Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu Kubota naomba kukuuliza swali ambalo litakua linarudi nyuma kidogo....
Mfano nikiamua kuwalaza kuku wakubwa kwenye banda moja na wakawa wanatumia banda hilo hilo katika utagaji, wakimaliza kutaga nakusanya mayai na kuyahifadhi sehemu tofauti na yalipotagiwa na nikigundua kuku ameanza kuatamia namwekea mayai kwenye kiota cha kuatamia halafu namuhamisha banda na kumuweka kwenye banda la pili maalumu kwa kuatamishia je huyo kuku muatamiaji hawezi kuyasusia mayai kama akikuta alipozoea kutagia mayai yake yamehamishiwa kwenye banda jingine??
Au anaweza kuvamia viota vingine vya kuku wengine ambao bado wanataga na kuanza kuyatia joto mayai ya kuku wengine??
Thanks in advance
Asante ndugu. Tatizo lingine ni utunzaji wa vifaranga. Mimi nina banda kubwa lakini vijana wanaoangalia kuku wameshindwa kulea vifaranga. Kuku akitotoa vifaranga 15 vinavyokuwa ni 5 au hata chini yake.
Pia mkuu Kubota kadri navyorudia kusoma soma huu uzi kuna maswali mengine yanazidi kujitokeza utanisamehe kwa hilo...
Kuhusu suala la JELA, kuku wanaokuwa wamekwisha atamia na kutotoa vifaranga nao unaweza kuwapeleka JELA ili kuwaachisha vifaranga??,
Vifaranga vikishafika wiki nne au mwezi mmoja unaweza kuviachisha kwa mama yao kwa nguvu, je hapa napo JELA hutumika kuviachisha au kuna mbinu mbadala???
LiverpoolFC umepotelea wapi? Ukimaliza kuwanywesha dawa vinyoya wako njoo umwage update mkuu! Ha ha haaa
Dah mkuu unanitamanisha sana na hao vinyoya wako aisee natamani na mie niwaone naweza kupata shule nzuri sana practically. Mkuu huezi kutupia picha angalau moja mbili mkuu?? Halafu nomba kutupia kijiswali, hivi mfuko mmoja wa starter au chicken marsh weye unautumiaga siku ngapi mkuu?Kubota Mama Joe Mama timmy guta chasa Dafo asigwa MABAGHEE Na wadau wengine wote wa jukwaa letu! Niwasalimu wote katika Jina lake Bwana wetu! Hakika nimepotea kama wiki mbili kisa nilikuwa katika mambo ya kilimo kwani ndiyo majira yake huku nilipo. Na kwa uweza wake MUNGU mwenye mamlaka ya yote hakika nimeenda na kurudi salama! Hakika vinyoa vyote vilivyo totolewa tar 25/02/2013 vyote wana afya njema na viko 45 na vyote vipo kabisa!
Na hata hivyo vimeongezeka kama 37 na wote wanaendelea vema kabisa na wanaungana wote wanakuwa 82 na hata hivyo ukiviona unatamani usibanduke hapo walipo kwa afya waliyonayo. Ila wamekuwa wakitumia starter tu kwani ile Chick marsh niliikosa mahala nilipoenda kutafuta! Hakika humu jamvini ukizingatia masharti yote utaona mambo yanavyoenda kama unavyotaka! Ngoja nitarudi muda si mrefu!
Aisee hii sred nimeipenda sana, nimetumia almost siku nzima kusoma kila kitu, ila naamini imelipa kwa upande wangu. Nimejifunza mambo mengi sana. Namshukuru sana mleta mada Kubota na wachangiaji wote, pamoja sana!
Mama Timmy, Mama Joe, Guta, Dafo na wakuu wengine mapambano vipi huko? Mmepotea wakubwa!Niko sehemu mbaya mtandao unasumbua.darasa linanipita sana ila bado tuko pamoja sana
Ni kweli nimesahau kumuuliza ni vifaranga wangapi bana, maana isije kua ni viwili.Asigwa lakini Mkuu LiverpoolFC angetueleza Kg 25 analisha vifaranga wangapi, ingetusaidia mimi nimesahau idadi ya vifaranga vyake, mnaonaje hapo?
Ni kweli nimesahau kumuuliza ni vifaranga wangapi...Ila nahisi ni kama 82 hivi kulingana na post yake hapo juu.Asigwa lakini Mkuu LiverpoolFC angetueleza Kg 25 analisha vifaranga wangapi, ingetusaidia mimi nimesahau idadi ya vifaranga vyake, mnaonaje hapo?