Mkuu mito nami kwa niaba ya wachangiaji wote wa thread hii tunashukuru kama imelipa kwa upande wako maana hilo ndiyo lengo letu na kwako limetimia kwa hiyo tunafurahi sana kututia moyo! Wadau endeleeni kuchangia, na kuuliza maswali maana kwa kufanya hivyo wengi wananufaika zaidi! Huu uzi tusiuachie usinzie!
 
Naaaaaam! asigwa hakika nakwambia ya kwamba mfuko wa starter nanunua kg 25 na natumia kwa mwezi Kama mmoja na hata na nusu
asigwa umenipata?

Asigwa lakini Mkuu LiverpoolFC angetueleza Kg 25 analisha vifaranga wangapi, ingetusaidia mimi nimesahau idadi ya vifaranga vyake, mnaonaje hapo?
 
Asigwa lakini Mkuu LiverpoolFC angetueleza Kg 25 analisha vifaranga wangapi, ingetusaidia mimi nimesahau idadi ya vifaranga vyake, mnaonaje hapo?
Ni kweli nimesahau kumuuliza ni vifaranga wangapi bana, maana isije kua ni viwili.
 
Asigwa lakini Mkuu LiverpoolFC angetueleza Kg 25 analisha vifaranga wangapi, ingetusaidia mimi nimesahau idadi ya vifaranga vyake, mnaonaje hapo?
Ni kweli nimesahau kumuuliza ni vifaranga wangapi...Ila nahisi ni kama 82 hivi kulingana na post yake hapo juu.
Mkuu LiverpoolFC njoo utujibu bana huku eti hizo KG 25 unalisha vifaranga/vinyoya wangapi kwa mwezi mmoja?
 
Last edited by a moderator:
Kuhusu wale Kuku wa Israeli jamaa naona wanakuwa wagumu kuuza Bongo sijui why, Ila kuna wafugaji binafisi huko huko Kenya walio nao na ndo nafanya nao mpango wa kuwapata kutoka kwao.
 
Back
Top Bottom